Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Basi nilivyoendelea kusoma vitabu vya Wakristo na Waislamu, nilikuja kugundua kuwa.
Waislamu wana ukaribu sana na Majini.
Hadi kufikia kulindwa na Majini na wakapewa Sura nzima ya Majini kwenye kitabu chao cha Qurani.
Wakafikia Hadi kuitana ndugu.

Nikagundua kuwa Wakristo wanaukaribu sana na Malaika, na kufikia kulindwa na Malaika.
Wakristo:
Zaburi (Psa) 91:11
Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.

Waislamu:
Mas'ud reported God’s messenger as saying, “Do not cleanse yourselves with excrement or bones, for that is the provision of your brethren among the jinn.”

Nikatafakari na kuona Wakristo wako karibu na Mwenyezi Mungu na Malaika zake.

Waislamu na Majini wako mbali na Mwenyezi Mungu.

Katika Uislamu kumejaa sana habari za Majini, Majini Majini. yaani hao akina Arsis, na wengine.
Ni nadra sana na ni kama hakuna kabisa habari za uhusiano wa Malaika na Waislamu katika mafundisho ya Waislamu.

Basi nikaona ni Bora niwe Mkristo, kama kuna habari ngeni niwaulize Malaika tofauti na Waislamu wanao wauliza Majini ambao walisha fukuzwa Mbinguni kwa kumwasi Mwenyezi Mungu.
...........
وَأَنَّا لَمَسْنَا السَّمَاءَ فَوَجَدْنَاهَا مُلِئَتْ حَرَسًا شَدِيدًا وَشُهُبًا
(AL - JINN - 8)
Nasi tulizigusa mbingu, na tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu na vimondo.
وَأَنَّا كُنَّا نَقْعُدُ مِنْهَا مَقَاعِدَ لِلسَّمْعِ ۖ فَمَن يَسْتَمِعِ الْآنَ يَجِدْ لَهُ شِهَابًا رَّصَدًا
(AL - JINN - 9)
Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini sasa anaye taka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia!
وَأَنَّا ظَنَنَّا أَن لَّن نُّعْجِزَ اللَّهَ فِي الْأَرْضِ وَلَن نُّعْجِزَهُ هَرَبًا
(AL - JINN - 12)
Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani, wala hatuwezi kumponyoka kwa kukimbia.
.............
Hizo Aya zinathibitisha kuwa Majini waliwahi kuishi Mbinguni na yakafukuzwa kwa uasi wao na yakitaka kuchungulia Mbinguni yanapigwa na walinzi wa huko(Malaika) kwa nguvu ya vimondo.

Mtoa mada:
Mwulize Arsis, mosi,ni kwa nini alifungwa miaka zaidi ya 900 na bila kulindwa na Mungu wake.

Pili, ni kwanini hana uwezo tena wa kwenda mbingu aliko kuwa anaishi hapo awali.

Tatu, ni kwanini alifukuzwa Mbinguni hadi akaishi katika Dunia aliyoishia kufungwa kwenye chupa.
Cc FaizaFoxy,
Ukitaka kupata elim usiwe na haraka... Haya mambo yanahitaji utulivu wa hali ya juu!!

Halafu usipende kuweka vitabu mbele kwenye kila jambo,,, unakuwa umejiwekea ukuta kupata elim
(Hiyo biblia unayoiamini kupita kitu chochote kasome vizuri history yake.... Baada ya kupotea kwa miaka 600 warumi waliipeleka wapi, kasome mwenyewe uelewe haya mambo yamekaaje


Halafu nan kakwambia waislam hawako contact na malaika 🤔


Sisi tumepewa elim ambayo walotutangulia kwenye imani hawakuwa nayo...... Sisi tunaelim yenu yote ila nyie hamna elim yetu🤝

Maana muislam anasoma Taurat , Zaburi na Injili.... Tafsiri yake yeye anajua vyote kuwahusu ila ukristo haujui chochote kuhusu Qur'an

Note: Mungu kawaumba wanaadam ili wamuabudu.....

Haya turudi kwenye structure ya ibada kwa mwezi mzima

JUDAISM 👉 Wanaswali mara 90 mwez mzima (mara 3 kwa siku)

Wakristo👉 Wanaswali mara 4 kwa mwezi

Waislam 👉 Wanaswali mara 150 kwa mwezi

(We unadhani kwa akili tu ya kawaida ni kina nani hapo walio bora zaidi mbele za Mungu?
Maana ubora wa mtu zaidi ya mwingine unaletwa na kufanya ibada sana)


Anyway sipendelei sana kubishania mambo ya kidini hapa.... Ila tuheshimu hizi dini zetu jamani!!!
Wengine tukisikia dini yetu imetukanwa roho inakosa amani

Bwana Simba akizungumza chochote hapa, hii haina uhusiano wowote na uislam🤝
Kwahyo unapozungumzia uislam na kuusema vibaya sababu ya maneno ya mtu unakosea Sana!!!!

Pia yeye amna sehemu kahusisha uislam kwenye uzi wake, yeye anatoa mkasa wake wenye mazingatio na elim na alhamdulillah watu wanapata elim..... Mbona mnapenda chokochoko🚶🚶🚶
 
Wana ukumbi, kwanza inabidi nicheke maana Arsis kanipa ujumbe baada ya mimi kuanza kusoma posts. Ninacheka kwa sababu Arsis leo kanipa ujumbe kwa Kingereza, niwaambie wana ukumbi "they've opened the can of worms".

Akanipa maagizo nisijibu mtu leo mpaka baadae, mimi niendelee na kisanilioanza kukiandika jana lakini niwe mwangalifu "dont spill it, spell it".

Wana ukumbi nisaidieni kamaanisha nini, ujumbe wa kwanza wenu wa pili wangu. Leo Arsis anapiga "ngeli" tu.
Hilo la kwanza anamaanisha "wameanzisha mambo wasiyokuwa na ujuzi nayo".

La pili hilo ujumbe kwa simba "asikosee maandishi, ayamwage kama yalivyo".

Huyo Mtemi anazidi kunishangaza.
 
We Simba kwasababu gani unayakwepa majukum yako.... Humu Sasa hivi kila mtu anakutizama kwa jicho la mkombozi kwenye matatizo yake...... Lakini Arsis anasema wewe uko busy na kutengeneza magari😴😴

Arsis kasema unaweza kuwasaidia watu humu ukiamua wewe na jinn bakora
Watu hawana nguv za kiume, watu wanasaratani, watu wanamashetwan, watu washajikatia tamaa ya maisha😭😭

Watizame kwa jicho la huruma... Ni kweli most of them hawana tena sehemu ya kupata msaada
Naunga mkono hoja, kama tiba anazijuwa kwanini watu wateseke?
. Simba tunataka majibu. Wewe unaona magari yana maana sana kuliko binadam wenzako?
 

Tofauti yetu na wazungu kwenye haya mambo ni objectivity. Nenda kwenye YouTube channel ya huyo jamaa usikilize interview zake na wasomi wanao amini haya mambo.

Ukikutana na wazungu wenye imani ya ‘sixth sense’ achana na wakawaida nazungumzia wasomi wenye doctorates na Phd za science maelezo yao ni tofauti na waganga wa Tanzania.

The way hawa watu wanavyotafsiri ‘Plato Repulic’ esoterically au meaning ya vitabu vya ‘Karl Jung’ kwenye hoja hizi hizi it makes you think. Especially when they use those arguments to their own life experiences and attempt to justify with their science knowledge (that includes archeology findings).

Sina maana hawa walimu wetu wa bongo hawana wanachojua Iła chumvi nyingi sana. Hivi tukimtafuta huyu mjomba na fimbo yake tukamwambia ailaze chini itanyanyuka kweli mbele ya ushahidi. Si hadithi tu hiyo sasa kama unaweza ongopa kitu cha wazi mangapi mengine kaongopa.
 
Basi nilivyoendelea kusoma vitabu vya Wakristo na Waislamu, nilikuja kugundua kuwa.
Waislamu wana ukaribu sana na Majini.
Hadi kufikia kulindwa na Majini na wakapewa Sura nzima ya Majini kwenye kitabu chao cha Qurani.
Wakafikia Hadi kuitana ndugu.

Nikagundua kuwa Wakristo wanaukaribu sana na Malaika, na kufikia kulindwa na Malaika.
Wakristo:
Zaburi (Psa) 91:11
Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.

Waislamu:
Mas'ud reported God’s messenger as saying, “Do not cleanse yourselves with excrement or bones, for that is the provision of your brethren among the jinn.”

Nikatafakari na kuona Wakristo wako karibu na Mwenyezi Mungu na Malaika zake.

Waislamu na Majini wako mbali na Mwenyezi Mungu.

Katika Uislamu kumejaa sana habari za Majini, Majini Majini. yaani hao akina Arsis, na wengine.
Ni nadra sana na ni kama hakuna kabisa habari za uhusiano wa Malaika na Waislamu katika mafundisho ya Waislamu.

