Simiyu: Askari Polisi Bariadi watuhumiwa kumpiga mtuhumiwa na kusababisha kifo chake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Kwa mara nyingine tena, Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu linatuhumiwa kuhusika katika kifo cha Mwananchi aliyekamatwa na Askari Polisi kisha kudaiwa kumpiga na kumsababishia maumivu makali na hatumaye kusababisha kifo chake.

Matukio ya Jeshi la Polisi kupiga au kujeruhi watuhumiwa na kuwasababishia vifo yameripotiwa mara kadhaa kwa miezi ya hivi karibuni, yanayotajwa kwa siku za hivi karibuni ni yaliyotokea Arusha, Vingunguti (Dar es Salaam) na Simiyu.

Mifano ni kama hii, unaweza kusoma hapa:
- Simiyu: Askari wawili wadaiwa kumshushia kipigo kijana na kumsababishia kifo wakimtuhumu kuiba baiskeli

-
Simiyu: Maafisa wa Serikali watuhumiwa kutumia gari la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupora Wakulima kwa silaha za moto

Tukio lingine Simiyu
Askari wa Kituo cha Polisi Bariadi, Mkoani Simiyu wanatuhumiwa kusababisha kifo cha Limbu Kazilo (41) Mkazi wa Mtaa wa Kilulu, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Inadaiwa Kazilo alikamatwa nyumbani kwake Kilulu Desemba 31, 2023 majira ya saa 7 Usiku, muda huo pia alikamatwa ndugu yake aitwaye Sitta Kidanha.

Inadaiwa Askari hao walifika katika mtaa huo wakiwa na gari binafsi aina ya Toyota Noah ambapo ndani ya gari hilo, askari hao walikuwa wameambatana na Wananchi wengine ambao ni wakazi wa mtaa huo.
fcb19e23-9b01-48eb-a6b2-0654f0e2345d.jpeg

Watu wakiwa katika msiba wa Limbu Kazilo

Mama mzazi wa marehemu anasimulia
Nyahoga Nandi ambaye ni mama mzazi wa marehemu anasema “Tuliwaona Askari pamoja na Wananchi wengine wanne ambao ni Wakazi wa hapa, hao Wananchi tuna mgogoro nao wa shamba ambao ni wa muda mrefu sana.”

Anaendelea kusema kuwa walikamatwa kisha kufungwa pingu na kuanza kupigwa, anasema Kazilo alipigwa sana na Askari hao kwa kutumia mpini wa shoka licha ya kuwa alitoa ushirikiano walipofika Kwa ajili ya kumkamata.

Maelezo zaidi…
Mashuhuda wanaeleza kuwa baada ya kukamatwa walipelekwa Kituo cha Polisi Bariadi, ambapo kesho yake ndugu walikwenda kuwaona lakini hawakufanikiwa baada ya Askari kuwaeleza hawawezi kuwaona.

Siku ya Pili ndugu walikwenda tena Kituo cha Polisi Bariadi, ndipo walipomkuta Kazilo akiwa na hali mbaya, Askari waliokuwepo kituono hapo wakawaeleza kuwa wamletee chai kwani alikuwa na hali mbaya.

Askari wadai hawana gari la kumpeleka hospitali
Ndugu anasimulia: “Baada ya kumletea chai, Kazilo alishindwa kunywa, tukawaambia Askari huyu apelekwe Hospitali, wakatueleza hawana gari na mafuta, tukawaambia huyu amepata matatizo mikononi mwenu, hivyo mpelekeni wenyewe, ndipo askari wakatafuta gari na kumpeleka hospitali.

“Ndugu yetu akaanza kupata matibabu huku akiwa kwenye hali mbaya, kwani alianza kutumia mashine kulishwa na kupumua, ilipofika Januari 02, 2024 wakatuambia ndugu yetu amefariki.”

Ndugu wa marehemu wanasema tangu siku amefariki, wamekuwa katika mazungumzo na Jeshi la Polisi kutaka kujua chanzo cha kifo cha ndugu yao.

