Mkutano wa Kitaifa wa Haki, Amani na Maridhiano, 2022: Rais Samia asema Maendeleo hayafanywi na CCM na Rais pekee, aahidi ushirikiano na vyama vingine

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
Rais Samia.PNG

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefungua Mkutano wa Kitaifa wa Haki, Amani na Maridiano ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) leo tarehe 05 Aprili, 2022 katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.

=========

Updates:

RAIS SAMIA AMEELEZA HAYA:

Binafsi nikiwa mdau wa demokrasia ya vyama vingi naona kukutana hapa kama fursa adhimu ya kujadiliana, kushauriana na kujenga muafaka, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Nilikuwa naangalia ndani ya chumba hiki kuanzia kwa Komredi Kinana mpaka mstari wa mwisho – wote ni Watanzania. Hapa kuna wageni wasio Watanzania lakini tumewapa jina Wadau au washiriki wa Kisiasa.

Nataka leo tuzungumze Kitanzania ili tuone tunapozungumza Maridhiano, ambayo ndiyo nataka kuanza nayo, tuone tunazungumza vipi, tunaridhiana wapi, katika maeneo yepi, tunakwenda mpaka wapi. Na haya Maridhiano ndiyo sasa.

Tukitoka kwenye Maridhiano tunakwenda kwenye Haki. Haki zetu ni zipi kama Watanzania. Haki zetu kama Vyama vya Siasa ni zipi. Tutazizungumza haki zetu na pale tulipobinya haki hizo tuweze kuzifungua. Lakini kwa mazingira yetu ya Kitanzania.

Tukitoka hapo sasa tunakwenda kudumisha Amani ya nchi yetu. Hakuna atakayetusaidia kwenye hili - ni sisi. Tutasaidiwa kukusanyika hapa, tutasaidiwa maposho na usafiri lakini haya matatu, ni sisi. Kwahiyo kaeni, zungumzeni tuone tunaenda vipi.

Unapozungumza Haki, ujue ya kwako inapoishia basi ya mwenzako ndiyo inapoanzia. Usije kujadili ya kwako ukataka kubinya ya mwenzako.

USHIRIKIANO NA USHIRIKISHWAJI TOKA SERIKALINI UPO 'GUARANTEED'
Tulichagua kuingia mfumo huu wa Vyama Vingi tukijua kwamba ndani ya mfumo huu tutakwenda kupata maendeleo ya haraka kwasababu macho yapo mengi, vyama vipo vingi na maono yapo mengi.

Ndiyo maana tukasema vyama vingi hivi kazi yake ni kuangalia yanayoendelea, yanayofanywa na serikali na kutoa maoni yao kwamba “Jamani, mmepanga hivi, mnakwenda hivi – lakini mbona tunaona hivi?”

Kwa Serikali kazi yetu ni kuwashirikisha katika hayo. Nami nataka nitoe ahadi kwenu kwamba tutashhirikishana katika haya. Kwasababu Tanzania hii haitajengwa na mtu mmoja. Haitajengwa na chama kimoja. Wote kama Watanzania lazima tujadili mambo yetu – iwe sera, iwe sheria, iwe dira.

Na tukikubaliana tunaenda kutekeleza wote kama Watanzania. Atakayekiuka hapo ni mkosa. Awe ametoka kokote kule, ni mkosa.

Kwahiyo niseme kuwa ushirikiano au ushirikishwaji kutoka Serikalini ni guaranteed.

Nafurahi kuwa katika mkutano huu wamealikwa watu mbalimbali: Taasisi za kijamii, vyama vingine, washirika wetu wa maendeleo. Ni utanuzi wa wigo wa mawazo. Na nimeambiwa hapa leo mtazungumza Mapendekezo ya Rasimu ambayo imetayarishwa na wenzetu.

MAENDELEO HAYAFANYWI NA CCM NA RAIS WAO PEKEE
Ndugu zangu, leo siyo siku ya kusema makubwa sana. Makubwa mtazungumza wenyewe. Kuna vichwa vingi hapa, vyenye akili kuliko zangu. Nimekuja hapa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye nina wajibu na dhima ya ulezi na ulinzi wa Amani ya nchi hii. Ndiyo maana nikaitwa Amiri Jeshi Mkuu.

