Kinana aitaka chadema kuthamini nia njema ya rais samia katika maridhiano

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
KINANA AITAKA CHADEMA KUTHAMINI NIA NJEMA YA RAIS SAMIA KATIKA MARIDHIANO.

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU Makamu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana, amesema nia njema iliyooneshwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kutaka maridhiano inapaswa kuendelezwa na vyama vyote vya siasa.

Aidha, amevishauri vyama vya siasa vya upinzani hususan CHADEMA kuacha kufanya maandamano yasiyo na msingi badala yake wathamini utayari wa Dk. Samia katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa katika maendeleo yakiwemo ya demokrasia.

Kinana ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, ambapo alitumia muda mwingi kuzungumzia, maridhiano yaliyoingiwa kati ya CCM, CHADEMA na vyama vingine vya upinzani nchini.

Kinana aliitaka CHADEMA kueleza ukweli kuhusu mambo mazuri yaliyopatikana baada ya kuwepo kwa maridhiano ikiwemo serikali kukipatia chama hicho ruzuku ya Sh. bilioni 2.7 ambayo waliikataa kwa miaka mitatu nyuma.

Akielezea kuhusu sheria mpya, Kinana alisema pamoja na uzuri wake ikiwemo kuzingatia maoni ya wadau wakiwemo CHADEMA wenyewe, lakini bado kinasema haifai.

“Nilifikiri sheria hii mpya wangesema itatufikisha mbali zaidi, lakini wao wanasema hii haifai, basi turudi kule. Sheria ya sasa ni bora kwa muundo, kwa maudhui, kwa malengo, kwa dhamira sijui mnanielewa?. Nitumie nafasi hii kuwasihi ndugu zangu wa CHADEMA waungane na Watanzania waachane na mandamano, waangalie dhamira ya Rais.

“Hivi Rais na baraza lake la mawaziri kama wasingepeleka hii sheria mpya ya uchaguzi nani angemlazimisha? Lakini Rais busara imemuongoza akasema hapana hebu twende pamoja na mimi ndio mtetezi mkubwa wa maridhiano na ustahimilivu. Hebu tupeleke sheria mpya bungeni na kila hoja aliyopelekewa, aliyoambiwa kwamba haya ndio maoni ya wadau Rais akasema sawa, nakubali,” amesema.

== ==
 
Attachments

  • IMG-20240204-WA1894.jpg
    IMG-20240204-WA1894.jpg
    239.9 KB · Views: 1
  • IMG-20240204-WA1897.jpg
    IMG-20240204-WA1897.jpg
    664.7 KB · Views: 1
  • IMG-20240204-WA1895.jpg
    IMG-20240204-WA1895.jpg
    232.4 KB · Views: 1
Chadema hawajui wanalotaka
Ccm hawana nia ya DHATI ya hayo Maridhiano kwa mfano suala la Wabunge 19 Chadema ilipowafukuza ilipeleka barua Kwa Spika na Tume ya Uchaguzi ili iwaondoe Bunge kwani hawana chama kama Walivyoondolewa Wabunge wa CUF na CCM.lakini wa CHADEMA hawakuondolewa wakasubiriwa Wakate Rufaa kwanza Tofauti n Wabunge wa Cuf na Ccm ilivyokuwa .Ukweli ni kwamba Wabunge 19 wapo kimkakati CCM inawalinda kwa nguvu zote mpaka 2025 na hayo MARIDHIANO hayatawatoa hao bungeni kamwe

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
KINANA AITAKA CHADEMA KUTHAMINI NIA NJEMA YA RAIS SAMIA KATIKA MARIDHIANO.

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU Makamu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana, amesema nia njema iliyooneshwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kutaka maridhiano inapaswa kuendelezwa na vyama vyote vya siasa.

Aidha, amevishauri vyama vya siasa vya upinzani hususan CHADEMA kuacha kufanya maandamano yasiyo na msingi badala yake wathamini utayari wa Dk. Samia katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa katika maendeleo yakiwemo ya demokrasia.

Kinana ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, ambapo alitumia muda mwingi kuzungumzia, maridhiano yaliyoingiwa kati ya CCM, CHADEMA na vyama vingine vya upinzani nchini.

