Matokeo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 24, 2019: CCM yashinda kwa 99.9%, CHADEMA wapata Kijiji kimoja na Vitongoji 19, CUF nao Kijiji

Yaani huyu Jasho nae akili zake ziko kwa wake zake tu....nimecheka badala ya kununa
IMG-20191125-WA0094.jpeg
IMG-20191125-WA0089.jpeg
 
Yale yale waliokuwa wakiyafanya Zanzibar ndio hayo hayo wanayowafanyia nduguzao sasa maana hiyo ndio siasa ya chama Dola inayo shindwa kutowa ushawishi na kushindwa kutowa hoja za maana.,sasa wanautumia vitisho. Prof Lwaitama amesema kweli kabisa.
 
Mrema kajipendekeza mpa uso umekuwa mweupe utafikiri chotara leo ccm inamlipa unyama wa hali ya juu hadi anasema a nawacha siasa.
 
Jafo kijana kuwa muongo mbele ya wazee huku macho makavu kabisa bila kupepesa ni dalili kuwa umetithishwa uchawi na uzeeni lazima uwe mchawi.
Makabila mengi ya huku bara zamani ilikuwa lazima uuwawe ili kuiponya jamii na mchawi hapo baadae.
Jee kabila lenu halina utamaduni huo?
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwa nafasi ya wenyeviti wa mitaa huku nafasi ya wenyeviti wa vijiji ikishinda kwa asilimia 99.9 wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikishinda nafasi moja ya mwenyekiti wa kijiji na kupata wajumbe 110 wa kundi la wanawake na wajumbe mchanganyiko.

Vyama vingine vya CUF, ACT Wazalendo, UDP na DP vimeshinda baadhi ya nafasi katika uchaguzi huo uliofanyika juzi. Pia vyama vya Chadema, CUF na ACT Wazalendo baadhi ya maeneo wagombea wao walipita bila kupingwa. Akitangaza matokeo hayo ya jumla jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo alisema CCM imepata ushindi mkubwa katika uchaguzi huo.

Alisema katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 kwa jumla ya nafasi 332,160 zote zilizohusika katika uchaguzi huo, ambapo vijiji ni 12,262, mitaa 4,262, vitongoji 63,992, wajumbe kundi la wanawake 106,622 na wajumbe kundi mchanganyiko 145,021. CCM kinara Jafo alisema CCM imeshinda katika nafasi zote 12,260 za wenyeviti wa vijiji sawa na asilimia 100.

Pia wenyeviti wa mitaa imeshinda nafasi 4,263 sawa na asilimia 100, wenyeviti wa vitongoji nafasi 63,970 sawa na asilimia 99.4, wajumbe kundi la wanawake imepata nafasi 106,577 sawa na asilimia 99.96 na wajumbe mchanganyiko nafasi 144,925 sawa na asilimia 99.6 Chadema Alisema kwa nafasi ya wenyeviti wa vijiji imepata nafasi moja, wenyeviti wa mitaa haikupata hata kiti kimoja, wenyeviti wa vitongoji nafasi 19, wajumbe kundi la wanawake nafasi 39 na wajumbe mchanganyiko nafasi 71.

CUF Wenyeviti wa vijiji nafasi moja, wenyeviti wa mitaa nafasi hakuna, wenyeviti wa vitongoji nafasi mbili, wajumbe kundi la wanawake nafasi tatu na wajumbe mchanganyiko nafasi 14 ACT Wazalendo Kimepata nafasi moja ya mwenyekiti wa kitongoji, wajumbe kundi la wanawake nafasi moja, wajumbe mchanganyiko nafasi 11, wakati UDP kimepata mjumbe moja kutoka kundi la wanawake, huku DP kimepata nafasi moja ya kundi la wanawake.

Jafo alisema jumla ya vyama 19 vilishiriki katika hatua mbalimbali za uchaguzi wa serikali za Mitaa ikiwemo CCM, Chadema, CUF, ACT Wazalendo, NCCR Mageuzi, UPDP, NLD, NRA, SAU, ADATADEA, TLP, UDP, Demokrasia Makini, DP, AAFP, CCK, UMD na Chauma. Alisema mikoa ambayo wagombea wa nafasi zote za uongozi wamepita bila kupingwa kupitia CCM ni Tanga, Katavi, Ruvuma na Njombe.