Basi nikaona ni Bora niwe Mkristo, kama kuna habari ngeni niwaulize Malaika tofauti na Waislamu wanao wauliza Majini ambao walisha fukuzwa Mbinguni kwa kumwasi Mwenyezi Mungu.
...........
وَأَنَّا لَمَسْنَا السَّمَاءَ فَوَجَدْنَاهَا مُلِئَتْ حَرَسًا شَدِيدًا وَشُهُبًا
(AL - JINN - 8)
Nasi tulizigusa mbingu, na tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu na vimondo.
وَأَنَّا كُنَّا نَقْعُدُ مِنْهَا مَقَاعِدَ لِلسَّمْعِ ۖ فَمَن يَسْتَمِعِ الْآنَ يَجِدْ لَهُ شِهَابًا رَّصَدًا
(AL - JINN - 9)
Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini sasa anaye taka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia!
وَأَنَّا ظَنَنَّا أَن لَّن نُّعْجِزَ اللَّهَ فِي الْأَرْضِ وَلَن نُّعْجِزَهُ هَرَبًا
(AL - JINN - 12)
Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani, wala hatuwezi kumponyoka kwa kukimbia.
.............
Hizo Aya zinathibitisha kuwa Majini waliwahiNaam,hi Mbinguni na yakafukuzwa kwa uasi wao na yakitaka kuchungulia Mbinguni yanapigwa na walinzi wa huko(Malaika) kwa nguvu ya vimondo.

Mtoa mada:
Mwulize Arsis, mosi,ni kwa nini alifungwa miaka zaidi ya 900 na bila kulindwa na Mungu wake.

Pili, ni kwanini hana uwezo tena wa kwenda mbingu aliko kuwa anaishi hapo awali.

Tatu, ni kwanini alifukuzwa Mbinguni hadi akaishi katika Dunia aliyoishia kufungwa kwenye chupa.
Cc FaizaFoxy,
Naam, umeniita?

Hizo porojo zako ntakujibu mstari mmoja mmoja, hoja mfu hizo hazina mashiko.

Kwanza jibu alivyosema Arsis jana kuhusu wewe. Au umeshajibu sijaliona jibu lako?
 
Naam, umeniita?

Hizo porojo zako ntakujibu mstari mmoja mmoja, hoja mfu hizo hazina mashiko.

Kwanza jibu alivyosema Arsis jana kuhuasu wewe. Au umeshajibu sijaliona jibu lako?
Tatizo lako husomi.
Arsis, alinitabilia na mimi nilimkubalia utabiri wake kuwa ni sahihi kabisa.
Tatizo lako husomi unaendeshwa na mihemuko ya Kidini tu.
إقرأ أيها المسلم المؤمن
'iiqra 'ayuha almuslim almumin
 
JUDAISM 👉 Wanaswali mara 90 mwez mzima (mara 3 kwa siku)

Wakristo👉 Wanaswali mara 4 kwa mwezi

Waislam 👉 Wanaswali mara 150 kwa mwezi

(We unadhani kwa akili tu ya kawaida ni kina nani hapo walio bora zaidi mbele za Mungu?
Maana ubora wa mtu zaidi ya mwingine unaletwa na kufanya ibada sana)
Mkristo anasali kila siku, asubuhi na jioni hata usiku pia, hiyo usemayo wewe ni katika mapumziko ya juma... Imani ya mtu huwa bora ikiunganishwa na matendo mema. Hivyo kusali sana na imani bila matendo mema ni bure kabisa.
 
Babu yangu alijaaliwa maarifa siku nyingi sana. Alijichagulia hiyo sehemu ambayo watu wote walikua wanaiogoppa. ikawa kajichagulia katikati ya matawi mawili ya mto ambayo yote,a yanatoa kamba kwa wingi wakati wa msimu, lile tawi kubwala mashariki na lile lenye mapango ya kiajabu, yote yapo kwenye eneo la shamba lake. Ule mto wa Mashariki ndio kwa upande wa pili jamii wanapata kuvuna msimu wa kamba, mto ule ndio mpaka wa shambani kwetu, huu mto wa Magharibi ni tawi dogo tu lisilokauka, linapita katikati ya shamba letu, mapango mawili makubwa moja ni kama ukumbi tu mkubwa, hayakutani kwa ndani, yote yapo ndani ya shamba letu.

Mji wa babu bado wanakaa wana familia au wanafunzi wanaokuja hapo mpaka leo hii.

Ukifika kuanzia mpakani horohoro mpaka unafika Duga maforoni ukiuliza Mzee mabruki kwake wapi, unaletwa hata na mtoto mdogo. Babu wengi wanafikiri Mbaruki ni jina lake, lakini ukweli ni kua kuanzia anafanya kazi Tanga 'Mabruki" ulikua ni msemo wake mkubwa, akimaanisha kupongeza kila zuri utaloilfanya,anakupongeza kwa kusema "mabruk" basi ikashika ndio likawa jina lake "Mzee Mabruki". Ukija Duga Maforoni tuna kwetu, vizazi vya Mzee Mabruki mpaka kesho. Lakini kwa Mzee Mabruki alipo ni kule shamba, baharini kwenye kamba wa kufa mtu. Qengi wanajua anakaa Duga mjini, hawajui pale ni kwake anakuja kwa shughuli zake tu, lakini makazi yake hasa ni kule shamba.

