Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Arsis

JF-Expert Member
Jan 25, 2024
1,626
5,776
Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 1

Ilikuwa ni siku chache kabla sijatimiza miaka 18. Nilipelekwa Tanga, kijiji kimoja kipo karibu sana na mpaka wa kwenda Kenya. Kabla ya kuingia huko kijijini ndani kuna ki mji kinaitwa Duga. Ilikua sio mara yangu ya kwanza kupelekwa huko kwa mambo ya kimila na jadi.

Lakini hii ya safari hii ilikua kidogo yakutisha. Kijiji chenyewe kipo ufukweni kabisa na kina mito miwili inapita, mmoja Kaskazini mashariki ya kijiji, huu mkubwa kiasi na mmoja mdogo unapita kusinii ya kijiji. Kwa hio kijiji ni kama kimezungukwa na maji, maana mashariki yake ni bahari ya hindi, Kaskazini mto na kusini mto. Magharibi tu ndio kuna njia ya kwenda mpaka barabara kubwa ya lami, ambayo ipo kama kilomita 3 au 4 kutokea hapo kijijini.

Safari hii ilikua ni nzito kidogo kwa sababu niliambiwa unaweza kukaa kijijini huko wiki moja au mbili, itategemea na "babu" huko ataamua kama mambo yako tayari au bado.

Nilifatana na Baba na Mama yangu kwenye gari la nyumbani mpaka hapo barabara kuu kutokea Tanga, hapo nikakuta vijana wawili wakubwa kwangu, wananingoja na baiskeli mbili, moja ya kunipakia mimi na moja ya kupakia mizigo yangu.

Mizigo yangu kweli ilikua mingi, yangu binafsi lilikua ni begi kubwa na racksack ya mgongoni, lakini kuna maboksi kama matatu makubwa yalikua ya mama akanambia haya yote mkabidhi babu yako mkifika.

Basi tukaagana pale, wao wakanambia ukimaliza kazi yako watakuleta hapa barabarani utapanda gari za kuja Tanga, sisi utatukuta Tanga, tutakuja baada ya wiki mbili, kama utakua umemaliza kabla ya wiki mbili ukifika Tanga tusubiri. Wakaondoka zao, na mimi nikapakiwa kwenye baiskeli kama abiria, na nyingine ikafungashwa ile mizigo yetu yote, ikatangulia.

Hatukuchukua muda sana, tukafika kijijini, moja kwa moja mpaka kwa babu yangu. Babu yangu tunajuana sana, na alikua ni sahiba yangu sana, ni mtu ma story ya kizamani na mimi nilikua mdadisi sana. uzuri wa babu alikua hakwepi swali lolote utalomuuliza na alikua hamumunyi maneno, anakujibu mpaka likuingie. Nilikua namshangaa sana, kwani hakuna swali lilililokua gumu kwake.

Hata niwe na swali, mwenyewe naliona gumu kweli, nikimuuliza babu ananijibu huku ananisifia "swali zuri sana hilo", ananijibu kiurahisi kabisa, mengine huwa anachukua muda kuyajibu, mtindo wake wa kuibu ulikua kama anakusimulia hadithi, anaweza akatoka kabisa nje ya swali ulilomuuliza lakini atakuhadithia mpaka utalipata jibu. Mara nyingi akikujibu basi lazima utakua na maswali mengine mawili matatu ya kuuliza. Kwa ufupi alikua anaelewa kufungua "kichwa" kwa mujibu baba yangu.

Links za muendelezo zipo chini hapo (bofya maandishi ya buluu).

Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 2
Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 3
Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 4
Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 5
Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 6
Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 7
Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 8
Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 9
Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 10
Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 11
Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 12
Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 13
Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 14
Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 15
Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 16
Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 17

Episode 2 Nilioyaona Dar.

Nilioyaona nilipoingia Dar. 1
Nilioyaona nilipoingia Dar. 2
Nilioyaona nilipoingia Dar. 3
Nilioyaona nilipoingia Dar. 4
Nilioyaona nilipoingia Dar. 5

Episode 3 Safari ya Shinyanga.

