Serikali ituonee huruma wananchi mkoa wa Arusha katika masuala ya uhifadhi

Midimay

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
2,908
4,771
Habari za Alfajiri Watanzania wenzangu.

Bila shaka kila mmoja wetu ni shahidi kwamba Mkoa wa Arusha umekuwa ni HOST wa uhifadhi hapa nchini hasa unaohusisha Wanyama Pori.

Na hili sio automatic. Sababu kubwa ni nature ya watu wa asili wa mkoa wa Arusha kutokuwa adui kwa Wanyama Pori kwa maana ya kutoawaua kinyama au hata kwa ajili ya chakula.

Wamaasai ni marafiki wa Wanyama Pori ndio maana tunaona Mbuga nyingi za Wanyama wengi zipo katika ukanda wanaoishi Wamaasai.

Mtu mzima mmaasai kwenda kuwinda huchukuliwa kama aliyepotea, aliyepatwa na laana, anayejitafutia mikosi na umaskini wa kizazi chake.

Hali hii ndio iliyowavutia wakoloni kuanzisha Mbuga za Wanyama kuzunguka jamii ya kimaasai pande zote.

Lakini sasa uhifadhi huo unarudi kuziwinda(coming back to hunt) jamii zinazoishi karibu na hifadhi hizo na kufanya mkoa mzima wa Arusha(isipokuwa pale mjini/jijini) kuwa mkoa usio support maisha ya watu wake.

Kwanini?
Wizara ya Mali Asili na Utalii kupitia Mamlaka ya Wanyama Pori(TAWA) wanajenga hoja kwamba mkoa mzima wa Arusha ilikuwa ni mapori tengefu. Hoja hii wanaijenga kwa kutumika sheria ya kikoloni(Fauna Conservative Ordinance ya 1951).

Kwa sheria hiyo inaonyesha kabisa kwamba asilimia 99 ya mkoa wa Arusha ni mapori tengefu.

Wakati mkoloni anatunga hiyo Sheria, tayari kulikuwa na watu katika maeneo hayo wakiendelea na shughuli zao za ufugaji na kilimo.

Katika andiko lao lilionekana mtandaoni, lililokusudiwa kwenda kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, TAWA wanadai kwamba asilimia 92 ya Wilaya ya Longido ni mapori tengefu

Ni asilimi 8 tu ndio imeachwa kwa wananchi na kwa Wilaya zingine hasa Monduli na Ngorongoro pia inakaribia au zaidi ya asilimia hizo.

Mkoa wa Arusha tayari ni mwenyeji wa maeneo yaliyohifadhiwa kwa kiwango kikubwa katika Taifa hili kama ifuatavyo:

1. Eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika Wilaya ya Ngorongoro.
2. Lake Manyara National Park katika Wilaya za Monduli na Karatu.
3. Pori la Akiba Loliondo katika Wilaya ya Ngorongoro.
4. Arusha National Park katika Wilaya ya Arumeru.
5. Sehemu ya Tarangire National Park katika Wilaya ya Monduli.
6. Hifadhi ya misitu Esimingor.
7. Hifadhi ya misitu katika milima Monduli, Longido, Ketumbeine, Lolkisale na Meru.
8. Pori la JWTZ kubwa kuliko mapori yote Tanzania linapatikana katika mkoa wa Arusha, Wilaya ya Monduli.
9. Eneo la JKT Makuyuni
10. Eneo la JKT Mto wa Mbu.
11. Sehemu ya Serengeti National Park ipo katika Wilaya ya Ngorongoro.
Na maeneo yote hayo ni makubwa sana.

Sasa kama TAWA wakiruhusiwa kuchukua maeneo mengine, kisa uwindaji, huu mkoa utaendelea Ku support maisha ya watu wake kwa namna gani?

Na sio kwamba TAWA hawana corridor za uwindaji karibu na Mbuga za Wanyama, wanazo.
Na kama wakihitaji basi wamegewe kutoka kwenye Mbuga za Wanyama na sio kutaka tena kuchukua ardhi inayotumiwa na wananchi katika maisha yao ya kila siku.
Naomba serikali ituonee wananchi huruma.

Uhifadhi usioangalia maisha ya watu katika nchi, hauna maana. Maendeleo yoyote ni kwa ajili ya mwanadamu na mazingira.
TAWA wasiruhusiwe kufanya wanachotaka kufanya.

Imagine kihifadhi 92% ya wilaya. Kuweni wazalendo. Dolar za Marekani zisituchanganye, tukawasahau wananchi. Sheria ya kikoloni isitumike kuwaumiza wananchi ambao ndugu zao tayari wameumizwa katika mapori ya Loliondo na Eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Hata kisiasa na kimahusiano ya kijamii, hii proposal ya TAWA haijakaa sawa. Hoja zao nyingi no dhaifu na za uongo. Na Lengo lao kuu wala sio uhifadhi au kulinda korido za Wanyama.

Msiwafanye wananchi wakamuona Rais wa JMT, mama Samia anawachukia, hawajali au anawatenga.

