- Thread starter
- #1,321
Uchokozi huo.Nenda MOI.
Au ngunga hizo?
Simba.
Uchokozi huo.Nenda MOI.
Au ngunga hizo?
Yesu alikua ana ngozi kama Wahabeshi au Wasomali. Siku hizi mnawaita wakushi.Ni kwamba Arsis Yesu mwenyewe anajishangaa? Vipi muulize Arsis kama Yesu alikuwa ana ngozi nyeusi kweli ama ni stori tu? Vipi mchekeche akuoneshe picha halisi ya Yesu.
Unaposema athari unamaanisha nini?Dah ndio sababu mwenyewe nilishangaa sana nilipoisikia sauti yake....... Haina athari hata kidogo!!!
Watu wenye elim na maqam kiibada huwa wanaathari sababu ya uchamungu wao🤝
Dada angu aliniandama Sana nilipomwambia ndugu yake hana elim ya majinn ni kama anasikia tu kwa watu🤔🤔
Hapa umefanya nikuamini wewe na Arsis zaidi🚶🚶
Mimi elim yangu n ya kubahatisha bahatisha hivihivi
Nnajifunza mengi hapa
Hata mm hii habar nishawahi kuisikia piaYesu alikua ana ngozi kama Wahabeshi au Wasomali. Siku hizi mnawaita wakushi.
Simba.
Wacha na Mimi nifuatilie hayoKuwa na shaka ni akili. Lakini muhim ni ama umeelewa ama hukuelewa.
Hata mimi kuna baadhi ya mambo simuelewi, nitam'uliza.
Sema kuna mambo manne kanimaliza kabisa, inabidi nimfatilie.
Kuhusu Yesu na Adam. Kwa sababu hayo nineshaandika articles zake zamani hapa JF. Halafu kuhusu watu wawili alivyowajibu humu, ni kitu cha ajabu.
Na leo nimemsoma simba akisema kuhusu majinni wa kibuki ambao wapo Comoros na Japan na wote wapiga maji. Hilo la comoro sio geni kwangu kakini hilo la Japan limeniwacha hoi, nimeingia jwenye mtandao kulitafuta, dah! Sina la kusema zaidi kwa sasa.
Kuhani mose, siku hizi sikusikii sana ukipaza sauti yako ya kitume kuitangaza ile dini au Imani yako mpya.
Unaweza kutukumbusha.
Inaitwaje.
Na misingi yake ni ipi.
Mtume yupi alitufahamisha? Ushahidi.Kuna ishu imezuka hapa kwamba katika qur'an au hata biblia kuwa hakuna aya ambayo inasema adam ndio mwanadam wa kwanza
Lakini nadhan wote tunatambua kwamba elimu ya Mwenyezi Mungu ipo katika vitabu na mafundisho ya Mitume na Manabii wake
Kwahiyo itoshe kujua kwamba mitume wake walitufahamisha kuwa Adam ndio kiumbe wa mwanzo,maana kinyume na hapo ina maana tutakuwa na mashaka na mafundisho ya manabii na mitume,na hapo tutakuwa tumekufuru
Yaan sawa sawa na leo hii muislamu asema swala tano zimeamrishwa katika qur'an lkn hatujaambiwa namna ya kuziswali,wakati Mtume rehema na amani zimuendee ameelekeza namna ya kuziswali
Narudia tena dini husomwa kama maarifa mengine pia,,kwahiyo acha kutafuta sababu
Waislamu wengi tunaijua biblia kiasi chake,kwahiyo acha porojo,we endelea na mistari yako pendwa tu,,Yesu ndio ndimi njia na uzima,hakuna aendaye kwa baba bila yeye,ishi nayo hiyo
Hatuna cha kujadiliana na wewe
Asante
Hebu msomeni Kuhani mose, hapo nilipo mnukuu kuna kitu kipya kakizungumzia.HAKUNA 'DINI' WALA UHITAJI WA 'DINI MPYA'....