Alisema CCM ilipita bila kupingwa kwa jumla ya nafasi za uongozi 316,474 kati ya nafasi hizo, nafasi ya mwenyekiti wa kijiji 12,028, mwenyekiti wa kitongoji 62,927, mwenyekiti wa mtaa 4,207, wajumbe kundi la wanawake 105,935 na wajumbe kundi mchanganyiko 131,359. Alisema Chadema kilipita bila kupingwa kwa jumla ya nafasi za uongozi 69 ambapo kati ya hizo, nafasi ya kundi la wanawake 27 na kwa kundi mchanganyiko 42.

Pia chama cha CUF kilipita bila kupingwa kwa jumla ya nafasi za uongozi nane, kati ya nafasi hizo nafasi ya wajumbe kundi la wanawake ni tatu na kundi mchanganyiko tano. ACT Wazalendo kilipita bila kupingwa kwa jumla ya nafasi za uongozi 12 ambapo nafasi ya kundi la wanawake ni moja na kundi mchanganyiko ni 11.

Alisema sababu za wagombea hao kupita bila kupingwa ni wagombea wa vyama vingine kutochukua kabisa fomu za kuomba kuteuliwa, wagombea wa vyama vingine kutorejesha fomu, baadhi ya wagombea kutoteuliwa au kuwekewa pingamizi na rufaa kwa kukosa sifa kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa na kanuni za uchaguzi.
 
~walioshinda hawana furaha
~na walioshindwa hawana furaha

ngoma droo
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Kijani noma sana

Nina T-shirt ya kijani nyumbani naenda kuigawa

Nuksi sana kuvaa nguo za kijani hata akili inaharibika.
 
Kama ingekua ukipiga risasi kwenye picha ya mtu anakufa, kunawatu wangeshapotea siku nyingi
 
Naona kuna Watanzania wanasema upinzani umeshidwa. Watanzania ni lazima tujue demokrasia sio siasa na kushidwa kwa demokrasia ni kushidwa kwa Watanzania na sio chama.

Mpaka sasa kuna mafanikio mengi lakini kwenye demokrasia bado hatujaweza kwasababu hatuna utamaduni wa kujituma.

Watanzania wengi nikiwa mojawapo mimi tunaona kama mambo mengine hayatuhusu demokrasia ni ya wale sio mimi.

Najiona mimi sio mwandishi wa habari siwekwi ndani, mimi sio mpinzani biashara zangu ziko sawa, mimi sina mtandao kama huu wa jamii hivyo sitaenda mahakamani, mimi sio sio.

Sasa baadae unajiuliza ni nani atabadilisha nchi kama watu wenyewe ni wapeteshaji kila kitu na bado wanalalamika. Siku ambayo mambo yatapandisha hasira za watu sana ndipo tutainuka.

Hong Kong walikuwa wapeteshaji, Sudan walikuwa wapeteshaji mpaka pale ilipofikia mwisho. Hong Kong waliambiwa demokrasia haina maana na China lakini wamekuja kuona ni muhimu kuliko pesa.
 
Siungi mkono hoja, tumeshindwa vipi wakati hii ndio demokrasia yetu.

Hii ni Tanzania Democracy ambayo ni part of African Democracy, nimeizungumza hapa.


P
 
Wandugu,

Natafuta takwimu za uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika November 2019.

Idadi ya waliojiandikisha nchi nzima.

Idadi ya walipiga kura nchi nzima.

Idadi ya mitaa/vijiji/vitongoji vilivyopiga kura.

Idadi ya waliojiandikisha kwenye mitaa/vijiji/vitongoji vilivyopiga kura.

Idadi ya waliopiga kura kwenye mitaa/vijiji/vitongoji vilivyopiga kura.

Wagombea walipata kura ngapi?

Kura ngapi ziliharibika?

Asanteni.
 
Tume ya uchagzi itakwambia tumevuka lengo tulilojiwekea la idadi ya watu watakaopiga kura,malengo yetu yalikua ni 65% lkn waliojitokeza ni 95% so tumevuka malengo na tunampongeza mh.Rais kwa kuchapa kazi na kutusaidia kuvuka malengo yetu.

Full stop.
 
Idadi ya waliojiandikisha na hususani waliopiga kura huwezi kupata hata kwa ndumba. Labda baada ya awamu hii hizo takwimu unaweza kupata.
 
Back
Top Bottom