Safari yangu ya Shinyanga. 1
Safari yangu ya Shinyanga. 2
Safari yangu ya Shinyanga. 3
Safari yangu ya Shinyanga. 4
Safari yangu ya Shinyanga. 5
Safari yangu ya Shinyanga. 6
Safari yangu ya Shinyanga. 7.

Kisa Cha Adam.

Kisa cha Adam. Utangulizi 1
Kisa cha Adam. Utangulizi 2
Kisa cha Adam. Utangulizi 3

Rejea ya baadhi ya istilahi (terminologies) 1
Kisa cha Adam 1
Kisa cha Adam 2
Kisa cha Adam 2.1
Kisa cha Adam 2.2
Kisa cha Adam 2.3
Kisa cha Adam 2.4
Kisa cha Adam 2.5
Kisa cha Adam 2.6
 
Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 1

Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 2

Babu akatupokea pale, tukakumbatiana kwa furaha, mara na bibi nae akaja aliposikia nimefika, akanambia "aah, sasa mume wangu ndio kaingia, sio hiki kizee, sina habari nacho tena". na yeye bibi akanikumbatia akanipiga mabusu ya nguvu shavuni, akanambia twende ndani mume wangu, nimekutayarishia chumba chako.

Nyumba ya babu yangu ilikua ni kubwa sana kwa maisha ya kijijini, ina vyumba self-contain vitatu, umeme utafikiri upo mjini. maana umeme umepita hapo hapo kijijini kwao, wenyewe wanasema huu unakwenda Kenya, unatokea Hale. Kwa ufupi hauhisi kabisa kama upo kijijini mpaka utoke nje ya boma lake. babu alikua na nyumba hiyo yake kubwa na nyingine ndogo ndogo za vyumba viwili au kimoja zimetapakaa pote kumzunguka. Nyingi zilikua za kufikia wageni wanaokuja kwa matatizo yao kwa babu yangu, babu alikua mganga wa jadi, tena anaesifika kweli. Kwake hapakosi wageni, mpaka mawaziri utawakuta huko. Kila mmoja na shida yake.

Babu toka nimefika alikua haniwachi peke yangu, ana nyumba moja ipo karibu na kwake hiyo mwenyewe ndio ofisi yake, ina chumba kizuri tu, cha kufanyia shughuli zake na wageni wake, na kama ina baraza kubwa ndipo wanaposubiri wageni wanaokuja kumuona, ina vumba viwili vidogo ndani, mwenyewe anaviita "operation rooms". Babu alikua anaongea na kuandika Kiarabu, Kingereza na Kijerumani kwa ufasaha kabisa. Kabla ya kuamua kurudi kuishi kijijini, mwenyewe anapaita shamba, hapaiti kijijini hata siku moja. Alikua ni fundi mekanika, tena foreman, wa idara ya vifaa na magari ya serikali hapo Tanga. Mwenyewe anakwambia mimi foreman tokea ukoloni, Uhuru haukunipa u foreman.

Alikua ni mtu anaejulikana sana Tanga na anaheshimika sana. Ni mcheshi sana, kutwa anatabasamu, akikasirika humjui kabisa, wewe kutwa kucha unamuona ni mtu wa furaha tu.

Inaendelea post #7.
 
Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 2

Nilioyashuhudia nilipofunguliwa macho 3.

Siku ya kwanza ilikua haina pirika yoyote zaidi ya kusalimiana na ndugu jamaa na marafiki, walikua wengi wengi tu. Babu alikua bize (busy) sana na wageni wake, kwa hiyo nilipata muda mrefu wa kuongea na bibi. Bibi akanambia, umekuja msimu wa kamba, kesho kutwa tutaanza kuvuna kamba, mito yote safari hii imeshona kamba, hivi wengine wameshaanza kuvuna huko. Sifahamu kwanini bibi alikua anasena "kuvuna" kamba wakati wapo kwenye maji, mimi najua kuvua.

