Kuelekea 2025 Vyama vya Siasa vya upinzani vijikite kuwaandaa wagombea mapema kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,111
4,226
Tunapoelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 ni vyema vyama vyote vya upinzani vitakavyoshiriki vikaanza maandalizi mapema kabla giza halijazama.

Wote tunakumbuka uchafuzi uliofanyika katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 ambapo vyama vya upinzani vilipata pigo moja matata tokea kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa. Uchaguzi huo ulighubikwa na uonevu mkubwa sana wagombea wengi wa CCM walijikuta wakipita bila kupingwa kutokana na kinachodaiwa wagombea wengine wa vyama vya siasa walishindwa kujaza fomu kwa usahihi.

Tunakumbuka mwaka 2019 wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa jinsi ambavyo wagombea wa upinzani walivyoenguliwa kiubaguzi kwa kasoro ambazo hazikuwa za Kikatiba na ambazo zingeweza kusahihishwa.

Kimsingi Chaguzi za mwaka 2019 na 2020 zilirudisha nyuma mafanikio ya kuratibu chaguzi na matokeo yake.

Maandalizi yaanze mapema sana, vyama hivyo viteue wagombea wenye uwezo, kwanza wajue kusoma na kuandika. Baada ya kupata competent candidates, vyama viwajengee uwezo masuala mazima ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kujaza fomu kwa usahihi.

Ni aibu kubwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA kukuta kwenye fomu kajaza CDM badala ya CHADEMA.

Naamini wagombea wakipatikana mapema na kujengewa uwezo, basi mchakato mzima wa uchaguzi utapungua kasoro, vyama vya upinzani vitapata wawakilishi wengi Serikali za Mitaa na kuamsha ari uchaguzi mkuu 2025.

Ni hayo tu.
 
Tunapoelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 ni vyema vyama vyote vya upinzani vitakavyoshiriki vikaanza maandalizi mapema kabla giza halijazama.

Wote tunakumbuka uchafuzi uliofanyika katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 ambapo vyama vya upinzani vilipata

Ni hayo tu.
Kuandaa wagombea na mifumo ya Kikomunisti, katika siasa za ushindani wagombea wanajiandaa wenyewe na wanajitokeza kugombea, sio kuandaliwa na vyama.
 
Tunapoelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 ni vyema vyama vyote vya upinzani vitakavyoshiriki vikaanza maandalizi mapema kabla giza halijazama.

Ni hayo tu.
Tanzania hakuna uchaguzi, Bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura. Ni ujinga kusema unaanda wagombea, huko wenzako wanapanga kiwango Cha ushindi wao, na nani wameachie kidogo. Kuendelea kushiriki kwenye uchaguzi ulio chini ya tume ya mwenyekiti wa ccm ni upuuzi kama upuuzi mwingine.
 
Ni maigizo tupu
 
Kuandaa wagombea na mifumo ya Kikomunisti, katika siasa za ushindani wagombea wanajiandaa wenyewe na wanajitokeza kugombea, sio kuandaliwa na vyama.
Hao hao wanaojitokeza na kutangaza nia kuna sababu za msingi za kuandaliwa ili kuepusha kuliwa vichwa juu kwa juu.
 
Mnashiriki uchaguzi kwa tume hii ya ccm,alafu uchaguzi ukiisha mnaanza
Kulialia
Watu wengi hawatoshiriki hizo chaguzi zenu

Ova
 
Kuandaa wagombea na mifumo ya Kikomunisti, katika siasa za ushindani wagombea wanajiandaa wenyewe na wanajitokeza kugombea, sio kuandaliwa na vyama.
Mimi nafikiri sio vibaya vyama vya upinzani kushiriki na kuhakiki form za wagombea wao zimejazwa vizuri na kuchukua evidence kama picha na video kwamba form zipo 100% sawa. Tamisemi ikiwakata kwa kisingizio cha hawakujaza form vizuri waweze ku-challenge hio decision kwa ushahidi tosha na itaongeza nguvu kudai tume huru kwa uchaguzi mkuu ujao.
 
Mpaka Sasa Bado unahitaji hayo Ili kupata nguvu ya kudai tume huru?! Ni kipi ambacho hakipo wazi Bali ndio ushahidi utafufutwe Sasa?
 