Kamba wa kufuga ilishindikana kabisa kule. Walikua na kazi kubwa sana, babu akasema sina hamu nao, hawa wa msimu wanatutosha na pesa zake hatuzimalizi. Ndio miradi ya kuvuna kamba kwa mwaka mzima ikaishia kwa kauli hiyo ya babu. Sasa kuna misimu miwili tu, msimu mkubwa na mdogo, na kila msimu una aina tofauti ya kamba. Miuiiza ya Muumba wetu hio.

Mpaka kesho, misimu yote ya kamba, nakua shmbani kwetu, navuna kamba tu.
Hiv huyu Mzee Mabruki co ndio mmiliki wa mabasi ya bin nasoro pale maforoni karibu na mckiti wa mashia?
 
Ilikuwa ni siku chache kabla sijatimiza miaka 18. Nilipelekwa Tanga, kijiji kimoja kipo karibu sana na mpaka wa kwenda Kenya. Kabla ya kuingia huko kijijini ndani kuna ki mji kinaitwa Duga. Ilikua sio mara yangu ya kwanza kupelekwa huko kwa mambo ya kimila na jadi.

Lakini hii ya safari hii ilikua kidogo yakutisha. Kijiji chenyewe kipo ufukweni kabisa na kina mito miwili inapita, mmoja Kaskazini mashariki ya kijiji, huu mkubwa kiasi na mmoja mdogo unapita kusinii ya kijiji. Kwa hio kijiji ni kama kimezungukwa na maji, maana mashariki yake ni bahari ya hindi, Kaskazini mto na kusini mto. Magharibi tu ndio kuna njia ya kwenda mpaka barabara kubwa ya lami, ambayo ipo kama kilomita 3 au 4 kutokea hapo kijijini.

Safari hii ilikua ni nzito kidogo kwa sababu niliambiwa unaweza kukaa kijijini huko wiki moja au mbili, itategemea na "babu" huko ataamua kama mambo yako tayari au bado.

Nilifatana na Baba na Mama yangu kwenye gari la nyumbani mpaka hapo barabara kuu kutokea Tanga, hapo nikakuta vijana wawili wakubwa kwangu, wananingoja na baiskeli mbili, moja ya kunipakia mimi na moja ya kupakia mizigo yangu.

Mizigo yangu kweli ilikua mingi, yangu binafsi lilikua ni begi kubwa na racksack ya mgongoni, lakini kuna maboksi kama matatu makubwa yalikua ya mama akanambia haya yote mkabidhi babu yako mkifika.

Basi tukaagana pale, wao wakanambia ukimaliza kazi yako watakuleta hapa barabarani utapanda gari za kuja Tanga, sisi utatukuta Tanga, tutakuja baada ya wiki mbili, kama utakua umemaliza kabla ya wiki mbili ukifika Tanga tusubiri. Wakaondoka zao, na mimi nikapakiwa kwenye baiskeli kama abiria, na nyingine ikafungashwa ile mizigo yetu yote, ikatangulia.

Hatukuchukua muda sana, tukafika kijijini, moja kwa moja mpaka kwa babu yangu. Babu yangu tunajuana sana, na alikua ni sahiba yangu sana, ni mtu ma story ya kizamani na mimi nilikua mdadisi sana. uzuri wa babu alikua hakwepi swali lolote utalomuuliza na alikua hamumunyi maneno, anakujibu mpaka likuingie. Nilikua namshangaa sana, kwani hakuna swali lilililokua gumu kwake.

Hata niwe na swali, mwenyewe naliona gumu kweli, nikimuuliza babu ananijibu huku ananisifia "swali zuri sana hilo", ananijibu kiurahisi kabisa, mengine huwa anachukua muda kuyajibu, mtindo wake wa kuibu ulikua kama anakusimulia hadithi, anaweza akatoka kabisa nje ya swali ulilomuuliza lakini atakuhadithia mpaka utalipata jibu. Mara nyingi akikujibu basi lazima utakua na maswali mengine mawili matatu ya kuuliza. Kwa ufupi alikua anaelewa kufungua "kichwa" kwa mujibu baba yangu.

Tutaendelea baadae.
Eti Arsis hivi kwanini Waarab tu ndiyo majini / misukule? Na huku kwetu utakuta jini ni mwanamke wa kiswahili aliye na maisha duni na muislam. Kila kukicha analilia wanaume wa wenzake wenye uwezo ili wamnunulie chips kuku au vitenge vya wax.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom