Duh, mwingine nakumbuka aliitwa Ota Benga, the Man in the Zoo 1906.

Huyu aliwekwa sehemu moja na nyani na walomtumia kama sehemu ya maonyesho katika mji wa New York city, Bronx Zoo
Yeah. Ota Benga alitoka Congo kwenye familia ya pigmies(Wale watu wafupi) Alikuwa maarufu kwa ufupi wake, meno yake yalochongoka ilipelekea wazungu kusema anakula watu na walimwona kama si binadamu kamili kwa sura yake mbaya. Ota Benga alijiua kwenye cage akiwa na nyani.
 
Katika kabila la Khoikhoi huko Afrika ya Kusini mnamo mwaka 1789 alizaliwa mwanamke mmoja mwenye maumbile makubwa ya kuvutia kama unavyomuona katika picha.

Umbo lake liliwavutia sana wazungu na kufanya mwaka 1810 apelekwe uingereza ambako alitumika kuwa KIVUTIO cha watu kwenye maonesho ya kwenye majukwaa na aliwaingizia pesa nyingi sana wazungu hao.

Mwaka 1814 alihamishiwa Ufaransa ambapo alikuwa akifanya maonesho akiwa uchi (MZUNGU SIO MTU MZURI). Alikuwa akitwa Hottentot Venus (Mungu wa Mapenzi wa Khoikhoi).

Sara akifariki mwaka 1815 akiwa na umri wa miaka 26 na taarfa zinasema alikufa kwa ugonjwa wa zinaa unaoitwa kaswende (Syphilis).

Mabaki ya mwili wake kama fuvu pamoja na sehemu zake nyeti ziliendelea kufanyiwa maonesho katika Makumbusho ya jiji la Paris huko Ufaransa hadi miaka ya 1970's lakini mwaka 2002 mabaki hayo yalizikwa.

Screenshot_20211019-025400_1.jpg
 

Sarah Baartman: Mwanamke mweusi kutoka Afrika Kusini aliyesafirishwa Ulaya kwa maonesho​


Sarah Baartman

Karne mbili zilizopita Sarah Baartman alifariki baada ya kuishi akifanya "maonyesho ya vituko ". Sasa tetesi kwamba kuna uwezekano wa kutengenezwa kwa filamu ya Hollywood inayohusu maisha ya Baartman zimeibua utata.

Sarah Baartman alifariki dunia tarehe 29 Disemba 1815, lakini maonyesho yake yakaendelea

Ubongo wake, mifupa, na viungo vyake vya uzazi viliendelea kuoneshwa katika jumba la makumbusho ya Paris hadi mwaka 1974. Masalia yake hayakuwahi kuhamishwa na kuzikwa mpaka ilipofika mwaka 2002

Aliletwa Ulaya kwa njia za madai ya uongo na daktari Muingereza , akiitwa kwa jina la jukwani "Hottentot Venus", ambapo alioneshwa katika kumbi za "maonyesho ya vituko" mbali mbali katika miji ya London na Paris, huku umati wa watu ukialikwa kuyaangalia makalio yake makubwa.

Lakini sasa anaangaliwa na wengi kama kielelezo cha unyonyaji wa kikoloni na ubaguzi wa rangi, kejeli na utumiwaji wa watu weusi kama vyombo.

Taarifa kwamba Beyonce anapanga kuandika na kucheza katika filamu kuhusu Baartman zilikanushwa na wawakilishi wa mwanamuziki huyo. Lakini minong'ono ilikuwa tayari imesababisha hofu ya kutosha.

Jean Burgess, chifu kutoka kikundi cha Khoikhoi ambacho ndicho alichotoka Baartman , alidai kuwa Beyonce alikosa "utu wa kimsingi wa binadamu kuweza kuwa na thamani ya kuandika hadithi ya Sarah, mbali na kucheza filamu kama Sarah ".

Lakini Jack Devnarain, mwenyekiti wa Shirikisho la wachezaji filamu wa Afrika Kusini alisema kuwa watengenezaji wa filamu walikuwa na ''haki ya kuelezea hadithi za watu unaopata kuwa wanavutia na hilo ndio tunapaswa kuwa waangalifu na hilo".