Mimi nafikiri sio vibaya vyama vya upinzani kushiriki na kuhakiki form za wagombea wao zimejazwa vizuri na kuchukua evidence kama picha na video kwamba form zipo 100% sawa. Tamisemi ikiwakata kwa kisingizio cha hawakujaza form vizuri waweze ku-challenge hio decision kwa ushahidi tosha na itaongeza nguvu kudai tume huru kwa uchaguzi mkuu ujao.
Wagombea hawatakiwi kuondolewa katika uchaguzi kwa kujaza tu fomu vibaya. Hayo ni mambo ya hovyo sana na kuwakosesha raia haki yao ya kuchagua.

TAMISEMI ndio inatakiwa ihakikishe wagombea wote wamejaza fomu zao vizuri bila kuwaengua.
 
Hao hao wanaojitokeza na kutangaza nia kuna sababu za msingi za kuandaliwa ili kuepusha kuliwa vichwa juu kwa juu.
Kinachotakiwa kupambaniwa kwanza ni huo utaratibu mbovu wa kuwaengua watu kwa technicalities za kijima. Watu wanatakiwa waenguliwa kwenye uchaguzi kama wamethibitika kuhusika katika jinai, sio raia au hawajakidhi vigezo muhimu sana kama vya elimu na umri.
 
Wagombea hawatakiwi kuondolewa katika uchaguzi kwa kujaza tu fomu vibaya. Hayo ni mambo ya hovyo sana na kuwakosesha raia haki yao ya kuchagua.
TAMISEMI ndio inatakiwa ihakikishe wagombea wote wamejaza fomu zao vizuri bila kuwaengua.

Tunajua ilitakiwa iwe hivyo, lakini Tamisemi ikisema wamejaza form vibaya wakati kuna ushahidi wazi wamejaza form vizuri, Tamisemi haitapata hata hiyo nafasi ya kusema huo uongo.

Ingesaidia kwenye vyumba vya wasimamizi na eneo husika lote kuwe na kamera ku -record mchakato wote.
 
Makosa ya kawaida ya kibinadamu hayawezi kukosekana kwa yeyote katika ujazaji wa fomu, kama hawakutaki wakiamua kukuengua wanakuengua tu.
 
Wasishiriki wawachie CCM unaendaje kushiriki mechi wakati referee ana kadi ya uanachama wa timu unayoenda kucheza nayo?
 
Wagombea hawatakiwi kuondolewa katika uchaguzi kwa kujaza tu fomu vibaya. Hayo ni mambo ya hovyo sana na kuwakosesha raia haki yao ya kuchagua.
TAMISEMI ndio inatakiwa ihakikishe wagombea wote wamejaza fomu zao vizuri bila kuwaengua.
Ni sawa uende bank halafu ukosee kujaza deposit slip, kisha wenye bank wakutoe nje, badala ya kukuelekeza ujaze hiyo slip kwa usahihi.
 
Tatizo siyo maandalizi ya Wagombea! Tatizo ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi! Kama hakuna mabadiliko ya sheria za uchaguzi, hata wangeandaliwaje!
 
Tunajua ilitakiwa iwe hivyo, lakini Tamisemi ikisema wamejaza form vibaya wakati kuna ushahidi wazi wamejaza form vizuri, Tamisemi haitapata hata hiyo nafasi ya kusema huo uongo.

Ingesaidia kwenye vyumba vya wasimamizi na eneo husika lote kuwe na kamera ku -record mchakato wote.
Halafu unaenda kushitaki wapi kama umejaza fomu kwa usahihi kisha wakakuengua?
 
Tunajua ilitakiwa iwe hivyo, lakini Tamisemi ikisema wamejaza form vibaya wakati kuna ushahidi wazi wamejaza form vizuri, Tamisemi haitapata hata hiyo nafasi ya kusema huo uongo.

Ingesaidia kwenye vyumba vya wasimamizi na eneo husika lote kuwe na kamera ku -record mchakato wote.
Umeme ukikatika muda mrefu kamera hata hazifanyi kazi pia.
 
Kuandaa wagombea na mifumo ya Kikomunisti, katika siasa za ushindani wagombea wanajiandaa wenyewe na wanajitokeza kugombea, sio kuandaliwa na vyama.

Kama wapiga kura watakuwa wanachagua watu badala ya vyama, hivyo vyama havitakuwa na sababu ya maana ya kuwepo.

Ukiacha nafasi nyeti kama ya rais wa nchi na uwakilishi kwenye majimbo machache, inatosha kwa wapiga kura kujua tu wanachagua chama gani, kama kikiwa chama kilichokamilika.

Huu wito ni sahihi hata kama umechelewa kwa baadhi ya vyama vyetu vya siasa.

Kama mmeamua kuingia kwenye demokrasia ya vyama vingi ambalo ni jambo jema, jaribuni kuwa makini na kujifunza.
 
Back
Top Bottom