Dini ni katalisti/Kichochezi/Kiuhuishisaji cha 'Mfumo/Mifumo'... Kwa mfano, ilikuwepo na 'fanusi jamii--functional society', ni lazima mazingira yawepo kwa ajili ya 'Kuijumuisha Jamii--integrative factor/basis'--mambo kama vile sheria, miongozo, maono n.k
Dini ni 'Shughuli' ya kuijumuisha Jamii ili 'ijiweze ama/na kujimudu' mapito ya matamanio yake ya Kiutu...
SASA, jamii inaweza kujumuishwa kwa 'ladha mbalimbali' za Utu na Kujichagulia--'sura' ama/na 'utukufu' mbalimbali; lakini 'Ukweli' wa 'Uzima/Sifa/Hali/Mwenendo' wa jamii huwa na 'Mbegu yake Mahsusi'--mbegu mahsusi ya 'Utabia wa Kishirika--organizational behaviour' wa wanajamii wowote.
Dini ni 'Shughuli' ya kuratibu 'Utabia wa Kishirika' wa 'Fanusi Jamii' yoyote; kuhakikishia wanajamii mazingira rafiki ya kukuwa na kustawi kiutamaduni kama jamii moja.
Ni kwa mintarafu ya haya, Dini, daima huwa ni 'Udhamirifu wa Kujumuisha na kutangamanisha' yote ya watu/wanajamii--mambo ya 'MRABA' wa 'Wakati-Jamii-Machaguo ya Kitaasisi-Matukio'.
Hili ndilo linaweza kushangaza humu kwa nini 'kinara' wa Uzi huu 'hana nongwa' kuhusishwa na 'Dini Yoyote'--iwe tuseme Uhindu, Uislam, Ukristo n.k.
Hivi ni kwa kuwa, Siri ya Dini ipo kwenye 'Ufahamu'--mambo ya maandiko na mapelekeo ya tafsiri; ndiyo 'tatizo la kiufundi' la wanadamu na vipawa vya akili/kiakili.
Sasa, siyo kila mtu mwenye 'daraja' ni bingwa ama fundi wa 'maneno'... Hili linaweza kuwashangaza wengi kusikia hivi... Kwa hivyo kudhani 'kinara' wa huu uzi 'atamudu' maswali na udadisi kwa 'maajabu' ni 'shauri mushkeli'....
'Tatizo la Kiufundi' la wanadamu na vipawa vya akili/kiakili linatatuliwa kwa udhamirifu wa 'Maarifa' na 'Maarifu' kupitiliza 'mashauri ya kawaida' ya 'habari na kuhabarika'...
Kwa hivyo, ukisikia mtu anazungumza kuhusu 'code' ama 'password', kiufundi huyu anakumbushia 'umma kujiongeza': 'kujua-maarifa-maarifu' huja kwa 'alama za kiutambuzi' na 'wepesi wa kuifungua milango ya fahamu'; si kumendea 'stori stori za mambo ya maajabu'...
Hichi ndicho hata humu, kwenye huu uzi, bado kidogo ni 'mtihani', ila In Shaa Allah, Elimu na Ilimu tayari imeshajengewa msingi kwa hili jukwaa. Siku za mbele kidogo, mwishoni mwa mwaka huu ama kufika mwakani, humu watakuwepo wadau wengi ambao si 'wanadamu wa Duniani' ila watashiriki 'maarifa na funguo za mafahamu'--wapo kwenye 'maandalizi ya kidiplomasia'; jambo linalotaka sana humu kusisitiza 'mkao sahihi' wa kunufaika na mambo/shughuli kama hizi za makutano ya 'viumbe-wanadamu na viumbe-watu wengine wenye nasibu ya mawanda yenye kutofautiana mapana ya fahamu/ufahamu'.
Jambo linaweza kujenga mnufaiko na mambo/shughuli kama hizi za makutano ya 'viumbe-wanadamu na viumbe-watu wengine wenye nasibu ya mawanda yenye kutofautiana mapana ya fahamu/ufahamu' ni UONO NA UFIKIRIFU MIFUMO...