“Ajabu ni kuwa Askari Polisi wakatugeuka na kusema kuwa eti ndugu yetu aliokotwa njiani akiwa na majeraha, suala ambalo ndugu tumelikataa kwa kuwa wakati wanamkamata sisi tulikuwepo na majirani pia walishuhudia kila kilichokuwa kikiendelea na jinsi walivyokuwa wakitumia nguvu kubwa.”
57f1bdae-c535-4c94-b8a6-de1d80c4f7dc.jpeg

Wanafamilia wakiwa katika mjadala kuhusu msiba wa Limbu Kazilo.

Ndugu wakataa majibu ya Polisi
Baada ya kukataa majibu ya Polisi waliomba kwenda kuona mwili na kupata maelezo ya Daktari katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambapo walifika na kushuhudia mwili ukiwa na majeraha mengi na makubwa mwili mzima.

“Yale majeraha yanaonyesha kabisa kuwa ndugu yetu alipigwa sana, tulimuomba Daktari atupe ripoti ya chanzo cha kifo cha ndugu yetu, Daktari akasema hana uwezo wa kujua chanzo labda waridhie mwili upelekwe Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa ajili ya vipimo vikubwa zaidi ili kujua chazo cha kifo.”

Ndugu wanaeleza kuwa baada ya kuona utata mwingine kutoka kwa Daktari wameamua kuacha mwili kwanza wakati wakiendelea kutafakari na kujadiliana kuona ni hatua gani watachukua kama familia ili kuweza kupata haki yao.

Hata hivyo, wanafamilia hao wanasema kuwa tukio hilo, chanzo chake ni mgogoro wa shamba uliopo baina yao ndugu, ambapo ndugu yao mmoja kwa kushirikiana na watu wengine amekuwa akitumia Jeshi la Polisi kuwanyanyasa na kuwabambikizia kesi lengo likiwa wote waishie gerezani ili aweze kuuza eneo hilo lenye mgogoro.

“Huyu ndugu yetu amekuwa akitutishia, amefanikiwa kuwapeleka gerezani ndugu zetu sita kwa kesi ya mauaji, ambayo haipo kabisa, na kila siku amekuwa akitwambia kuwa wote atatupeleka gerezani ili auze hili eneo,” anasema ndugu kutoka familia ya marehemu.

Asubuhi ya Januari 6, 2024 ndugu wa marehemu wanafanya kikao ili kujua hatima ya mwili wa ndugu yao kisha watatoa tamko la kifamilia.

UPDATES...

MAJIBU YA JESHI LA POLISI

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Maulidi Shaban amesema “Marehemu na mwenzake mmoja walikamatwa wakituhumiwa kesi ya mauaji, marehemu alipofikishwa kituoni akapata homa, akapelekwa hospitali.

"Wakati akiendelea na matibabu akafariki Dunia Usiku wa Januari 2, 2024, ndugu zake wamekataa majibu ya uchunguzi wa hapa (Bariadi) wanataka uchunguzi ukafanyike Hospitali ya Bugando (Mwanza).

"Hivyo na sisi Jeshi la Polisi tunasubiri majibu ya Daktari huko atakapoenda kufanyiwa vipimo, pia kuhusu madai ya kuwa alishambuliwa na Askari wakati anakamatwa pia si kweli, hayo ni maneno tu na ndio maana uchunguzi unaendelea.”

Pia soma - RPC Simiyu asema wanafanya uchunguzi aliyefariki akiwa chini ya ulinzi, ndugu wapeleka mwili Bugando
 
Polisi pale simiyu mkoani ni majambazi nina experience na pale. Something should be done kuna polisi wezi wenye yunifomu.
 
Again hii ni another cold case, sababu uzuzu wa kiuoga wa watanzania, hakuna push back hapa kutoka kwa ndugu au wanajamii wengine, guys in uniforms wanaua tu left/right, yule mzazi wa pale Lindi ambaye binti yake aliuliwa, dada Akwilina etc etc, within two day hii issue itakua cold one
 
Kwa mara nyingine tena, Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu linatuhumiwa kuhusika katika kifo cha Mwananchi aliyekamatwa na Askari Polisi kisha kudaiwa kumpiga na kumsababishia maumivu makali na hatumaye kusababisha kifo chake.

