Freeman Mbowe: Naagiza ngazi zote za chama ziandae wagombea wa kushinda Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
127
420
Akihutubia kwenye mkutano wa BAWACHA, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe emetoa agizo kwa Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika kuhakikisha ngazi zote za chama nchi zima zinaandaa viongozi wa kugombea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na uchaguzi mkuu mwaka 2025. Viongozi hawa wawe na sifa za kushinda uchaguzi.

"Niwaagize mama zangu, rudini kwenye majimbo yenu kakipangeni chama, kila kitongoji, kila kijiji, kila mtaa. Hakuna kitongoji ambacho kitapita bila kupingwa na CHADEMA katika uchaguzi ujao, hakuna"

Mbowe ameongeza kuwa viongozi wazembe ambao hawataweka watu wa kugombea nafasi za uongozi kwenye chaguzi zijazo watachukuliwa hatua.

Amesema macho yote ya watanzania yapo kwa CHADEMa hivyo ni lazima wasimamishe viongozi kwa kila ngazi.

"Naagiza, na siyo kwa BAWACHA peke yake, katibu mkuu tafadhari na mfumo mzima wa mabaraza yote ya chama, kila kiongozi ahakikishe kila nafasi inayogombewa katika serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, lazima CHADEMA iweke mgombea, na siyo mgombea tu wa kujaza nafasi, mgombea wa ushindani wa kushinda."

Amewataka kwenda kusuka chama kwa nguvu ili waizike CCM kwenye chaguzi zijazo.
 
Kama ndivyo walivyokubaliana chamani hakuna tatizo, lakini kwa tahadhari tu, isijekutokea baada ya matokeo ya 2024 na 2025 zikaanza lawama za kuibiwa kura, huo utakuwa usanii.

Binafsi nionavyo ubaya wa hii kauli ya Mbowe, ni kama vile wanacheza ngoma ya CCM either kwa kujua au kutokujua, hasa nikikumbuka Samia alivyowahi kusema kule ndani kwao hakukaliki...

Sasa kama Chadema wameamua kushiriki uchaguzi naona ni kama vile wamemua wenyewe kujipeleka kwenye mdomo wa mamba kwa tamaa za kupata majimbo, siamini hata kidogo kama wanafikiria kwenda ikulu.

CCM wanaweza kuchakachua matokeo makusudi wakijua lawama zitarudi kwa waliochakachuliwa, yes, kama tunazijua tabia zao miaka yote kwanini tukawaamini na kushiriki uchaguzi?

Kama Chadema wangeweka mkazo kwenye Katiba mpya na Tume Huru kwa namna tuliyoona kwenye yale maandamano, naamini wangefanikiwa kupata kimojawapo kama sio vyote.

Bahati mbaya maridhiano yakageuzwa utapeli na CCM wanayoiamini sasa kwa kutaka kushiriki uchaguzi bila tume huru.
 
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Kauli na matamko aliyotoa Lissu baada ya ile sheria kupitishwa bungeni nilijua ndio msimamo wa chama!
 
Si walisema hawatoshiriki chaguzi mpaka tupate katiba mpya na tume huru ya uchaguzi?

WTF is going on with them?

CHADEMA wanavunja moyo sana wakati mwingine.
 
Kama ndivyo walivyokubaliana chamani hakuna tatizo, lakini kwa tahadhari tu, isijekutokea baada ya matokeo ya 2024 na 2025 zikaanza lawama za kuibiwa kura, huo utakuwa usanii.

Binafsi nionavyo ubaya wa hii kauli ya Mbowe, ni kama vile wanacheza ngoma ya CCM either kwa kujua au kutokujua, hasa nikikumbuka Samia alivyowahi kusema kule ndani kwao hakukaliki...

Sasa kama Chadema wameamua kushiriki uchaguzi naona ni kama vile wamemua wenyewe kujipeleka kwenye mdomo wa mamba kwa tamaa za kupata majimbo, siamini hata kidogo kama wanafikiria kwenda ikulu.

CCM wanaweza kuchakachua matokeo makusudi wakijua lawama zitarudi kwa waliochakachuliwa, yes, kama tunazijua tabia zao miaka yote kwanini tukawaamini na kushiriki uchaguzi?

Kama Chadema wangeweka mkazo kwenye Katiba mpya na Tume Huru kwa namna tuliyoona kwenye yale maandamano, naamini wangefanikiwa kupata kimojawapo kama sio vyote.

Bahati mbaya maridhiano yakageuzwa utapeli na CCM wanayoiamini sasa kwa kutaka kushiriki uchaguzi bila tume huru.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app

..wanaweza kuwa wamepima na kuona hakuna support ya kutosha toka kwa wananchi ktk kususia uchaguzi.
 
Akihutubia kwenye mkutano wa BAWACHA, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe emetoa agizo kwa Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika kuhakikisha ngazi zote za chama nchi zima zinaandaa viongozi wa kugombea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na uchaguzi mkuu mwaka 2025. Viongozi hawa wawe na sifa za kushinda uchaguzi.

"Niwaagize mama zangu, rudini kwenye majimbo yenu kakipangeni chama, kila kitongoji, kila kijiji, kila mtaa. Hakuna kitongoji ambacho kitapita bila kupingwa na CHADEMA katika uchaguzi ujao, hakuna"

Mbowe ameongeza kuwa viongozi wazembe ambao hawataweka watu wa kugombea nafasi za uongozi kwenye chaguzi zijazo watachukuliwa hatua.

Amesema macho yote ya watanzania yapo kwa CHADEMa hivyo ni lazima wasimamishe viongozi kwa kila ngazi.

"Naagiza, na siyo kwa BAWACHA peke yake, katibu mkuu tafadhari na mfumo mzima wa mabaraza yote ya chama, kila kiongozi ahakikishe kila nafasi inayogombewa katika serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, lazima CHADEMA iweke mgombea, na siyo mgombea tu wa kujaza nafasi, mgombea wa ushindani wa kushinda."

Amewataka kwenda kusuka chama kwa nguvu ili waizike CCM kwenye chaguzi zijazo.
kwahiyo ameagiza vikumbo vianze vitongojini, mitaani na majimboni mapema tu 🐒

ni jambo zuri sana kujua wagombea mapema japo ni hatari, ila iwe kwa utaratibu maalumu, vinginevyo ni fujo inayoweza kuleta madhara na uharibifu baina ya wagombea juu ya nafasi Fulani 🐒

Katibu Mkuu weka utaratibu mzuri mapema, vinginevyo manyumbu yataanza kukanyagana, kutekana na kuumizana kwa, kiu ,tamaa na uroho wa madaraka soon 🐒
 
CCM walikuwa wanasubiri CHADEMA ijitoe wachekelee. Pia ACT walikuwa wanasubiria CHADEMA wajitoe ili wawe chama kikuu Cha upinzani. Naona wamepigwa chenga ya mawili.
 
mbowe kachezwa na machale hii kususasusa ni tabia za kike

chadema kariruni kwenye mtanange
 
Back
Top Bottom