SASA, asili ya 'code' ama 'password' ni mambo ambayo humu wengi hawajajiandaa kumaizi kwa kuwa hapa Duniani kuna matatizo ya 'Kielimu' yanayofanya watu wawe na tabia 'kudaka hili na kutupa lile' eti kwa kuwa habari zake si za eneo la utaalam/usomi wa mtu--hili jambo ni kasumba, na ubovu wa kimaarifa; tena linaathiri moja kwa moja mawezekano ya 'Mageuzi ya Kijamii' na Uwezo wake kukumbatia 'Nuru ya Ufahamu'--ilivyo ni njia ya Wongofu...
Kwa hivyo, jambo moja la muhimu na tena la msingi kuwakumbusha watu wote, wale wanaodhani wanayoyakunufaika na 'wageni' ama 'wenyeji' wenye mapana zaidi ya fahamu na ufahamu, ni kufuta na kuondoa kasumba juu ya visomo-maarifa-ujuaji walivyonavyo.
Haifadii mtu kusema yeye 'si msomi'--hajasoma shule; ama 'hana elimu ya kutosha'; basi huyu akiona mwanajamii mwenzake anadadavua jambo kwa fasaha na mapana yeye kujiambia 'Hii michosho/Kuchoshana/Ndefu--nitasoma baadaye'... Kwa kuwa inawezekana hayo yanawekwa hivyo ili iwepo 'Subira'--siku akiwa tayari kuijaribu 'Elimu' basi akitulia na kudhamiria atanufaika moja kwa moja...
Haifadii mtu kusema yeye 'ni msomi'--amesoma na madigrii kama yote katika sheria, sanaa ama/na uhandisi; basi huyu akiona mwanajamii mwenzake anadadavua jambo kwa fasaha na mapana nje ya ugani wake wa kitaaluma basi ajiambia: ah huyu anaandika 'mambo yake sana'; ama hata mimi nimesoma sana--najua mengi; tusichoshane! Kwa kuwa 'usomi' na 'kujisikia' vinaweza kuwa kiburi na ujivuni. Kwa hivyo si ajabu kuona watu wengi wakishakuwa na 'elimu za vyeti' akili zao zikalala na vyeti vyao masandukuni ama zimetundikwa ukutani na vyeti--hawana maajabu! Si kwa maneno ama busara ya mapana ya mambo...
Uono na Ufikirifu Mifumo ni Elimu 2.0; hii inahusika kwa wote wenye 'kudhamiria kujua ilivyobora' na basi inawezekana kwa 'Msomi' na hata vile vile mtu 'Asiye Msomi' kwa dhana ya 'Madarasa'... Elimu 2.0 ni mwanzo wa 'Hekima'; na Hekima ni Uhuru...
Mambo ya 'Code' na 'Password' ni mambo ya Elimu 2.0 kujinasibu na Elimu 3.0; Ambavyo Elimu 3.0 ni ILIMU--ILIMU ilivyo ni metafizikia ya Elimu. Basi yawa, NENO ILIMU limeshatohorewa rasmi kuwa msamiati wa lugha ya Kiswahili kumaanisha 'UGANI WA MAARIFA NA MAARIFU' ya 'MIFUMO'--Mifumo ya UTU-MAISHA-UISHO.
Kwenye maarifa ya Elimu ya Jamii, 'sosholojia' ELIMU 3.0 ndiyo mambo yanayohusiana na 'Ualama Oanifu' wa 'Kawaida za Jamii'. Kwa mintarafu ya hivi, mifumo yote huja kutokana na 'Mwangaza wa Jamii', 'Kujichagulia' na 'Matendo'--Mambo yanafanya kwa mfano Elimu, Siasa na Mipango kuwa pembetatu ya Utaifa/Jamii/Dola...
Kwa nchi ya Tanzania kwa mfano, 'Code' na 'Password' ya Elimu na 2.0 na Elimu 3.0 huja kwa 'Mazingatio ya Kikatiba': Udhamirifu wa Taifa la watu wenye kusudi la kuijenga na kuilinda nchi-dola kwa misingi ya UHURU-UDUGU-HAKI-AMANI. Ni adha ya jamii 'kujisahau' tu ama 'Kutojitambua' kusudi la utaifa na maisha yao... Haya manne ni 'Code' na 'Password' ya Nchi ya Watanzania...
