Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Nashukuru kwa Faraja hii kwamba tiba ipo. Sasa Arsis naomba umshawishi Simba ajitowe tu anisaidie kwa hili Kaka yangu apone, nahitaji sana msaada wake hapa. Maana hili jambo linaninyima Amani na Furaha muda wote.
In shaa Allah wasiliana nae hapa hapa Jumatatu, tutamshauri afanye nini ujitibu mwenyewe.
 
Hivi wewe umewahi zungumza na malaika au kuonana nao?
Toka nimezaliwa sijawahi sikia mtu katokewa na malaika.... Ila kwenye vitabu zamani ilikuwa kawaida waja wema kutokewa na malaika🤔🤔

Ila kesi za majini ni nyingi sana... Kwanini watu wa zamani (hasa bani israil) walikuwa na visa vya malaika ila sikuiz hakuna kabisa🤔🤔

Au ni sababu ya maaswi??
 
Hapana, sijawahi kusikia jini akiitwa Wolfgang au John, ni Kina Maiumuna, Zuchu, Muddy, Jafari na wengine wengi wenye asili ya Kiarab. Sasa naelewa kwanini Waarab si watu wa maana.
Chief wapo tena sana,kuna ndugu yangu mmoja yeye ni mkristo,aliwahi pandisha ,kuna mwamba mmoja toka Marekani anaongea slang ile yenyewe,hapo ndo niliamini kweli majini wapo,kwasababu huyo ndugu yangu hajui kiingereza kabisa

Sema hao wengine labda maarufu,hivi unajua mpaka kuna majini ya kimasai,je wamasai ni waarabu?

Tujifunze mambo jaman ,tuache kusema mambo bila elimu
 
Toka nimezaliwa sijawahi sikia mtu katokewa na malaika.... Ila kwenye vitabu zamani ilikuwa kawaida waja wema kutokewa na malaika🤔🤔

Ila kesi za majini ni nyingi sana... Kwanini watu wa zamani (hasa bani israil) walikuwa na visa vya malaika ila sikuiz hakuna kabisa🤔🤔

Au ni sababu ya maaswi??
Malaika hawana sababu ya kujijulisha kwako mpaka waamrishwe hivyo, hawana uamuzi huo, Hata akija huwezi kujua au kumjua. Lakini siku na wakati wa kuingia kwenye umauti utamuona.
 
Mimi Simba jamani, rsis ameaga, anawatakia heri nyote, anasema mwenye swali au elimu asisite kuuliza na kufundisha. Chovhte kile.

Mimi nitarudia posts na ninaloweza kujibu nitalijibu kivyangu na nisiloweza kujibu nitamuuliza Arsis.
 
Kuna sehemu huko nyuma umegusa kidogo kuhusu aina za elim...... Kuna elim ya kinaadam, kijinn na elim ya Allah 🤝

Hii elim ya Allah ndo ipi?
Au ndo hii tunasoma madrasa
Elimu ya/za Allah zipo nyingi Allah ndie mwenye kujua zaidi.

Moja ni ile anayotupa bila kufundishwa na mtu tuliozaliwa nayo. Nyingine ni ile aliowapa Mitume wake kutufundisha. Ya mwisho ni ile tunayojifunza sisi wenyewe kwa kufanya tafiti tofauti na kutujia ideas ambazo hatukuwa nazo wala kufundishwa kabla.

Simba.
 
Elimu ya Allah zipo nyingi Allah ndie mwenye kujua zaidi.

Moja ni ile anayotupa bila kufundishwa na mtu tuliozaliwa nayo. Nyingine ni ile aliowapa Mitume wake kutufundisha. Ya mwisho ni ile tunayojifunza sisi wenyewe kwa kufanya tafiti tofauti na kutujia ideas ambazo hatukuwa nazo wala kufundishwa kabla.

Simba.
 

Attachments

  • Screenshot_20240825-003727.png
    Screenshot_20240825-003727.png
    178.2 KB · Views: 51
We Simba kwasababu gani unayakwepa majukum yako.... Humu Sasa hivi kila mtu anakutizama kwa jicho la mkombozi kwenye matatizo yake...... Lakini Arsis anasema wewe uko busy na kutengeneza magari😴😴

Arsis kasema unaweza kuwasaidia watu humu ukiamua wewe na jinn bakora
Watu hawana nguv za kiume, watu wanasaratani, watu wanamashetwan, watu washajikatia tamaa ya maisha😭😭

Watizame kwa jicho la huruma... Ni kweli most of them hawana tena sehemu ya kupata msaada
 
Basi nilivyoendelea kusoma vitabu vya Wakristo na Waislamu, nilikuja kugundua kuwa.
Waislamu wana ukaribu sana na Majini.
Hadi kufikia kulindwa na Majini na wakapewa Sura nzima ya Majini kwenye kitabu chao cha Qurani.
Wakafikia Hadi kuitana ndugu.

Nikagundua kuwa Wakristo wanaukaribu sana na Malaika, na kufikia kulindwa na Malaika.
Wakristo:
Zaburi (Psa) 91:11
Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.

Waislamu:
Mas'ud reported God’s messenger as saying, “Do not cleanse yourselves with excrement or bones, for that is the provision of your brethren among the jinn.”

Nikatafakari na kuona Wakristo wako karibu na Mwenyezi Mungu na Malaika zake.

Waislamu na Majini wako mbali na Mwenyezi Mungu.

Katika Uislamu kumejaa sana habari za Majini, Majini Majini. yaani hao akina Arsis, na wengine.
Ni nadra sana na ni kama hakuna kabisa habari za uhusiano wa Malaika na Waislamu katika mafundisho ya Waislamu.

Basi nikaona ni Bora niwe Mkristo, kama kuna habari ngeni niwaulize Malaika tofauti na Waislamu wanao wauliza Majini ambao walisha fukuzwa Mbinguni kwa kumwasi Mwenyezi Mungu.
...........
وَأَنَّا لَمَسْنَا السَّمَاءَ فَوَجَدْنَاهَا مُلِئَتْ حَرَسًا شَدِيدًا وَشُهُبًا
(AL - JINN - 8)
Nasi tulizigusa mbingu, na tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu na vimondo.
وَأَنَّا كُنَّا نَقْعُدُ مِنْهَا مَقَاعِدَ لِلسَّمْعِ ۖ فَمَن يَسْتَمِعِ الْآنَ يَجِدْ لَهُ شِهَابًا رَّصَدًا
(AL - JINN - 9)
Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini sasa anaye taka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia!
وَأَنَّا ظَنَنَّا أَن لَّن نُّعْجِزَ اللَّهَ فِي الْأَرْضِ وَلَن نُّعْجِزَهُ هَرَبًا
(AL - JINN - 12)
Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani, wala hatuwezi kumponyoka kwa kukimbia.
.............
Hizo Aya zinathibitisha kuwa Majini waliwahi kuishi Mbinguni na yakafukuzwa kwa uasi wao na yakitaka kuchungulia Mbinguni yanapigwa na walinzi wa huko(Malaika) kwa nguvu ya vimondo.

Mtoa mada:
Mwulize Arsis, mosi,ni kwa nini alifungwa miaka zaidi ya 900 na bila kulindwa na Mungu wake.

Pili, ni kwanini hana uwezo tena wa kwenda mbinguni aliko kuwa anaishi hapo awali.

Tatu, ni kwanini alifukuzwa Mbinguni hadi akaishi katika Dunia aliyoishia kufungwa kwenye chupa.
Cc FaizaFoxy,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom