NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania

Verified Member
Sep 13, 2014
93
150
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
 

masai dada

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
14,023
2,000
habari naomba msaada NMB nilikua natoa ela ikazunguka like 10 mints bila kutoa nika cancel then kadi ikatoka ila ela haikutoka lakini msg ikaonesha kwamba ela imetoka
sasa huduma kwa wateja hata hawapokei.msaada plz
 

NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
28,005
2,000
Mie mnanikera sana NMB. Hivi kwanini mteja anakuja kwenye tawi lenu, ana bili au sijui niseme vocha ambayo tayari amepewa kwenye ofisi ya serikali, hiyo karatasi inakuwa ina control number, lakini bado mnataka mteja ajaze tena zile karatasi zenu za benki za kuwekea hela. Kwanini hamfanyi kama CRDB mkaweka hela kwa kutumia ile karatasi ya bill aliyonayo mteja kutoka ofisi husika ya serikali. Mnaboa sana aiseee!!!
 

Jua usiyoyajua

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
1,139
2,000
NMB Mandela Road branch Manager wenu ni tatizo kubwa, yule mama ni kiburi, customer care ni O+, hana majibu mazuri kwa wateja fanyeni atoke haraka iwezekanavyo. Nahisi kuna mkubwa anaeyejivunia.
 

Mzolewa

Member
Dec 15, 2016
34
95
NMB Klik mimi sielewi baada ya kufanya update haifunguki baada ya kuweka password, shida iko wapi?
 

uujn

Senior Member
Mar 24, 2019
198
250
Tabia yenu mtu amemaliza mkopo kisha mnaendelea kumkata mnakera sana...mkifuatwa mnajibu eti tulikosea mahesabu deni lilikuwa bado halijaisha...hilo linakera zaidi na ninalichukulia ni utapeli tu
 

namba force

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
712
500
Hivi loan advance NMB mmesitisha?????
Maana toka asubuhi hakuna kitu jibu ni kwamba tembelea tawi lolote ukiwa na kitambulisho
 

Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
61,383
2,000
Wako wapi NMB kujibu maswali humu?
NMB Tanzania ni janga kama yalivyo majanga mengine. Nilijitoa hili libenki kwa tatizo la kitoto sana. Nashangaa mpk leo wananisumbua na vimeseji vyao wakati niliwakacha nikiwaachia zaidi ya 400K.

Kuwa mteja wa NMB unapaswa kuwa na kichwa chenye IQ ndogo kama ya nyau
 

Ilongailunga

JF-Expert Member
Jan 18, 2012
1,268
2,000
Kwanini mnatuletea usumbufu, tulishajaza vendor forms na kupitia kwa waajiri wetu na mkazihakiki, sasa tena mnatuambia tukahakiki kadi zetu kwenye tawi hamuoni huu ni usumbufu kwa wateja? Kwani mtu anawezaje kuwa na kadi feki?
 

BUMIJA

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
3,382
2,000
Nina shida kwenye Nmb mobile kwenye sehemu ya Nikopo.Nikiomba Salary advance inasema niende na kitambulisho Nmb branch.Nimeenda wakaniambia niwape salary slip na kitambulisho cha kazi lakini bado tatizo liko pale pale.Naomba mnisaidie.Naomba ikiwezekana mnitumie namba zenu za wasap nitume salary sleep na Kitambulisho cha kazi. Jina la akaunti ni John Yohane,Account no 51010013034. check no 111664825,85T3 5008,85T3-002.Natuma kitambulisho chino.
 
Top Bottom