Hata katika kukanusha kuhusika katika filamu, alisema mwakilishi wa Beyonce : "Hii ni hadithi muhimu ambayo inaweza kuelezewa."

Maisha ya Baartman yalikuwa ni moja ya maisha magumu sana.

Inadhaniwa kuwa alizaliwa katika jimbo la Afrika Kusini la Eastern Cape mwaka 1789, mama yake alifariki dunia alipokuwa na umri wa miaka miwili na baba yake, mfugaji, alifariki alipokuwa katika umri wa kubalehe.

Aliingia katika utoaji wa huduma za nyumbani mjini Cape Town baada ya mkoloni Mholanzi kumuua mwenza wake, ambaye alikuwa tayari amezaa naye mtoto ambaye alikufa.

Mwezi Oktoba 1810, ingawa hakuwa amesoma, Baartman alidai kuwa alisaini mkataba na daktari wa upasuaji wa meli ya Uingereza William Dunlop na mjasiriamali chotara Hendrik Cesars, ambaye alimfanyia kazi kama kijakazi, akisema alisafiri kwenda Uingereza kushiriki katika maonyesho.

Haya yalimfanya asababishe mvuto wakati alipokuwa akifanya onyesho katika eneo la Piccadilly Circus jijini London baada ya kuwasili.

"Unapaswa kukumbuka hilo, wakati ule ,ilikuwa ni kitu kilichokuwa kwenye fasheni na kupendwa kwa wanawake kuwa na makalio makubwa, kwa hiyo watu wengi walimuonea wivu kwa kile alichokuwa nacho cha asili yake, bila kuongezea umbo lake ," anasema Rachel Holmes, mwandishi wa kitabu cha maisha na kifo cha Bi Baartman-The Hottentot Venus: The Life and Death of Saartjie Baartman.

Jukwaani alivaa nguo ya kubana mwili wake ( skin-tight) yenye rangi, pamoja na shanga na manyoya na alikuwa akivuta tumbaku. Wateja matajiri walikuwa wanalipa pesa zao kwa ajili ya kuburudishwa kibinafsi majumbani mwao, huku wageni wakiruhusiwa kumgusa.

Kuwasili kwake nchini Uingereza kulitokea wakati kukiwa na tetesi juu ya iwapo Lord Grenville na muungano wake Whigs - wanaofahamika kama "makalio mapana" kwasababu ya ukubwa wa nyuma wa Grenville- wangejaribu kuiteka serikali . Hii ilikuwa ni zawadi kwa wachoraji wa vibonzo.

Katuni moja, iliyokuwa na kichwa cha habari-A Pair of Broad Bottoms, iliwaonesha Grenville na Baartman wakiwa wamesimama mmoja nyuma ya mwingine, huku mtu mwingine akipima ukubwa wa makalio yao.

Jumba la makumbusho la Uingereza

Mapromota wa Baartman walimpatia jina la bandia "Hottentot Venus", huku "hottentot" - sasa ikionekana kama udhalilishaji- wakati ule likitumiwa na Waholanzi kuelezea makundi ya Khoikhoi na San, ambao kwa pamoja huunda jamii ya watu wanaofahamika kama Khoisan.

Himaya ya Uingereza ilikuwa imezuia biashara ya utumwa katika mwaka 1807, lakini sio utumwa wenyewe. Hata hivyo, wanaharakati walishtushwa na jinsi Baartman alivyotumikishwa London.

Waajiri wake walishitakiwa kwa kumshikilia Baartman kinyume na matakwa yake, lakini hawakuhukumiwa, huku Baartman mwenyewe akitoa ushahidi uliowatetea.

"Swali linasalia-je Baartman alilazimishwa, kama wanaharakati wa haki za binadamu wanavyodai, au alikuwa katika maonyesho hayo kwa hiari?" anasema Christer Petley, mwalimu wa historia katika Chuo kikuu cha Southampton.