Hili swala linahitaji kutafakari mara nyingi nyingi kabla ya kutekeleza. Ikiwezeka hali ya uhifadhi katika Mkoa wa Arusha ibaki kama ilivyo sasa. Kite do chochote cha kuongeza ni kusababisha insustainability na migogoro isiyoisha.

Uhifadhi katika mkoa wa Arusha umefika its maximum.
Naomba tuonewe huruma. Bad Enough, hili swala lilifika katika Bunge la Jamhuri ya Kuungana wa Tanzania wakati wa bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo pia lilipingwa vikali na wabunge wanaotokea maeneo yatakayoaathirika, mfano. Christopher Ole Sendeka wa jimbo la Simanjiro.

Na katika kuhitimisha, siku ya kuahirisha Bunge, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, katika hotuba yake alielekeza kusitishwa kwanza kwa mchakato huo.

Mnaweza mkajisomea wenyewe taarifa hii ya TAWA.
 

Attachments

  • PRESENATION MAPORI TENGEFU YANAYOTAKIWA KUPANDISHWA HADHI (1).pdf
    12.6 MB · Views: 6
Mkuu nashukuru kwakuleta mada hi hapa. Ndugu yangu elewa maeneo mengi ya mkoa wa Arusha na Manyara yalikuwa hifadhi kwa mda mwingi.

Mwanzoni mwa miaka 90 ongezeko la watu kwa mikoa hyo yalifanya watu kuvamia mapori nakufanya shughuli za kibinadamu kitu ambacho ni kinyume na sheria.

FIKIRI MAENEO KAMA LOLIONDO ENDULEN TARANGIRE BUGER WASO yamegeuzwa kuwa mashamba na vijiji ya ujamaa. SIASA imeingia kwenye maeneo nyeti kama hayo TULIORISISHWA JE NA SISI TUTARISISHA NINI KWA WATOTO WETU NA WAJUKUU?

TUACHE UBINAFSI SHERIA IHESHIMIWE NA WATU WOTE.TUACHE SIASA KWENYE VITU NYETI KAMA HII.
 
Mkuu nashukuru kwakuleta mada hi hapa. Ndugu yangu elewa maeneo mengi ya mkoa wa Arusha na Manyara yalikuwa hifadhi kwa mda mwingi.

Mwanzoni mwa miaka 90 ongezeko la watu kwa mikoa hyo yalifanya watu kuvamia mapori nakufanya shughuli za kibinadamu kitu ambacho ni kinyume na sheria.

FIKIRI MAENEO KAMA LOLIONDO ENDULEN TARANGIRE BUGER WASO yamegeuzwa kuwa mashamba na vijiji ya ujamaa. SIASA imeingia kwenye maeneo nyeti kama hayo TULIORISISHWA JE NA SISI TUTARISISHA NINI KWA WATOTO WETU NA WAJUKUU?

TUACHE UBINAFSI SHERIA IHESHIMIWE NA WATU WOTE.TUACHE SIASA KWENYE VITU NYETI KAMA HII.
Vijiji vingi katika maeneo hayo vilianzishwa na kusajiliwa 1968,1969,1970 baada ya azimio la Arusha. Isitoshe ni serikali ya JMT ndio iliwahimiza kwenda kuzaliana na kuongezeka huko. Lakini pia 1951 wakati mkoloni anaanzisha mapori tengefu, watu walikuwepo katika maeneo hayo.
 
Tanzania yetu mkuu tuna matatizo makubwa ya kujitakia,ongezeko la watu president Nyerere aliambiwa pamoja na side effects zake (Tanzania kipindi hicho ilikua na watu under 15M na tulikua tunaongezeka kwa kasi sana,more than 2.5%),president Nyerere kwa kuwaogopa RC akafagia onyo hili under zuria, but it's not all lost, wataalamu wa mali asili pale Arusha, watembelee Botswana na kujifunza wenzetu wametumia njia gani kwa binadamu na mifugo yao wanaishi pamoja na wild animals, Kasane mjini ni kitu cha kawaida kuona tembo ILA wana corridors zao
 
Tanzania yetu mkuu tuna matatizo makubwa ya kujitakia,ongezeko la watu president Nyerere aliambiwa pamoja na side effects zake (Tanzania kipindi hicho ilikua na watu under 15M na tulikua tunaongezeka kwa kasi sana,more than 2.5%),president Nyerere kwa kuwaogopa RC akafagia onyo hili under zuria, but it's not all lost, wataalamu wa mali asili pale Arusha, watembelee Botswana na kujifunza wenzetu wametumia njia gani kwa binadamu na mifugo yao wanaishi pamoja na wild animals, Kasane mjini ni kitu cha kawaida kuona tembo ILA wana corridors zao
Sisi hatujapungukiwa na maeneo. Mbuga zetu za wanyama ni kubwa sana. Kwa kuwa Lengo(Ultimate Goal) la TAWA ni kupata maeneo ya kugawa vitalu vya uwindaji, basi wapewe corridors hizo kwa kumega national parks na siyo vijiji. Wananchi wanahitaji ardhi kwa ajili ya uzalishaji. Utalii hauwezi kutupatia kipato Watanzania wote. Ni wachache tu watafaidika na utalii na hivyo vitalu.
 
Back
Top Bottom