Mapato yatakayotokana na bandari za Tanganyika ni ya muungano na Zanzibar inapata mgao wake achilia mbali mgao wa 4.5% BoT kwa pato linalotokana na rasilimali za Bara.

Sasa hivi Zanzibar wanampango wa kulipa wajumbe wa nyumba kumi mishahara. Tayari wazee wanalipwa pensheni na waliobaki wanatumia umeme bure. Hapo hawajui gharama za ulinzi , mambo ya ndani na nje au taasisi zingine za muungano.

Huyu Mbarawa anakuwaje waziri wa jambo lisilo la muungano? Sasa Rais wa JMT ni Mzanzibar, Rais wa SMZ ni Mzanzibar na Waziri ni Mzanzibar. Nani anamtetea Mtanganyika kwa usawa huo.

Uuzwaji wa bandari hauna uchungu isipokuwa kwa Watanganyika.
Nyerere, Mkapa, Kikwete , JPM walijua hilo hawakuwahi kufikiria. Walijua ni rasilimali na hazina za Watanganyika
Mwinyi aliuza Loliondo ''ujombani'' akiwa na Waziri Diria. Historia bwana!



JokaKuu Pascal Mayalla
Na unaambiwa hii inchi ina wanausalama wa kimkakati wabobevu!!
KmaNyoKo##*
 
A huge miscalculation by SSH. Watanzania (watanganyika) wameibiwa sana kwa mgongo wa ubinafsishaji, yaani serikali inatumia matrilioni kuwekeza kwenye kitu alafu mwisho wa siku wahuni wachache wanapiga dili na kuuziwa kwa bei za kutupa.

Imetokea tena na tena na tena, ATCL, TTCL, TRC, NBC, mashamba ya serikali, nyumba za serikali, viwanda vya serikali na mengine mengi. Bado CCM haijifunzi tu??

Watu wanamlaumu JPM kuwa alikuwa katili lakini bwana yule alikuwa na akili za kutatua changamoto, akiona sehemu kuna mapungufu basi anaumiza kichwa kuona taitizo ni nini, watu? Mifumo? Sheria? Kisha anajaribu kutatua.
Una point sana ila umemaliza vibaya, eti Jiwe alikuwa na akili
 
Miongoni mwa siri zilizofichuliwa leo kuhusu Mkataba wa kuiuzia kampuni ya Waarabu Bandari za Tanzania, imo habari kwamba Bandari zitakazohusika ni zile za Tanganyika Pekee, za Zanzibar hazitahusika.

Ikumbukwe kwamba Bandari ni miongoni mwa mambo ya Muungano, ikiwa kama jambo hili lina faida kwanini tunaitenga Zanzibar. Je, Wazanzibar hawataki faida?

Bali kitu pekee ambacho tumekiona ni kwamba Waziri Aliyesaini Mkataba huu anayeitwa Makame Mbarawa anatokea upande wa Zanzibar kama alivyo Rais Samia Suluhu Hassan.
mh!!!
 
..ni kwasababu Watanganyika tuna tabia ya kulala usingizi tukidhani tuko salama ktk serikali ya muungano.

..hii sio mara ya kwanza Rais wa muungano toka Zanzibar kuteua Mzanzibar ktk wizara isiyo ya muungano, halafu waziri huyo kuanza kutenda ndivyo-sivyo.
Kusema kweli, waziri yule anazingua. Mambo hayaendi kabisa.
By the way, zipi ndio wizara za muungano?
 
kuna tanzaniaa na zanzibar... ila tanganyika haipoo tena! huu mkatabaa wa kifalaaa huyu mzanzibar mwenzao kaona ndugu zake wasiwepoo... sisi mazombi ya baraa ndo tuzagamuliwee na waarabu
Mpaka bandari ya KIBIRIZI mmmmmmae
FB_IMG_1686304029827.jpg
 
Mimi kama mtanganyika ninaona kabisa nchi yangu inawekwa rehani na mzanzibari ambaye ameamua kudidimiza upande wa bara kwa kuuza kitovu chetu cha uchumi na hakufanya hilo kwao.

Usalama wetu unawekwa rehani pia.

Ninadhani endapo jambo hili lingekuwa na manufaa basi bandari za Zanzibar zingehusishwa pia.

Ombi langu ni kuwa miradi hii ikafanyike Zanzibar, jengeni huko bandari kubwa kuliko zote duniani, sisi tuacheni.
 
Back
Top Bottom