"Iwapo alilazimishwa, lazima alihisi kutishwa kuelezea ukweli katika mahakama. Hatutajua hilo kamwe.

Baada ya kesi, onyesho la Baartman taratibu lilianza kupoteza umaarufu wake miongoni mwa watazamaji katika jiji kuu la London na akaenda katika maonyesho katika maeneo mengine ya Uingereza na Ireland.

Baartman

Mwaka 1814 alihamia Paris na Cesars​

Alikuwa mtu maarufu sana, akinywa kahawa katika mgahawa wa Cafe de Paris na kuhudhuria sherehe za kijamii. Cesars alirejea Afrika Kusini Baartman akawa muonyeshaji mwenye "tabia ya kinyama", akiwa na jina la jukwaani - Reaux. Alikunywa pombe kali, kuvuta sigara nzito na , kulingana Holmes, alikuwa "huenda kahaba" wake.

Baartman akikubali kufanyiwa utafiti na kuchorwa na kikundi cha wanasayansi na wasanii lakini alikataa kuonekana akiwa uchi wa mnyama mbele yao, akidai kuwa hilo lingekuwa chini ya heshima na utu wake - hakuwahi kufanya hili katika maonyesho yake mengine.

Kipindi hiki kilikuwa mwanzo wa utafiti wa kile ambacho kinafahamika kama "sayansi ya rangi ", anasema Holmes.

Baartman alifariki akiwa na umri wa miaka 26. Sababu ya kifo chake ilielezewa kama "majeraha na ugonjwa wa kulipuka". Ilisemekana kuwa hilo lilitokana na maradhi ya kifua, kaswende au ulevi.

Georges Cuvier, ambaye alicheza densi na Baartman katika moja ya sherehe zilizofanyika katika Reaux nchini Ufaransa, alitengeneza kadi iliyoonesha umbile la mwili wake kabla ya kuichana.

Alitunza mifupa yake na kuchukua ubongo wake na sehemu zake za siri, na kuziweka katika birauli na kuiweka kwenye jumba la maonyesho ya binadamu la Paris . Mabaki ya mwili wake yalioneshwa kwenye jumba hilo hadi mwaka 1974, kitu ambacho Holmes anakielezea kama "cha kutisha"

Baada ya kuchaguliwa kwake aliyekuwa rais wa Afrika Kusini 1994 , Nelson Mandela aliomba kuhamishwa kwa mabaki ya mwili wa Baartman na sanamu yake . Serikali ya Ufaransa hatimaye ilikubali na mwezi Machi mwaka 2002 mabaki hayo yakapelekwa Afrika Kusini.

Mwezi Agosti mwaka huo, mabaki yake yalizikwa katika eneo la Hankey, katika jimbo la Eastern Cape province, miaka 192 baada ya Baartman kuondoka akielekea Ulaya.

images - 2021-11-03T070217.239.jpeg
 
Himaya ya Uingereza ilikuwa imezuia biashara ya utumwa katika mwaka 1807, lakini sio utumwa wenyewe.
Bro! hii ipo mpaka sasa, hakuna biashara ya utumwa lakini Utumwa wenyewe upo.. mambo mengi jamii za watu weusi hawana kauli yao,ila wanataka kauli itoke kwa wazungu
huu ni utumwa.....
kuna wakati PSB aliwahi sema KIKITOKA ULAYA NI TECHNOLOGY lakini kikitoka Africa hicho kitu watasema ni Witchcraft......

swali la kizushi, who said the devil is black in colour? and who said Jesus is white in colour?
 
Wakuu ni muda sijapost huku.

Naomba tuujadili ukweli kuhusu Sarah Baartman, mwanamke mweusi aliyezaliwa Afrika Kusini 1789. Inasadikika alifanya kazi kama mtumwa kwa wakati na kugunduliwa kuwa alikuwa na "umbo la ajabu (physical shape). Hivyo akalazimishwa kuchukuliwa kwa nguvu hadi nchini Ufaransa na kuanza kuonyeshwa akiwa "Utupu" kama sehemu ya maonyesho.

Inasadikika pia alitumika vibaya sana kimwili, hali iliyopelekea kifo chake na mwili kukaushwa kisha kuhifadhiwa kwenye majumba yao ya kumbukumbu.

Nimeleta huu mjadala kuchochea udadisi wa kile kichotokea Wakati wa ukoloni. Sina nia mbaya.

Ahsanteni...na karibuni mezani-
Ogaaah! Ilkuwa INARUHUSIWA kufanya naye ngono KWA kulipia na waliingizwa pesa nyingi sana
 
71808ceacf4d40229004550952b85dbb



Saartjie (Sara) Baartman was one of the foremost people of shading known to be persecuted to human sexual managing. She was disparagingly named the "Hottentot Venus" by Europeans as her body would be transparently examined and uncovered savagely all through the term of her young life.

Baartman was first shown in London in the Egyptian Hall at Piccadilly Circus on November 24, 1810. Her public treatment, regardless, quickly drew the thought of British abolitionists who charged Dunlop and the Cezars with holding Baartman without needing to.

e9b91c9aeedf4d81a7655df1651d5c72


Source :



https://www.blackpast.org/overall african-history/baartman-sara-saartjie-1789-1815/
Did Sarah Baartman have any children?
She finally moved to be a wet-sustain in the group of Peter Cesars' kin, Hendrik Cesars, outside of Cape Town in present day Woodstock. There is verification that she had two youths, but both passed on as youngsters.
Source :

https://www.encyclopedia.com/humanistic systems/reference books accounts records and-guides/hottentot-venus
Baartman was brought into the world to a Khoekhoe family close by the Camdeboo in what is as of now the Eastern Cape of South Africa, (then, the Dutch Cape Colony, a British state when she was an adult). Saartjie is the little kind of Sarah, in Cape Dutch the use of the unassuming construction customarily exhibited shared trait, appeal or contempt. Her unique name is dark.
Source : Sarah Baartman - Wikipedia
 
Aaaah, hivi inaruhusiwa kuchangiwa kiswahili wakati mada ni ya kiingereza? Ok, sawa.
Huyu dada alikuwa na msambwanda mkubwa wazungu wakambeba hadi ulaya wakamuweka kwenye jumba la maonyesho, ikawa ukitaka unapewa muda wa kumchunguza, sasa katika kumchunguza wakawa wanamla mzigo.

Alifariki kwa sexually transmitted diseases!
 
Huyu ndie sarabatman mwanamke alieteseka enzi za utumwa kuliko wanawake wote kutokana na shepe ama umbo lake alilokuwanalo lililowashangaza wazungu i alikua raia wa south Africa mwaka 1843
FB_IMG_1651121639007.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha!!

Alichorwa kama chombo cha starehe, na kuwaingizia watu vipato kwa kumfanya kama maonyesho.
 
main-qimg-24c8330be61808115dac1632fd2d316b.jpg
Saartjie (Sara) Baartman alikuwa mmoja wa wanawake wa kwanza weusi wanaojulikana kuteswa na biashara haramu ya ngono. Alipewa jina la dhihaka "Hottentot Venus" na wazungu kwani mwili wake ulichunguzwa hadharani na kufichuliwa kinyama katika muda wote wa maisha yake ya ujana. Ukubwa wa makalio yake ndio kilikua kivutio kikubwa kwa wazungu.

Sara Baartman alizaliwa mwaka 1789 katika Mto Gamtoos, sasa unajulikana kama Rasi ya Mashariki nchini Afrika Kusini. Baartman na familia yake walikuwa washiriki wa kikundi cha Gonaquasub cha Khoikhoi. Baartman alikulia kwenye shamba la kikoloni ambapo yeye na familia yake kuna uwezekano mkubwa walifanya kazi kama watumishi. Mama yake alikufa akiwa na umri wa miaka miwili na babake, ambaye alikuwa dereva wa mifugo, alikufa akiwa bado msichana mdogo.