Siku ya pili alfajiri babu akanigongea chumbani kwangu, nikajua kama kawaida yake, lazima uamke alfajiri muende mkasali msikitini. Kuna msikiti hapo hapo kwenye boma lake na ndio nyumba ya kwanza kabisa kabla hujafika kwake kama unatokea barabara ya kuja kwake, ni msikiti, mzuri tu wa kisasa. Basi nikatoka na babu tukaelekea msikitini, tukasali, tulipomaliza akanambia sasa "bwana mkubwa" hakuna kurudi kulala nyumbani, tunaianza kazi yako wakati jua linachomoza, linapanda juu, tunaenda kwenye yale mapango upande wa pili.

Nilikua nayajua hayo mapango, yapo upande wa pili wa mto ule wa Kaskazini, na kuyafikia msimu wa maji, lazima upite baharini uuzunguke mto kwa baharini ndio ufike kiurahisi, la sivyo uukatize mto. Babu alikua hapendi hili, anasema maji ya chumvi dawa, kama huyaogi japo yakanyage.

Tukaenda na babu, na kijana mmoja katika wale waliokuja kunifata na baiskeli. Huyo mwenyewe anasema ni "mwanafunzi" wa babu. Tulipoingia baharini akanambia tqwende maji ya kifuani, zama mwili wote, piga mbizi maji ya chumvi yakupate mwili mzima, kila sehemu. Na mimi ninavyopenda kuogelea, ikawa ndio kanifikisha. Babu alikua anacheka tu. Mpaka akanambia, inatosha Simba, umegeuka samaki unataka kukaa baharini tu?

Kutoka hapo tukavuka tukatokea upande wa pili wa mto, kabla ya kuingia mapangoni akanambia, sasa kakoge mtoni, nikaenda, nilikua mwenyeji wa ule mto. Nikaingia nikakoga, maji yalikua sio mengi sana, mto wenyewe unatokea mapangoni tena wakati wa mzimu ndio unaonekana, maji ya kufika vifundo vya mguu, kawaida huo ni kama kimchirizi kinapita , kutokea vichakani huko, babu anasema hautoki mbali huu unatoka chemchem za mapangoni, zimetobia njia. Mwenyewe alikua anasema, maji yake dawa, ukiona maji mpaka yametoboa sehemu yenyewe elewa kua hayo ni maji yenye faida kubwa sana, kama hayanweki basi japo yakoge. babu tangu wadogo alikua anatukataza kuufata kuona unapotokea, anasema huko wadudu na wanayama wengi, msende, wadiudu na wanayama na wao wanafta maji, tena wao wanayasikia harufu kutoka mbali sana.

Nilipokua mtoni, ikaona kweli msimu huu kamba wengi kupita kawaida, maana pale nilipoingia ni kama bwawa kubwa, mto umechanua. Sio kwenye mkondo wa mto, walikua kamba wamejaa. Nilipotoka kwenda pangoni, babu akanambia umeona neema ya kamba mwaka huu? Nikamwambia nimeona babu, ni wengi sana. Akanambia imekua vizuri utapata zawadi ya kuwapelekea mjini.

Basi tukaingia pangoni, babu akaanza kunipa dawa akanambia hii jipake mwili mzima, kama mafuta ya nazi hivi yamechanganywa na majani majani ya kupondwa kupondwa, akanambia usiache sehemu. Nikafanya kama alivyoniagiza. Akanambia sasa hiyo dawa haitakiwi ukoge mpaka kesho, sana sana unachukua udhu. Fanya hima usitengue udhu. Nikamuelewa.

