Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Vionjo vya Arsis 4 Kumwokoa Msukule Unguja 1 .

kama nilivyoahidi. Hiki kisa ni cha kusikitisha sana. Hii dunia ina hatari, kisa hiki kimetokea kama miaka 16 iliopita.

Siku hio mamangu mzazi alikwenda Zanzibar na wenzake kundi zima, waliletewa habari usiku, kua kuna binti kigori kafa ghafla baad ya kuumwa kuchqa kwa muda mfupi.

Kuna rafiki ya mamangu mzazi kaolewa kwenye ukoo huo na mjomba wa huyo binti, alipopata habari usiku huohuo akawajulisha habari ya kifo watu wa karibu, ikabidi mamangu na rafiki zake wengine wandoke nae alfajiri kuwahi maziko, waliondoka wao na ndege ndogo ya kukodisha, wengine kundi kubwa walienda na boti za asubuhi.

Walipofika Unguja wakaenda moja kwa moja wakaenda mpaka nyumba ya msiba wakawa ni kama wametokea palepale Unguja tu, watu wanajazana na wao wapo hapo. Kikatokea kitu cha ajabu sana, lakini Mwenyezi Mungu akitaka jambo lake liwe hakuna wakulizuwia. Kuna mama mmoja mtu mzima aliyekuja masibani akamwita mama mzazi wa yule binti aliyefariki pembeni. Akamwambia.

Mtu mzima; Mama pole sana, lakini nakuomba msihimize kumuosha huyu mtoto, mimi naona kama kuna mchezo umefanyika hapa, mbona hio sio maiti hapo? Usimwambie mtu, fanya hima na mimi kuna mazee namjua nakwenda kumwambia yupo ng'ambo. Yule bibi akatoka. Yule mama akabaki analia kwa kwikwi. Watu wanafanya maandalizi aoshwe, yule mama akamwita yule wifi yake amabae ni rafiki wa mamangu pia akamweleza alivyoambiwa na yule bibi, akamsisitiza asiseme kwa mtu yeyote wa pale, lakini maiti isioshwe mpaka yule bibi arudi.

Yule rafiki wa mamangu akmatonya mamangu, mamangu, unajua mambo ya wanawake tena, akatoka nje akampigia simu babu yangu tanga, saa hio hio. Babu yangu akmwabia nipe nusu saa nitakupigia. Babu akafanya mamboi yake akanipigia simu, kama saa tano hivi akanieleza alivyopigiwa simu, akanambia fanya hima uende Unguja lakinimwite Arsis uongee nae hili jambo.

Mimi kwa msisitizo wa babu na mamangu yuko kule nikamwita Arsis, ikaja sauti yake tu kama kawaida, akanambia usiwe na waiwasi, sisi na majeshi yapo kule. Wewe nenda kesho mpema usiende leo. Leo usiku tuonane pale mlangoni. Sehemu yetu ya kukutania Arsis alikua aniita mlangoni.
Mimi: Nikamwambia sawa lakini roho hainipi. Nikarudi nyumbani nikaingia ofisini kwangu, nikamwita Jini 1. Hakuchelewa akaja, live, tukasalimiana pale.
Jini1; Mbona una wasiwasi, mambo yapo vizuri.
Mimi; Najua mpaka sasa unafahamu kinachoendelea. Arsis kanambia nisiende leo kwanini?
Jini1; Tena babu yako kishaongea nao Unguja huko, kawaambia waoshe wazike tu leo hii, kama kawaida, wafanye kama hawajui kitu.Yule mama kazuiliwa hukohuko kwa mganahga wake asirudi mazikoni na mganga wake. Kwa hio huko mambo yanaendelea kama kawaoida na leo saa 10 wanazika, mpaka kaburi limeshachimbwa maiti imeshaoshwa watu wapo kama kawaida.
Mimi: Na huyo binti vipi?
Binti: Yupo palepalee kwao kafichw kichawi, hakuna anaemuona lakini yeye anaona kila kitu, leo watakuja kumchukua usiku sana kabla ya alfajiri, ndio watafatwa washikwe wpoyte ili huo ufisadi ukomeshwe, si unajua mambo ya Arsis?
Mimi; Sasa mi si niende leo?
Jini1; Wewe ukienda leo unaweza ukapatwa na hasira utaona kinachoendelea, tuwachie sisi tupo huko, hivi mama yupo huko, Bakora yupo huko na mimi nilikua huko msibani. Niwache niende, wewe mapema sana nenda usiwe na shaka kazi zitakungoja wewe, hakuna wa kuifanya hii kazi kabla wewqe hujafika, kunamajeshi huko si mchezo. Arsis anasisitiza usiku ukaonane nae.