Matumaini yangu kwenu ni kuwa mtajadili vyema na kuleta mapendekezo yatakayokwenda kuweka Amani katika nchi yetu. Nasema Amani kwakuwa jitihada tunazofanya kujenga uchumi wetu, nchi yetu, underlying condition ni Amani, Maelewano na Mshikamano.

Maendeleo yale hayafanywi na Chama cha Mapinduzi na Rais wao peke yao, hapana. Maendeleo yale yanafanywa na kila Mtanzania.

TUTAKUWA TUMERUDI UCHUMI WA KATI IFIKAPO 2025
Twendeni tukalinde maendeleo yanayoendelea sasa hivi. Tanzania yetu ilikwenda tukafika Uchumi wa Kati na kisha tukarudishwa kwa uwezo wa Mungu, wala si kwa uwezo wa mtu. Kwa sasa kazi yetu ni kupambana kurudi tulipokuwa, tusije tukarudishwa tukaambiwa hatufai kuwa kule.

Kwa mipango na jinsi ninavyoiendesha Serikali, nina imani tutakapofika 2025 kama hatujafika tutakuwa tunatarajia kwani mwaka ninatarajia mwaka ujao tunakwenda kukua kwa asilimia 5; miaka miwili inayokuja tutakwenda kufika kwenye 6.8 tuliyokuwa tukikua before. Kwahiyo, hiyo si nguvu ya mtu mmoja. Ni nguvu yetu wote Watanzania.

UPO UTAYARI WA KUBADILISHA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA, ILA KAMA HAIPO 'CONTROVERSIAL'
Mwenyekiti amaeomba mwaka huu tukiwa tunaadhimisha miaka 30 ya Mfumo wa Vyama Vingi, Julai mwaka huu tuwe tumekuwa tumefanya maboresho ya Sheria za Vyama vya Siasa. Sasa inategemea mtakavyotuletea na sisi tutakavyochuja kwa mazingira yetu. Lakini kama haitakuwa controversial.

Kama itakuwa controversial itabidi tukutane – vikao baada ya vikao mpaka tufike. Kama haitakuwa controversial tunaweza kuimaliza kwenye muda huo ili tukasema kwamba Sheria yetu ya Vyama vya Siasa tumeibadilisha baada ya miaka 30. Hili halina shida.

SUALA LA RUZUKU KWA TCD LINAZUNGUMZIKA
Kuhusu suala la Ruzuku kutoka serikalini kwa TCD. Aaah! Kwa bajeti ijayo umechelewa Mwenyekiti kwasababu nimeshaweka sealing na tumeshagawa bajeti. Ila, linazungumzika. Linazungumzika.
 
Binafsi ninaanza kupata matumaini ya kuishi kwenye Tanzania mpya.

Mipango ya kisiasa, kiuchumi na kijamii inayofanywa na awamu hii ya uongozi wa nchi, kwa kiwango kikubwa inaleta matumaini makubwa ya matumaini haya kutimia.

Nachelea kusema hata kauli ya MITANO TENA, kwa mara ya kwanza katika miongo zaidi ya mitatu inaanza kuniingia akilini.

Nadhani muda utaongea zaidi.
 
Huyu mama ana maneno matam sana sasa sijui utekelezaji wake utakuaje hauwezi kutekelezwa kwa sababu ya asili ya watu alio nao kwenye CCM ni watu wasio penda madiliko au ni watu wanao amini kuwa wao ndio wana haki ya kuongoza NCHI kwa hiyo nina uona ugum uko mbaeleni
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anafungua Mkutano wa Kitaifa wa haki, Amani na Maridiano Tanzania leo tarehe 05 Aprili, 2022 katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.

Updates:

RAIS SAMIA

Binafsi nikiwa mdau wa demokrasia ya vyama vingi naona kukutana hapa kama fursa adhimu ya kujadiliana, kushauriana na kujenga muafaka, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Nilikuwa naangalia ndani ya chumba hiki kuanzioa kwa Komredi Kinana mpaka msatari wa mwisho – wote ni Watanzania. Hapa kuna wageni wasio Watanzania lakini tumewapa jina Wadau au washiriki wa Kisiasa.