Akaniachia dawa za kula, akanambia babu, hapa usitoke kuja nyumbani leo, leo utalala hapahapa, mimi nitakuja baadae, wacha nikashughulikie wageni. Wewe na mwenzako huyo leo zungukeni upande huu huu. Mtaletewa chai na chakula hukuhuku. Msiende mbali na mapango wala msiende kuogelea. leo mpo kwenye himaya ya viumbe ambavyo hamvioni. Nikaguna kimoyomoyo.

Inaendelea post #43.
 
Inatokea post namba 4.

Siku ya kwanzq ilikua haina pirika yoyote zaidi ya kusalimiana na ndugu jamaa na marafiki, walikua wengi wengi tu. Babu alikua bize sana na wageni wake, kwa hiyo nilipata muda mrefu wa kuongea na bibi. Bibi akanambia umekuja msimu wa kamba, keshi kutwa tutaanza kuvuna kamba, mti yote safari hii imeshona kamba, hivi wengine wameshaanza kuvuna huko. Sifahamu kwanini bibi alikua anasena "kuvuna" kamaba wakati wapo kwenye maji, mimi najua kuvua.

Siku ya pili alfajiri babu akanigongea chumbani kwangu, nikajua kama kawaida yake, lazima uamke alfajiri muende mkasali msikitini, kuna msikiti hapo kwenye boima lake la ndio nyumba ya kwanaza kabisa kabla hujafika kwake ni msikiti, mzuri tu wa kisasa. Basi nikatoka na babu tukaelekea msikitini, tukasali,tulipomaliza akanambia sasa "bwana mkubwa" hakuna kurudi kulala, tunaianza kazi yako wakati jua linapanda juu, tunaenda kwenye yale mapango upande wa poili. Nilikua nayajua hayo mapango, yapo upoande wa pili wa mto ule wa Kaskazini, na kuyafikia lazima upite baharini uuzunguke mto ndio ufike.

Tukaenda na babu, na kija mmoja katika wale waliokuja kunifata na baiskeli. Huyo mwenyewe anasema ni "mwanafunzi" wa babu. Tulipoingia baharini akanambia zama mwili wote, piga mbizi maaji ya chumvi yakupate kila sehemu. Na mimi ninavyopenda kuogelea, ikawa ndio kanifikisha. Babu alikua anacheka tu.

Kutoka hapo tukavuka tukatokea upoande wa poili wa mto kabal ya kuingia mapangoni akanambia, sasa kakoge mtoni, nikaenda, nilikua mwenyeji wa ule mto. Nikaingia nikakoga, nikaona kweli msimu huu kamba wengi mtoni, maana pale nilipoingia ni kama bwawa kubwa, mtoi umechanua. Sio kwenye mkondo wa mto, walikua kamba wamejaa. Nilipotoka kwenda angoni, babu akanambia umeona neema ya kamba mwaka huu? Nikamwambia nimeona babu, ni wengi sana. Akanambia imekua vizuri utapata zawadi ya kuwapelekea mjini.

Basi tukaingia pangoni, babu akaanza kunipa dawa akanambia hii jipake mwili mzima, kama mafuta ya nazi hivi yamechanganywa na majani majani ya kupondwa kupondwa, akanambia usiache sehemu. Nikafanya kama alivyoniagiza. Akanambia sasa hiyo dawa haitakiwi ukoge mpaka kesho, sana sana unachukua udhu. Fanya hima usitengue udhu. Nikamuelewa.

Akaniwachia dawa za kula, akanambia babu hapa usitoke kuja nyumbani leo, leo utalala hapaahapa, mimi ntakuja baadae, wacha nikashughulikie wageni. Wrewre na mwenzako huyo leo zungukeni upande huu huu. Mtaketewa chai na chakula hukuhuku. Msiende mbali na mapngi wala msiende kuogelea. leo mpo kwenye himayta ya viumbe ambayo hamvioni.

Itaendelea.
Kwa nini usiandike story yako yote ndio upost?
 
Nasubiria
 
Twasubiri
 
Back
Top Bottom