Mongella amewataka wananchi wa tarafa ya Loliondo Wilayani Ngorongoro kuwa watulivu kutokana na uchonganishi wa watu wasiokuwa na nia njema na nchi yetu

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Me.John Mongella,
amesema hayo leo June 11 2022 katika tarafa va loliondo wilaya ya Ngorongoro alipokuwa anaongea na vyombo vya habari kuhusiana na zoezi linaloendea la uwekaji mipaka katika wilaya hivo, Amewambia waandishi wa habari kuwa kuna baadhi ya watu na
mitaandao va kijamii kupotosha kuhusiana na kinachoendelea katika zoezi la uwekaji mipaka katika wilaya ya Ngorongoro.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella amewataka wananchi Wa Tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro Kuwa watulivu na kusikiliza maelekezo ya serikali katika zoezi la uwekaji mipaka.
Aidha amesema kuwa katika siku ya jana kulitokea kundi la watu wenye silaha ambapo askari wetu alijeruhiwa na kukimbizwa hosptal lakini alifariki dunia wakati anapatiwa matibabu.
 

Attachments

  • VID-20220611-WA0050.mp4
    19.9 MB
IGP afanye maamuzi magumu vikosi viende Ngorongoro walio husika na mauaji ya askari wakamatwe na kufikishwa mahakamani sababu kama wamedhibiti magaidi wa mtwari sembuse hao wamasai.
 
Si Waziri Mkuu alisema hakuna makabiliano ya askari na wananchi? Na ile video ya Wamasai ikaitwa ni fake?

Sawa kuawa polisi, je ni wananchi wangapi wameuawa ? Maana hamuwezi kudanganya ni polisi wameuawa tu..
... na Spika akaelekeza aliyeiandaa na kuipost kwenye mitandao ashughulikiwe! Na Bunge likazizima kwa nderemo na vifijo!
 
Askari Polisi mmoja ameuawa kwa kupigwa mshale wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati wa zoezi la uwekaji mpaka katika eneo la pori tengefu kwenye Tarafa ya Loliondo.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella akisema kwamba kifo hicho kilitokea Juni 10 alasiri, na kusisitiza kwamba kama serikali wanatambua uzalendo wa askari huyo.

Ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa Tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro kuwa watulivu na kusikiliza maelekezo ya serikali katika zoezi la uwekaji mipaka.

Wananchi wanatakiwa na Serikali kuhama katika eneo la Ngorongoro na kwenda kuishi Handeni, Tanga ambapo Serikali itawasaidia katika kuhama. Nia ikiwa ni kuhakikisha uhifadhi endelevu katika Hifadhi ya Ngorongoro.

Baadhi ya Wananchi wa Ngorongoro hawataki kuhama katika ardhi yao ya asili kwani Wanaishi hapo kisheria na Wanatambulika.
View attachment 2257198
Ninachojiuliza mbona ili swala limekuja ghafa sana katika kuwaondoa,ila wanasiasa sio watu wa kuwaamini hata kidogo
 
Tutajuaje kama sio made up story ili kuhalalisha wanachotaka kukifanya?

What I see ni kwamba wanataka kuhalalisha matumizi ya nguvu kwenye kuwatoa hao watanzania huko ngorongoro, kupinga hilo basi uthibitisho upatikane juu ya kifo cha huyo askari.
 
Back
Top Bottom