Matukio ya Jeshi la Polisi kupiga au kujeruhi watuhumiwa na kuwasababishia vifo yameripotiwa mara kadhaa kwa miezi ya hivi karibuni, yanayotajwa kwa siku za hivi karibuni ni yaliyotokea Arusha, Vingunguti (Dar es Salaam) na Simiyu.

Mifano ni kama hii, unaweza kusoma hapa:
- Simiyu: Askari wawili wadaiwa kumshushia kipigo kijana na kumsababishia kifo wakimtuhumu kuiba baiskeli

-
Simiyu: Maafisa wa Serikali watuhumiwa kutumia gari la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupora Wakulima kwa silaha za moto

Tukio lingine Simiyu
Askari wa Kituo cha Polisi Bariadi, Mkoani Simiyu wanatuhumiwa kusababisha kifo cha Limbu Kazilo (41) Mkazi wa Mtaa wa Kilulu, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Inadaiwa Kazilo alikamatwa nyumbani kwake Kilulu Desemba 31, 2023 majira ya saa 7 Usiku, muda huo pia alikamatwa ndugu yake aitwaye Sitta Kidanha.

Inadaiwa Askari hao walifika katika mtaa huo wakiwa na gari binafsi aina ya Toyota Noah ambapo ndani ya gari hilo, askari hao walikuwa wameambatana na Wananchi wengine ambao ni wakazi wa mtaa huo.
View attachment 2863267
Watu wakiwa katika msiba wa Limbu Kazilo

Mama mzazi wa marehemu anasimulia
Nyahoga Nandi ambaye ni mama mzazi wa marehemu anasema “Tuliwaona Askari pamoja na Wananchi wengine wanne ambao ni Wakazi wa hapa, hao Wananchi tuna mgogoro nao wa shamba ambao ni wa muda mrefu sana.”

Anaendelea kusema kuwa walikamatwa kisha kufungwa pingu na kuanza kupigwa, anasema Kazilo alipigwa sana na Askari hao kwa kutumia mpini wa shoka licha ya kuwa alitoa ushirikiano walipofika Kwa ajili ya kumkamata.

Maelezo zaidi…
Mashuhuda wanaeleza kuwa baada ya kukamatwa walipelekwa Kituo cha Polisi Bariadi, ambapo kesho yake ndugu walikwenda kuwaona lakini hawakufanikiwa baada ya Askari kuwaeleza hawawezi kuwaona.

Siku ya Pili ndugu walikwenda tena Kituo cha Polisi Bariadi, ndipo walipomkuta Kazilo akiwa na hali mbaya, Askari waliokuwepo kituono hapo wakawaeleza kuwa wamletee chai kwani alikuwa na hali mbaya.

Askari wadai hawana gari la kumpeleka hospitali
Ndugu anasimulia: “Baada ya kumletea chai, Kazilo alishindwa kunywa, tukawaambia Askari huyu apelekwe Hospitali, wakatueleza hawana gari na mafuta, tukawaambia huyu amepata matatizo mikononi mwenu, hivyo mpelekeni wenyewe, ndipo askari wakatafuta gari na kumpeleka hospitali.

“Ndugu yetu akaanza kupata matibabu huku akiwa kwenye hali mbaya, kwani alianza kutumia mashine kulishwa na kupumua, ilipofika Januari 02, 2024 wakatuambia ndugu yetu amefariki.”

Ndugu wa marehemu wanasema tangu siku amefariki, wamekuwa katika mazungumzo na Jeshi la Polisi kutaka kujua chanzo cha kifo cha ndugu yao.

“Ajabu ni kuwa Askari Polisi wakatugeuka na kusema kuwa eti ndugu yetu aliokotwa njiani akiwa na majeraha, suala ambalo ndugu tumelikataa kwa kuwa wakati wanamkamata sisi tulikuwepo na majirani pia walishuhudia kila kilichokuwa kikiendelea na jinsi walivyokuwa wakitumia nguvu kubwa.”
View attachment 2863268
Wanafamilia wakiwa katika mjadala kuhusu msiba wa Limbu Kazilo.