Kinana aliitaka CHADEMA kueleza ukweli kuhusu mambo mazuri yaliyopatikana baada ya kuwepo kwa maridhiano ikiwemo serikali kukipatia chama hicho ruzuku ya Sh. bilioni 2.7 ambayo waliikataa kwa miaka mitatu nyuma.

Akielezea kuhusu sheria mpya, Kinana alisema pamoja na uzuri wake ikiwemo kuzingatia maoni ya wadau wakiwemo CHADEMA wenyewe, lakini bado kinasema haifai.

“Nilifikiri sheria hii mpya wangesema itatufikisha mbali zaidi, lakini wao wanasema hii haifai, basi turudi kule. Sheria ya sasa ni bora kwa muundo, kwa maudhui, kwa malengo, kwa dhamira sijui mnanielewa?. Nitumie nafasi hii kuwasihi ndugu zangu wa CHADEMA waungane na Watanzania waachane na mandamano, waangalie dhamira ya Rais.

“Hivi Rais na baraza lake la mawaziri kama wasingepeleka hii sheria mpya ya uchaguzi nani angemlazimisha? Lakini Rais busara imemuongoza akasema hapana hebu twende pamoja na mimi ndio mtetezi mkubwa wa maridhiano na ustahimilivu. Hebu tupeleke sheria mpya bungeni na kila hoja aliyopelekewa, aliyoambiwa kwamba haya ndio maoni ya wadau Rais akasema sawa, nakubali,” amesema.

== ==
Kinana nadhani ni mjinga anayeamini kila mmoja ni mjinga kuliko yeye.

Umasema ni sheria mpya, upya wake ni nini wakati context na malengo yamebakia yaleyale, ya Rais kujitengenezea mazingira ya kuwa na uwezo wa kuichezesha NEC kama anavyotaka?

Maandamano hayatakuwa ya CHADEMA bali ya Watanzania wote wanaoipenda nchi yao, wanaotaka nchi iongozwe kiuhalisia na siyo kitapeli.

Hapo tulipofika kuna machaguo mawili tu, moja ni Rais Samia kuamua kuongoza nchi kwa dhamira safi na siyo unafiki au utapeli, kisha asubirie na aheshimu maamuzi ya wananchi. Chaguo la pili ni kuwapuuza wananchi na kuamua kuendeleza utapeli wa CCM, kisha asunirie jinsi wananchi watakavyompuuza. Na hakika atajilaani hata kufikia kutamka kuwa aheri asingepata nafasi ya kuwa Rais.

Nyakati zaja atayakumbuka maneno haya.
 
Ccm Bado wanaamini wataendelea kutuchezea ulaghai ule ule wa miaka yote. Wanajificha kwenye maoni ya wananchi, wakati ukweli ni kuwa maoni yalitakiwa yawe ndani ya mswaada walioutunga wao. Maoni yote yaliyokuwa nje ya walichokitaka wao yamepuuzwa.

Hadaa Yao ni ili kupata idadi kubwa ya wapiga kura, maana wanajua wapiga kura wakiwa wachache kama wapinzani watasusia uchaguzi, itaonyesha ni kwa kiwango huwa wana wapiga kura wachache.
 
KINANA AITAKA CHADEMA KUTHAMINI NIA NJEMA YA RAIS SAMIA KATIKA MARIDHIANO.

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU Makamu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana, amesema nia njema iliyooneshwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kutaka maridhiano inapaswa kuendelezwa na vyama vyote vya siasa.

Aidha, amevishauri vyama vya siasa vya upinzani hususan CHADEMA kuacha kufanya maandamano yasiyo na msingi badala yake wathamini utayari wa Dk. Samia katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa katika maendeleo yakiwemo ya demokrasia.
Naunga mkono hoja Nimemwelewa sana Mbowe, usipoteze imani na Rais Samia. Alivyo kwa Kauli na Matendo hawezi kuwa ni yeye!
P
 
Nadhani itakuwa bora hawa makamu wa wenyeviti wakafanya mdahalo live... tueleweshwe ni yapi yalijadiliwa kwenye hayo mazungumzo ya maridhiano na yapi yalikubaliwa na yapi yalikataliwa.
Kinana vs Lissu njooni kwenye live mjadala mtuelimishe wananchi

..naunga mkono hoja yako 100%.

..kufanyike mdahalo kati ya Kinana na Lissu ili tupime hoja zao na kujua ukweli uko wapi.

..katika suala hili vyombo vya habari vimetuangusha kwa kutoandaa mdahalo kuhusu miswada iliyopelekwa bungeni.
 
Najipanga kwa hilo 2025, kwa kuanzia uwe unanifuatilia nina kipindi Channel Ten kila Jumapili saa 3:00 usiku, marudio ni Jumatano saa 9:30 Alasiri. Kipindi cha jana ni hiki
View: https://youtu.be/cQiwZySjhsg?si=-4HRmye7ClGDrC0C
P

..vyombo vya habari mmetuangusha.

..mlipaswa muandae mdahalo unaohusu miswada iliyopelekwa bungeni.

..mnaweza kufanya hivyo sasa hivi ili wananchi wajue ukweli.

..andaa mdahalo wa makatibu wakuu wa vyama.
 
KINANA AITAKA CHADEMA KUTHAMINI NIA NJEMA YA RAIS SAMIA KATIKA MARIDHIANO.

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU Makamu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana, amesema nia njema iliyooneshwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kutaka maridhiano inapaswa kuendelezwa na vyama vyote vya siasa.

Aidha, amevishauri vyama vya siasa vya upinzani hususan CHADEMA kuacha kufanya maandamano yasiyo na msingi badala yake wathamini utayari wa Dk. Samia katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa katika maendeleo yakiwemo ya demokrasia.

Kinana ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, ambapo alitumia muda mwingi kuzungumzia, maridhiano yaliyoingiwa kati ya CCM, CHADEMA na vyama vingine vya upinzani nchini.

Kinana aliitaka CHADEMA kueleza ukweli kuhusu mambo mazuri yaliyopatikana baada ya kuwepo kwa maridhiano ikiwemo serikali kukipatia chama hicho ruzuku ya Sh. bilioni 2.7 ambayo waliikataa kwa miaka mitatu nyuma.

Akielezea kuhusu sheria mpya, Kinana alisema pamoja na uzuri wake ikiwemo kuzingatia maoni ya wadau wakiwemo CHADEMA wenyewe, lakini bado kinasema haifai.

“Nilifikiri sheria hii mpya wangesema itatufikisha mbali zaidi, lakini wao wanasema hii haifai, basi turudi kule. Sheria ya sasa ni bora kwa muundo, kwa maudhui, kwa malengo, kwa dhamira sijui mnanielewa?. Nitumie nafasi hii kuwasihi ndugu zangu wa CHADEMA waungane na Watanzania waachane na mandamano, waangalie dhamira ya Rais.

“Hivi Rais na baraza lake la mawaziri kama wasingepeleka hii sheria mpya ya uchaguzi nani angemlazimisha? Lakini Rais busara imemuongoza akasema hapana hebu twende pamoja na mimi ndio mtetezi mkubwa wa maridhiano na ustahimilivu. Hebu tupeleke sheria mpya bungeni na kila hoja aliyopelekewa, aliyoambiwa kwamba haya ndio maoni ya wadau Rais akasema sawa, nakubali,” amesema.

== ==
Hivi Kinana na ccm wanafikiri hii nchi ni Mali Yao. Yaani wanaona kutenda matakwa ya wananchi na kuheshimu katiba kama ni hisani ya rasi. Sikio la kufa halisikii dawa. Ccm wanafikiri kila anaye wakosowaji ni chadema. Na kila anaye wapiga ni chadema. Ipo siku Hawa maccm watajikuta wanapambana na watu wasio kuwa na kiongozi kama vilivyo tokea sudani. Ndio wa tafuta pakujificha na itakuwa too late.
 
Ccm hawana nia ya DHATI ya hayo Maridhiano kwa mfano suala la Wabunge 19 Chadema ilipowafukuza ilipeleka barua Kwa Spika na Tume ya Uchaguzi ili iwaondoe Bunge kwani hawana chama kama Walivyoondolewa Wabunge wa CUF na CCM.lakini wa CHADEMA hawakuondolewa wakasubiriwa Wakate Rufaa kwanza Tofauti n Wabunge wa Cuf na Ccm ilivyokuwa .Ukweli ni kwamba Wabunge 19 wapo kimkakati CCM inawalinda kwa nguvu zote mpaka 2025 na hayo MARIDHIANO hayatawatoa hao bungeni kamwe

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
CCM ni matapeli
 
Back
Top Bottom