Ikabidi nitulizane, nikawa na mawazo mengi na nanona muda haufiki, nikampoigia mama, akanambia huki maiti imeshaoshwa na watu ni wengi sana wanawake kwa wanaume, wanangoja muda ufike wakazike.
Mimi: Sikuonge mengi, ikabidi nikubali matokeo.


usiku kama kawaida nikaenda mlangoni nikamwita Arsis. Siku nyingi ilikua sijaenda. Nikakuta kuna mabadiliko ya majengo, ujenzi unaendelea, uwanja umejifinya kidogo.

Arsis: Vipi hali simba?
Mimi: Kama ujavyo, mimi niko poa.
Arsis: Usiwe na wasiwasi. SAema.
Mimi; Niseme nini Arsis na wewe ndio umeniita nije hapa?
Arsis: naona una maswali mengi na una hofu.
Mimi; Kawaida tu, hayo mambo ya Unguja vipi?


Arsis: kwanza leo nimekuita kuna viumbe nataka kukujulisha nao, au unaogopa?
Mimi; Niogope nini?
Arsis: Unaona ile miti mwili ipo nyuma yako?
Mimi; Ndiyo.
Arsis; Ile miti ya zamani sana usiione midogo, ile mbegu waliipanda Wajerumani ya kwao huko, ile miti ni shida sana kufa, ikishashika ardhi, inakaa miaka mingi sana na inakua kidogokidogo sana, jhaikatwi na mtu ile kabisa, hata wakijenga hapa, ipo pale na ipo humo ndani Ikulu. Unaijua kazi yake nini?

Nikawa najiuliza huyu Arsis kaniita kunieleza habari ya miti?

Mimi; Siijui kazi yake.

Arsis; kwanza kacheka, kazi yake hio ni alama, alama ya miaka mingi sana ijayo, wamaoijua wanajua alama ipi. Usiwe na wasiwasi, nataka uelewe hilo. sasa tazama kwenye ile miti, unaona nini?

Mimi kutazama nikaona kuna watu wawili, mmoja mrafu kiasi ana mwili mpana mpna sio mnene lakini, na mmoja kavaa tshirt ya mikono mirefu na jeans, nikamweleza Arsis ninachoona.

Arsis; sawasawa, huyo mmoja ni binadam kama wewe na mmoja ni jinni. Nebda kawasalimie ujuane nao. Usiogope.
Mimi: Siogopi kitu.
Arsis; Haya nenda halafu urudi.

Nikaenda nikapeana nao mikono, yule aliyevaa kanzu alikua ana mikono mipana sio kawaida. Yule mewingine alikua kama mimi tu, sema anainesha kazisi umri. Tukasalimiana, yule binge la mtu akasema sisi tunakujua siku nyingi, wewe ndio hujatuona kabla.
Mimi: Nyie kina nani?
Binadam: Sisi wanafunzi wa Arsis kama wewe.

Mimi nikashangaa , kwa sababu Arsis hajawahi kunambia kama ana wanafunzi.
Mimi; Mnaishi wapi?
Jini mubwa; Sisis tunaishi inapotupeleka kazi, sisi wote wanafunzi wa Arsis lakini mimi ni mwanajeshi, huyu mwenzangu ni mwanafunzi w udaktari, sasa hivi anachukua shahada ya juu.
Mimi; Mmesema mnanijua, mona siwajui wala sijawahi kuwasikia?
Jini Mkubwa; Tulikua hatukutakiwa utujue, tulijulishwa tu kua na wewe ni mwanafunzi wa kipekee wa Arsis.

Jini Mkubwa; twende tukatembee, hutaki kwenda Ikulu ndani ukapaone pakoje?
Arsis: Njoo Simba usiende mahali, haya nyie kwaherini, mtakua nae pamoja leo.