Kufikia miaka yake ya ujana Baartman aliolewa na mwanamume wa Khoikhoi ambaye alikuwa mpiga ngoma. Walikuwa na mtoto pamoja ambaye alikufa muda mfupi baada ya kuzaliwa. Wakati Baartman alikuwa na umri wa miaka kumi na sita, mumewe aliuawa na wakoloni wa Uholanzi. Muda mfupi baadaye, aliuzwa utumwani kwa mfanyabiashara aitwaye Pieter Willem Cezar, ambaye alimpeleka Cape Town ambako alikua mtumwa wa nyumbani wa kaka yake, Hendrik. Mnamo Oktoba 29, 1810, ingawa hakuweza kusoma, Baartman mwenye umri wa miaka 21 alidhani alisaini mkataba na William Dunlop, daktari, ambaye alikuwa rafiki wa ndugu wa Cezar.

Mkataba huu ulimhitaji kusafiri na akina Cezar na Dunlop hadi Uingereza na Ireland ambapo angefanya kazi kama mtumishi wa nyumbani kwa vile kitaalamu utumwa ulikuwa umekomeshwa nchini Uingereza. Zaidi ya hayo, angeonyeshwa kwa madhumuni ya burudani. Baartman angepokea sehemu ya mapato kutokana na maonyesho yake na angeruhusiwa kurejea Afrika Kusini baada ya miaka mitano. Walakini, mkataba ulikuwa wa uwongo kwa maelezo yote na utumwa wake uliendelea kwa maisha yake yote
main-qimg-f6672903cc80cd84cc94aedba782b3b4.jpg
Baartman alionyeshwa kwa mara ya kwanza London katika Ukumbi wa Misri kwenye Circus ya Piccadilly mnamo Novemba 24, 1810. Jinsi alivyokuwa treated hadharani, hata hivyo, ulivuta hisia za wakomeshaji wa utumwa ambao waliwashtaki Dunlop na Cezars kwa kumshikilia Baartman bila ya mapenzi yake. Mahakama ilitoa uamuzi dhidi ya Baartman baada ya Pieter Cezar kutoa mkataba ambao ulikuwa umetiwa saini na Baartman. Baartman pia alishuhudia kwamba hakuwa akidhulumiwa au kuwa treated vibaya.

Baada ya kesi ya Baartman, Umaarufu wake uliongezeka na alizidi kufanya ziara za maonyesho ya makalio yake kwenye nchi tofauti barani Ulaya.

Mnamo Septemba 1814, baada ya kukaa miaka minne huko Uingereza, Baartman alipelekwa Ufaransa na kuuzwa kwa S. Reaux, mtangazaji ambaye alionyesha wanyama. Aliweka Baartman kwenye maonyesho ya umma ndani na karibu na Paris, mara nyingi kwenye Palais Royal. Pia alimruhusu kunyanyaswa kingono na walinzi waliokuwa tayari kulipa unajisi wake. Reaux alipata faida kubwa kwa sababu ya kuvutiwa kwa umma na mwili wa Baartman hususani makalio yake.

Sara Saartjie Baartman alifariki mjini Paris mnamo Desemba 29, 1815 akiwa na umri wa miaka 26. Inakisiwa kwamba alikufa kwa kifua kikuu au kaswende. Hata baada ya kifo chake, sehemu nyingi za mwili wake zilionyeshwa kwenye Makumbusho ya l’Homme (Makumbusho ya binanadamu), huko Paris ili kuunga mkono nadharia za ubaguzi wa rangi kuhusu watu wa asili za Kiafrika. Baadhi ya sehemu za mwili zilibaki kwenye maonyesho hadi 1974.
main-qimg-63fbfce54964f66b7ca90c121d8a17b1.jpg
Mnamo 1994 Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela aliomba rasmi kwamba mabaki ya Baartman yarudishwe Afrika Kusini. Mnamo Machi 6, 2002, mabaki yake yalirudishwa na kuzikwa huko Hankey katika Jimbo la Eastern Cape.
 
Back
Top Bottom