Nataka leo tuzungumze Kitanzania ili tuone tunapozungumza Maridhiano, ambayo ndiyo nataka kuanza nayo, tuone tunazungumza vipi. Tunaridhiana wapi, katika maeneo yepi. Tunakwenda mpaka wapi. Na haya Maridhiano ndiyo sasa.

Tukitoka kwenye Maridhiano tunakwenda kwenye Haki. Haki zetu nizipi kama Watanzania. Haki zetu kama vyama vya Siasa ni zipi. Tutazizungumza haki zetu na pale tulipobinya haki hizo tuweze kuzifungua. Lakini kwa mazingira yetu ya Kitanzania.

Tukitoka hapo sasa tunakwenda kudumisha Amani ya nchi yetu. Hakuna atakayetusaidia kwenye hili - ni sisi. Tutasaidiwa kukusanyika hapa, tutasaidiwa maposho na usafiri lakini haya matatu, ni sisi. Kwahiyo kaeni, zungumzeni tuone tunaenda vipi.

Unapozungumza Haki, ujue ya kwako inapoishia basi ya mwenzako ndiyo inapoanzia. Usije kujadili ya kwako ukataka kubinya ya mwenzako.

Tulichagua kuingia mfumo huu wa Vyama Vingi tukijua kwamba ndani ya mfumo huu tutakwenda kupata maendeleo ya haraka kwasababu macho yapo mengi, vyama vipo vingi na maono yapo mengi.

Ndiyo maana tukasema vyama vingi hivi kazi yake ni kuangalia yanayoendele, yanayofanywa na serikali na kutoa maoni yao kwamba “Jamani, mmepanga hivi, mnakwenda hivi – lakini mbona tunaona hivi?”

Kwa Serikali kazi yetu ni kuwashirikisha katika hayo. Nami nataka nitoe ahadi kwenu kwamba tutashhirikishana katika haya. Kwasababu Tanzania hii haitajengwa na mtu mmoja. Haitajengwa na chama kimoja. Wote kama Watanzania lazima tujadili mambo yetu – iwe sera, iwe sharia, iwe dira.

Na tukikubaliana tunaenda kutekeleza wote kama Watanzania. Atakayekiuka hapo ni mkosa. Awe ametoka kokote kule, ni mkosa.

Kwahiyo niseme kuwa ushirikiano au ushirikishwaji kutoka Serikalini ni guaranteed.

Nafurahi kuwa katika mkutano huu wamealikwa watu mbalimbali: Taasisi za kijamii, vyama vingine, washirika wetu wa maendeleo. Ni utanuzi wa wigo wa mawazo. Na nimeambiwa hapa leo mtazungumza Mapendekezo ya Rasimu ambayo imetayarishwa na wenzetu.
Hana mvuto huyo maza
 
Huyu mama ana maneno matam sana sasa sijui utekelezaji wake utakuaje hauwezi kutekelezwa kwa sababu ya asili ya watu alio nao kwenye CCM ni watu wasio penda madiliko au ni watu wanao amini kuwa wao ndio wana haki ya kuongoza NCHI kwa hiyo nina uona ugum uko mbaeleni
Yeye mwenyewe ni muongo sn
 
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni!, Zitto is one of the best opposition politician in Tanzania, Leo ameongea vizuri sana kwenye Mkutano huu.
P

Leo ndio ameongea vizuri, kwahiyo siku nyingine huwa haongei vizuri? Shida ni kuwa hatuna imani na huo mkutano maana kinachozungumzwa sio kinachotekelezwa. Ni mkutano ceremonial zaidi.
 
Ukiwa mjinga unaweza kufikiri kuwa ni kweli kuna mikutano ya haki,amani na maridhiano inaendelea Tanzania.
 
Huyu mama ana maneno matam sana sasa sijui utekelezaji wake utakuaje hauwezi kutekelezwa kwa sababu ya asili ya watu alio nao kwenye CCM ni watu wasio penda madiliko au ni watu wanao amini kuwa wao ndio wana haki ya kuongoza NCHI kwa hiyo nina uona ugum uko mbaeleni
Mama Imani ya Dini yake inambana sana, ndiyo maana anajaribu sana kwenda nao Kibinaadamu,lakini tatizo walengwa,na wao vichwani mwao Wana yao wanaoyawaza na kuyataka!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom