NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania

Verified Member
Joined
Sep 13, 2014
Messages
93
Points
150

NMB Tanzania

Verified Member
Joined Sep 13, 2014
93 150
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
 

KIMWAMU

Member
Joined
Jun 29, 2012
Messages
25
Points
45

KIMWAMU

Member
Joined Jun 29, 2012
25 45
NMB mobile Service nawapongeza kwa huduma zenu kwani zinatusaidia. MAKALAMIKO YSNGU KWENU NI PALE MNAPOKATA FEDHA ZA MTEJA KUTOKA SALIO LAKE KWENYE SIMU HATA PALE AMBAPO MUAMALA HAUJAKAMILIKA. Mfano, mteja anataka kununua muda wa maongezi, kutokana na tatizo la kiufundi kutoka NMB muamala hujakamilika. Sasa kwa nini MKATE FEDHA WAKATI HUDUMA HAIKUKAMILIKA?
 

namba force

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2017
Messages
707
Points
500

namba force

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2017
707 500
Nina shida kwenye Nmb mobile kwenye sehemu ya Nikopo.Nikiomba Salary advance inasema niende na kitambulisho Nmb branch.Nimeenda wakaniambia niwape salary slip na kitambulisho cha kazi lakini bado tatizo liko pale pale.Naomba mnisaidie.Naomba ikiwezekana mnitumie namba zenu za wasap nitume salary sleep na Kitambulisho cha kazi. Jina la akaunti ni John Yohane,Account no 51010013034. check no 111664825,85T3 5008,85T3-002.Natuma kitambulisho chino.
Hili tatizo limekuwa sugu.Kama wameishiwa pesa waseme
 

Atoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Messages
62,577
Points
2,000

Atoto

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2013
62,577 2,000
Nina shida kwenye Nmb mobile kwenye sehemu ya Nikopo.Nikiomba Salary advance inasema niende na kitambulisho Nmb branch.Nimeenda wakaniambia niwape salary slip na kitambulisho cha kazi lakini bado tatizo liko pale pale.Naomba mnisaidie.Naomba ikiwezekana mnitumie namba zenu za wasap nitume salary sleep na Kitambulisho cha kazi. Jina la akaunti ni John Yohane,Account no 51010013034. check no 111664825,85T3 5008,85T3-002.Natuma kitambulisho chino.
Duuuh!! Umejilipua haswa. Why usiwatumie hizo details pm? Au ndio vyuma kukaza
 

Katali

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2016
Messages
309
Points
250

Katali

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2016
309 250
Leo yamenikuta nimekwenda kwenye ATM moja katika jiji la Mwanza na kutaka kutoa shs.400000/=ajabu pesa haijatoa wala hata risiti pia haijatoka lakini nimetumiwa meseji kwamba nimetoa kiasi hicho cha fedha kuangalia salio nikaona wamekwisha kata pesa! Mbaya zaidi nilikuwa na dharura ambayo kukosa pesa hizi kumenifanya nipate hasara kubwa. Swali langu je, nikifungua madai kutokana na usumbufu nilioupata nitakuwa na cause of action? Au njia gani ya kunirudisha nilipokuwa? Au ni halali kwa bank kujifanyia wapendavyo katika kutunza pesa za mteja? Je, pesa yangu ipo salama?
 

ABIBU CHENGULA

Senior Member
Joined
Oct 15, 2017
Messages
155
Points
225

ABIBU CHENGULA

Senior Member
Joined Oct 15, 2017
155 225
Mie mnanikera sana NMB. Hivi kwanini mteja anakuja kwenye tawi lenu, ana bili au sijui niseme vocha ambayo tayari amepewa kwenye ofisi ya serikali, hiyo karatasi inakuwa ina control number, lakini bado mnataka mteja ajaze tena zile karatasi zenu za benki za kuwekea hela. Kwanini hamfanyi kama CRDB mkaweka hela kwa kutumia ile karatasi ya bill aliyonayo mteja kutoka ofisi husika ya serikali. Mnaboa sana aiseee!!!
Nenda kwa Wakala wa NMB hayo mambo hutayaona,kwakuwa wewe no mvivu wa kuandika Fanya hivo
 

Forum statistics

Threads 1,356,328
Members 518,876
Posts 33,130,647
Top