Ndugu wakataa majibu ya Polisi
Baada ya kukataa majibu ya Polisi waliomba kwenda kuona mwili na kupata maelezo ya Daktari katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambapo walifika na kushuhudia mwili ukiwa na majeraha mengi na makubwa mwili mzima.

“Yale majeraha yanaonyesha kabisa kuwa ndugu yetu alipigwa sana, tulimuomba Daktari atupe ripoti ya chanzo cha kifo cha ndugu yetu, Daktari akasema hana uwezo wa kujua chanzo labda waridhie mwili upelekwe Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa ajili ya vipimo vikubwa zaidi ili kujua chazo cha kifo.”

Ndugu wanaeleza kuwa baada ya kuona utata mwingine kutoka kwa Daktari wameamua kuacha mwili kwanza wakati wakiendelea kutafakari na kujadiliana kuona ni hatua gani watachukua kama familia ili kuweza kupata haki yao.

Hata hivyo, wanafamilia hao wanasema kuwa tukio hilo, chanzo chake ni mgogoro wa shamba uliopo baina yao ndugu, ambapo ndugu yao mmoja kwa kushirikiana na watu wengine amekuwa akitumia Jeshi la Polisi kuwanyanyasa na kuwabambikizia kesi lengo likiwa wote waishie gerezani ili aweze kuuza eneo hilo lenye mgogoro.

“Huyu ndugu yetu amekuwa akitutishia, amefanikiwa kuwapeleka gerezani ndugu zetu sita kwa kesi ya mauaji, ambayo haipo kabisa, na kila siku amekuwa akitwambia kuwa wote atatupeleka gerezani ili auze hili eneo,” anasema ndugu kutoka familia ya marehemu.

Asubuhi ya Januari 6, 2024 ndugu wa marehemu wanafanya kikao ili kujua hatima ya mwili wa ndugu yao kisha watatoa tamko la kifamilia.

UPDATES...

MAJIBU YA JESHI LA POLISI

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Maulidi Shaban amesema “Marehemu na mwenzake mmoja walikamatwa wakituhumiwa kesi ya mauaji, marehemu alipofikishwa kituoni akapata homa, akapelekwa hospitali.

"Wakati akiendelea na matibabu akafariki Dunia Usiku wa Januari 2, 2024, ndugu zake wamekataa majibu ya uchunguzi wa hapa (Bariadi) wanataka uchunguzi ukafanyike Hospitali ya Bugando (Mwanza).

"Hivyo na sisi Jeshi la Polisi tunasubiri majibu ya Daktari huko atakapoenda kufanyiwa vipimo, pia kuhusu madai ya kuwa alishambuliwa na Askari wakati anakamatwa pia si kweli, hayo ni maneno tu na ndio maana uchunguzi unaendelea.”
Pole sana kwa Wafiwa. Inauma sana Polisi wamegeuka Mbwamwitu kuangamiza raia wema kwa kisingizio cha Alikuwa mhalifu.
 
Division 4 hizo hata somo la uraia ni F mnazoweka zilinde nchi mnategemea nini ?

Siku hizi kaa chonjo, ukipisha kauli na polisi anakuja kukuua anasingizia wewe Panya road
 
Kuna watu wanashabikia hii kitu toka lile tukio la Dar kwa maelezo mepesi tu ya polisi kwamba et walikuwa wahalifu.

Hii ngoma ikiendelea hivi hata ukimt*mbea tu askari huko mtaani utauwawa na kupewa "beji" ya uhalifu.

Hakuna anayetetea wahalifu ila hii style kwa hawa polisi wetu hata wewe unaweza kuwa mhanga muda wowote.
 
Haya wale wazee wa Black matters
Vita palestina gaza
Mbona haya mauaji mko kimya

Ova
 
Yawezekana marehemu alikuwa mkorofi kupindukia ndio maana na police wakatumia nguvu kubwa mpaka kumsababishia umauti
 
Back
Top Bottom