Matokeo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 24, 2019: CCM yashinda kwa 99.9%, CHADEMA wapata Kijiji kimoja na Vitongoji 19, CUF nao Kijiji

Mdogo wangu alikuwa msimazi wa uchaguzi alisema kwenye mtaa wake walijiandikisha walikuwa 153 waliokuja kupiga kura ni 6 tu kuanzia saa mbili mpaka saa 10 jioni !Hata hao sita watatu walikuwa ni familia ya mgombea wa CCM
 
Wote mnakumbuka enzi za Sadam Hussein wa Iraqi. Ikumbukwe kwamba Wasuni ni wachane kwa idadi ukilinganisha na washia na baada ya hapo kuna wa Kurds.

Nilikua sijui chanzo cha haya maajabu kwamba Pamoja na upinzani mkubwa Sadam aliokua akiupata toka kwa washia na wakurds, bado kwenye chaguzi za Urais alikua anashinda kwa kwa asilimia 90 na kuna uchaguzi alishinda kwa asilimia mia. Kumbe inawezekana. CCM na mwenyekiti wao wa chama wametutoa tongotongo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Kwanza mwenyekiti wao nasikia hakuwahi kuruhusu ushindani kwenye jimbo lake. Basi hiyo tabia kaihamishia kwenye taifa zima bila kujali anatuharibia mshikamano wetu. Kwa Wakumbukao, kwenye kampeni 2015 huyu bwana alilalamika kuonewa kwa Sadam na aliowaita mabeberu kila alikopita.

Walichofanya CCM ni typical ya enzi za Sadam Hussein kwamba zuia kwa namna yoyote ile mchakato huru wa uchaguzi then tengeneza mazingira raghai kuonesha ushindi wa kishindo.

CCM wanajua kwamba Jinsi siku zinavoenda, Chama kimepoteza uungwaji mkono, kilichobaki sasa hata uchaguzi hawautaki.

Watajitofautisha vipi na kikundi cha watawalao inchi kimabavu, au enzi za ukoloni sijui.
 
Kiuhalisia ssm haiwezi simama kwa hoja ni sawa na mgonjwa bila mashine ya oxygen ( polis) lzm atakufa.Dalili ya chama mfu ni kubebwa badala ya kujibeba.Soma historia za kufa kwa vyama kongwe yafanana,chama chochote kinachobebwa na dollars ni chama mfu lzm kitakufa haihitaji mjadala.Ssm chama chenye nguvu leo kinaogopa chaguzi hadi kinakimbia na mpira,hata mwasisi wake atakuwa akishangaa huko alipo.Chama imara yafaa kibebwe na hoja na si bunduki kulazimisha kukubalika.Chama kibebwacho na mtutu hakina tofauti na makundi ya kihalifu kama alqaeda,isisi,boko,au alshabab hivi vinadumu kwa mtutu.Ssm mpya imekuwa sawa na certified gang criminals hata kumwaga damu kwenye chaguzi
 
Back
Top Bottom