Kwa hivyo kwa mtu wa Elimu 2.0 na Elimu 3.0 anaweza kuzibaini hizi 'codes' na 'Password' kirahisi kabisa; kwa mfano hivi vinne hukadirisha MRABA wa NISHANI ya UTU BORA. Kwenye Elimu na ILIMU ya mapokeo ya Ukristo UHURU-UDUGU-HAKI-AMANI ni kode za Uzabibu 13--Ufahamu Kristu. Kwenye Elimu na ILIMU ya mapokeo ya Uislam UHURU-UDUGU-HAKI-AMANI ni ufunguo wa Imani kwa 'Allah'--Katika majina 99 ya ALLAH, kuna haya ambayo huleta 'kumcha Mola' kwa baraka ya nusuru ya nchi-dola:, (1) AN NUR (Mwenyekuwa MWANGAZA), (2) AL JAAMI(Mwenye Kuwakusanya Waja Wema), (3) AL-'ADL (Mwenyekuwa na Uadilifu katika HAKI), na (4) AS SALAAM (Mwenyekuwa na Salama).
Sasa, ipo namna ya kutanuka haya yote kwa Elimu 2.0 na Elimu 3.0; In Shaa Allah, tuombe kheri haya tupate kuyafahamu kwa jicho jema na yatuingie moyoni na akilini...
Hmmm
Amani iwe juu yako Simba.Kuanzia Jumatatu nikumbushe.
Simba.
Ahsante.
Imebidi nifurahi tu. Ama hujuwi Qur'an au unapotosha kwa makusudi? Mbona umenukuu kipande tu Wapi katajwa Muhammad hapo?فَاصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ اللَّهِ حَقٌّ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَارِ
Hivi mtume Muhammadi alifanya dhambi gani hadi Mola wake alikuwa akimwamuru mara kwa mara kuwa atubu ?
Ziko Aya nyingi sana zinazo mhimiza Muhamadi atubu moja wapo ni hii hapa.
1. Hivi alifanya dhambi zipi ?
2. Hivi alitubu kweli ?
3. Hivi alisamehewa ?
4. Hivi kuna Aya inayo mwonyesha kuwa alitubu kama alivyo amriwa kwa Aya ?
5. Hivi ni kwanini hakutubu kama alivyo amriwa na mola wake ?
(GHAAFIR (AU AL MUUMIN) - 55)
Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli. Na omba msamaha kwa dhambi zako, na umtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi jioni na asubuhi.
Cc@Etugrul Bey,
Cc FaizaFoxy
Musa alimwua Mmisri akakimbia.Imebidi nifurahi tu. Ama hujuwi Qur'an au unapotosha kwa makusudi? Mbona umenukuu kipande tu Wapi katajwa Muhammad hapo?
Kwanini ume "quote out of context"?
Hapo Qur'an inatukumbusha, wewe na mimi, aliyoambiwa Musa. Hujui Musa alikosa nini tukupe darsa ?
Soma tafsiri kuanzia aya ya 53, hii hapa:
40:53. Na kwa hakika tulimpa Musa uwongofu, na tukawarithisha Wana wa Israili Kitabu, 53
54. Ambacho ni Uwongofu na Ukumbusho kwa wenye akili. 54
55. Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli. Na omba msamaha kwa dhambi zako, na umtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi jioni na asubuhi. 55
Kijana, unalijua kosa la Musa? Au niendeleze darsa?
Sasa umeelewa anaambiwa nani hapo eeh. Na jina lake lipo kwenye hizo ayat.Musa alimwua Mmisri akakimbia.
Na hii hapa anaambiwa Musa ?Sasa umeelewa anaambiwa nani hapo eeh. Na jina lake lipo kwenye hizo ayat.
Qur'an haifanyiwi utani kijana.