Itaendelea.
 
Kuna tatizo nimeku-quote mara nyingi nyuma huko na post number nimekutumia upitie zile post.
Ukiona kimya ujue bado sina jibu la kukupa, usichoke kunikumbusha, unipe siku mbili au tatu kunikumbusha. Ningekua sina nia ningeshakwambia nimeshindwa. Lakini nia yangu ni kila mwenye tatizo limuondokee, au kwa njia yangu au ya mwengine. Tumuombe Mwenyezi Mungu atufanyie wepesi.

Mwamba mwenyewe anatusoma hapa, angekua kishanikumbusha, hapendi ukiritimba kabisa. Anajua anafanya nini.
Simba.
 
Je , Nini Tiba ya macho kutoona vizuri baada ya kuondoshwa sihri? Je Kuna Tiba yoyote nikutumie, nitaanza kuona kama mwanzo ?
👇
Hakuna ugonjwa usiokua na tiba.

Pima sukari mwilini.
👇
Ahsante.
Sukari yangu ipo okay. nikipata changamoto hiyo nikiwa nasoma miaka 10 ilopita na kupata matibabu miaka 3 imepita ila macho hayajaweza Rudi kama zamani tena.

Kunayo Tiba waweza nisaidia ?

Nitashukuru.
👇
Simba atakuelekeza ufanye nini wasilina nae hapahapa.
Simba nimeambiwa Kuna kitu utanielekeza.
Msaada wako tafadhali.🙏
👇
Kuanzia Jumatatu nikumbushe.
Simba.
👇
Amani iwe juu yako Simba.
Naam, kuhusu Ile dawa uliniambia nikukumbushe kuanzia Leo.
Ahsante.
Arsis
👇
Ahsante.

Tutawasiliana hapa hapa baadae.
Simba:
👇
kama hujapata jibu basi hilo swali linamuhusu Arsis atakuja kujibu. Kama linanihusu mimi niulize tena.
Simba.
👇
Okay..

Swali nilishauliza na jibu nilijibiwa kwamba utanielekeza wewe ......na asubuhi post yako number 1342 umenijibu.

Imetokea post yako number 1068.

Arsis alinijibu post number 1038 baada ya kuuliza swali post number 1023.

Natumaini nimerefer vizuri umenielewa vzr.
👇
Nitazirudia posts hizo, nione yunafanyaje.
Simba.
👇
Kuhusu nini?
Simba.
👇
Kuna tatizo nimeku-quote mara nyingi nyuma huko na post number nimekutumia upitie zile post.
Natumaini mpaka hapa umenielewa.🙏
Arsis
 
Sasa mbona umekazana kusoma anachokiandika kama sio level nzima ya upanganga na upumbavu fool. Acha atoe ya sirini mnayoyatumia kuumiza watu. Unatetemeka siri zenu kuwekwa uchi. Kima wewe
We ni mjinga promax! Ngoja nikutungie kisa kingine nikuletee uendelee kuwa mjinga zaidi. Dunia ya leo sikuwahi kudhani watu kama myie bado mpo!
 
Alafu muda tu naona haya mabishano ya ukristo na uislamu kitu ambacho hakikuwa lengo la uzi sasa mimi na declare kuwa MIMI NI MUISLAMU sikuwa nataka kuingia kwenye mabishano ya dini ila kwakuwa tunatakiwa tupeane elimu basi nahitaji mkristo ambaye anataka kujifunza sio mabishano, nataka anayetaka elimu tu kuhusu dini yake ambaye huko kanisani hawaisemi aje nianze mjadala nae.
Nitaanza na msingi wa imani ya kikristo ipo hivi ili dini iwe dini lazima iwe na msingi wa imani sasa msingi wa imani wa uislamu ni Monotheism yaani Mwenyezimungu ni mmoja tu, naye ni ALLAH, msingi wa Ukristo ni Polytheism japo wengi huwa hawataki wakijificha katika kivuli cha Mungu mmoja katika utatu mtakatifu kwani wakikubli kuwa ukristo ni polytheism yaani kuami miungu wengi ni sawa na kusema kuwa ukristo ni upagani hivyo hawataki wanajificha kwenye mungu mmoja mwenye nafsi tatu what is this?
Sasa nijibuni haya maswali ya utatu mtakatifu
1. Je, Mungu ni watatu katika umoja na ni mmoja katika watatu kwa wakati mmoja au ni mmoja kwa wakati huohuo?
2.Ikiwa mungu ni mmoja na watatu kwa wakati mmoja, Hivyo hakuna hata mmoja kwa hao watatu ambae ni mungu kamili.Tukikubali kuwa huo ndio ukweli maana yake wakati yesu yupo duniani hakuwa mungu kamili, Na baba mbinguni hakuwa mungu kamili. Je hili halileti mkanganyiko pale yesu aliposema Baba ni mkuu kuliko yeye katika YOHANA 14:28 yesu aliposema ...kwa maana baba ni mkuu kuliko mimi, Sasa baba atakuwaje mkuu na haja kamilika?
3.Ikiwa Mungu ni mmoja na watatu kwa wakati mmoja je nani aliyekuwa mungu huko mbinguni kati ya zile siku za kusulubiwa na kufufuka?
Tuanzie hapa kwa leo.
Yani elimu ya Ukristo niichukue kwa muabudu majini!? Hauwezi kuwa serious.
 
Kuna anayopingana hata na masheikh.

Hapingani na vitabu anapingana na tafsiri za vitabu. Torati anasema haipo kabisa, kuijua Torati mpaka upewe elimu hio na Muumba wetu.
Simba.
Kitu nilichokigundua kutoka kwake, elimu yake ni kama yangu na yako.. ina mipaka kuna mengi anayaelewa ndivyo sivyo.
 
Kitu nilichokigundua kutoka kwake, elimu yake ni kama yangu na yako.. ina mipaka kuna mengi anayaelewa ndivyo sivyo.
Tupe mfano wa hicho ndivyo sivyo na sisi tufaidike. Maana wengine tunaona kama muujiza huu.

Hio ndiyo sivyo inawezekana wewe upo sahihi zaidi au yeye yupo sahihi zaidi. Ndio usomi huo, au usomi wako wa kuficha ficha kama Kanali_

Arsis kamsifu, mwenyewe anamuita, Sheikh, Che mittoga
Simba.
 
Tupe mfano wa hicho ndivyo sivyo na sisi tufaidike. Maana wengine tunaona kama muujiza huu.

Hio ndiyo sivyo inawezekana wewe upo sahihi zaidi au yeye yupo sahihi zaidi. Ndio usomi huo, au usomi wako wa kuficha ficha kama Kanali_

Arsis kamsifu, mwenyewe anamuita, Sheikh, Che mittoga
Simba.
Yeye mwenyewe majibu yake hayapo moja kwa moja anafichaficha.

Naomba anijibu kwanza yeye ni nani (ana cheo gani katika viumbe), maana huwezi kuwa kila kitu kama anavyodai yeye, kila kitu kina uhalisi wake.

Pia akiri kwamba haelewi kila kitu( jibu liwe ni NDIO au HAPANA).
 
Majini yalikuwepo hata katika ukristo,mfalme sauli alienda kwa mwanamke wa kike kutaka kupata ufumbuzi kutoka kwa pepo

1 Samweli 28:6-8
[6]Lakini Sauli alipouliza kwa BWANA, BWANA hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii.
And when Saul enquired of the LORD, the LORD answered him not, neither by dreams, nor by Urim, nor by prophets.
[7]Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori.
Then said Saul unto his servants, Seek me a woman that hath a familiar spirit, that I may go to her, and enquire of her. And his servants said to him, Behold, there is a woman that hath a familiar spirit at Endor.
[8]Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye na watu wawili pamoja naye, wakamfikilia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako.
And Saul disguised himself, and put on other raiment, and he went, and two men with him, and they came to the woman by night: and he said, I pray thee, divine unto me by the familiar spirit, and bring me him up, whom I shall name unto thee.
Bado unatolea mifano kwenye dini hizohizo za kuletewa! Umeambiwa kabla ya kuja hizo dini hakukuwa na habari za majini ila mizimu ya wazee tu na mambo yalienda...hizo dini zenu ndo zimetuletea majini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom