Ukisha sema hujui kwa nini nchi yako ni masikini tayari unakuwa umekwepa maswali million. Kila swali zuri utaendelea kusema hata mimi najiuliza vivyo hivyo. Huo ni Ujanja wa kitoto ambao Rais wa nchi hatakiwi kusema hata siku moja.

Rais alitakiwa kuelezea ndoto yake alo kuwa akiiota kila siku katika kipindi chote cha miaka 10 kabla ya kujiandaa kuwa rais wa nchi.
Unajua nini? Ukienda Ikulu bila mikakati na agedna zako mwenyewe za kuikwamua nchi kiuchumi, Kisiasa na kiutamaduni ukifika huko utapewa KIONGOZI CHA MWALIMU na Mafisadi ili usome majibu ya namna ya kuiongoza nchi.

Mtu aliye jiandaa miaka 10 kuwania kiti cha Urais hawezi kusema hajui kwa nini nchi yake ni masikini.Labda tu kama agenda yake ya kuwa rais wa nchi ina uhusiano na Ufisadi.
Mwonekano wa Tanzania na Watanzania wake ni kama tumetoka kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa kutumia mishale,pinde na mundu. Nchi iko hoi bin Taabani halafu Mshenzi Habithi huyu( JAKAYA KIKWETE) anadai hajui kwa nini tuko nyuma?

Kuna majibu yanaudhi hasa Msemaji akiwa ni Rais wa nchi.

Nikimwuliza leo hii ni kipi kina idadi kubwa kati ya vifuatavyo atasema nini.

A Matrekta ya wakulima wote Tanzania.

B Mashangingi ya serikali


Nikimwuliza leo hii kwa nini anatibiwa nchini Ufaransa hata ugonjwa wa mdogo tu wa shibe atasema nini?
Kwa sababu amefanya kila linalo wezekana huko Muhimbili na Muhimbili haijaweza kuwa Sibitali ya hadi yake?

Mfalme wa Japan aliwahi kutembea bila Viatu kwa muda fulani hadi siku nchi yake ilipo tengeza viatu kwa wanchi wake.

Japan enzi hizo walikuwa wakiagiza viatu toka China.

Leo hii sisi ile List ya Mafisadi na Makuadi wao telke ambao hawajatajwa wanashindana na kukogana kwa kuvaa viatu vya Mtaliano halafu majibu yao "Sijui kwa nini Tanzania iko nyuma?" Ya kweli hayo??

Ingekuwa vema kwa rais wa nchi kugoma kutibiwa nje ya nchi mpaka kieleweke pale Muhimbili.

Hivi serikali inashindwa kabisa hata kuanzisha VIP wing ya Muhimbili kwa ajili ya Viongozi wa serikali na kuindeleza hatua kwa hatua kwa kuipanua kila mwaka wa fedha hadi iwe ni Sibitali ya kila Mlalahoi?????

Akili nywele kila mtu ana zake, sasa sijui Mungai na kipara chake bado anaakili?

Mwalimu wangu wa somo la Critical Thinking aliwahi kuniambia njia rahisi ya kutambua matatizo yako na kutafuta masuluhisho yake ni kujiuliza maswali?

Marekani ni chi tajiri na iko dunia ya kwanza. Tanzania ni nchi masikini na iko dunia ya tatu kwa nini?

Marekani wanatengeneza matrekta yao wenyewe Tanzania hatutengenezi matrekta yetu wenyewe kwa nini?

Rais wa marekani hatibiwi Ufaransa au katika nchi nyingine yeyote duniani hata kama ugonjwa ni wa kuhatarisha maisha yake, Rais wa Tanzania anatibiwa nje ya nchi hata kama ugonjwa ni kuvimbiwa vitumbua sukari kwa nini?

Maswali yako mengi ambayo Rais Kikwete alitakiwa kujiuliza kabla ya kujiuliza na kujibu swali la kwa nini Tanzania haiendi mbele KIFISADI.

Kuhusu Mikataba ya kuchimba madini Tanzania.

Si kweli kwamba Kuna kipengere kimoja tu cha kutishia maendeleo yetu ndani ya mikataba hiyo, labda kama alisomewa mkataba huo na wasidizi wake.
Mikataba ya madini na makampuni ya uchimbaji yote ni Batili na lazima ibadirishwe kwa nguvu za wananchi kupitia Bunge lao ambalo litakuwa na 45% wabunge wa SISIEMU ifikapo mwisho wa 2010.

Kwa vile Rais Kikwete alisha shiriki kuingia mikataba ya madini na wachimbaji kwa lugha nyingine ameshiriki kuididimiza nchi kwenye lindi la umasikini.

Kikwete amesoma Political Ecomy pale Mlimani, sijui ni vipi anashindwa kujibu swali la nchi ya Tanzania kuwa masikini.
Akiletewa Balance sheet ya kiingiacho na kitokacho Tanzaniia na kinakwenda katika mfuko wa nani, hata kama yey Kikweteni mjinga wa Accounts kama mimi atajua kwamba Hesabu hazijatukali vizuri sisi watanzania.

Kikwete anaiambia Dunia SISIEMU imefanya kila lililo ndani ya uwezo wake kufuta umasikini Tanzania na sasa imefikia mahala imechanganyikiwa na inajiuliza kwanini kijiwe chao Haki Mix.

Maelezo hayo yana maana moja tu SISIEMU si chama cha kutupeleka kwenye maendeleo ila ni mzingo mzito kwa kila raia wa Tanzania.

Ni lazima tuachane na kundi la mbweha watu hao wajiitao SISIEMU walioishiwa mbinu za kujenga uchumi wa nchi.
Ni lazima tuachane na kundi la mbweha watu hawa wajiitao SISIEMU wasio weza kukiri kushindwa, kukiri kuvurunda na kuwa na shingo ngumu kugeukia uelekeo wa maendeleo.

Lazima tuachane na uongozi wa SISIEMU chama muflisi chenye viongozi wenye macho makubwa kama ya Bundi lakini hayatazami na masikio makubwa mithiri ya yale ya Tembo wa lake Manyara lakini hayasikii hata mlio wa radi.

CCM kama chama kimeshindwa kabisa, kwa hiyo sisi watanzania hatuna haja ya kukipa muda wa kuendelea kushindwa.

Endapo baada ya miaka 46 ya kutawala nchi rais wa awamu ya 4 hajui kwa nini nchi yake ni masikini! Sembuse mwanachama wa SISIEMU mlima Kunde kule kijiji cha Mtulingala Malangali?

Najiandaa kwenda gombea Ubunge mwaka 2010 kupitia chama cha upinzani.
Kama mimi sijitokezi na mtu mwingine mwenye uchungu na usongo na nchi yake hajitokezi basi tutaendelea kuongozwa na Mahabithi,Majuha na Mafisadi washenzi hawa milele.

ALUTA CONTINUA MAPAMBANO NDO KWANZA YANAANZA
 
JK anaelewa matatizo ya wananchi na maendeleo hayaji baada ya siku moja. subirini jamani eeehhhhhhhhhhhhh !
 
Yap ! Watu naona wanataka bubble gum development, yaani unatafuna na hapo hapo puto hilo !
 
KadaMpinzani,

hapana ndugu yangu hakuna anayetegemea maendeleo ya Bubblegum hata kidogo lakini hata kutegemea mtoto ni lazima kuwepo na mapenzi kati ya bwana na bibie?.. Huyu JK kiuchumi haonekani kama mwanaume rijali sasa kweli bado kuna mategemeo ya mwana wakati hata mimba hakuna!

Ebu nambie kuna kitu Policy gani ambayo imenzishwa na utekelezaji wake unakupa wewe matumaini ya kuwepoo maendeleo!

Wee hukuona kaulizwa kuhusu mikopo kwamba wananchi wanatakiwa kuwa na hati za kumiliki ardhi ili wapewe mikopo akajibu -Hilo sio tatizo! kisha asitoe solution ama kueleza kwa nini sio tatizo ikiwa wananchi wananyhimwa mikopo!.. Watapata wapi mikopo ikiwa serikali haian mgango wa kuwawezesha wananchi kupata mikopo hiyo!..

Sijui labda mwenzetu kuna kitu unakiona ambacho sisi tumeshindwa kukiona maanake hata hizo mikopo ya Mkukuta na kadhalika wanapewa matapeli wasiokuwa na mashamba wala viwanja... leo hii ni matajiri wababaishaji wasioongeza ajira wala kusimamisha biashara yenye manufaa kwa taifa. Kodi zenyewe wana zikwepa kutkana na contact zao huko TRA. Unategemea maendeleo yatatoka wapi, kwa hao mabillionea 100!
 
na mie nadhani itabidi nikujibu kwa kifupi kama JK alivyofanya (kama ulivyosema hapo juu ) alipoulizwa kuhusu mikopo, lol Mkuu ! anyway niliposema vile nilikuwa na maana kwamba its too early kuanza kusema jamaa kachemka, kuhusu policy hilo sijui maana am not paying too much attention to whats really going on there for me know to everything. Labda tuwaulize waliopo bongo not necessarily wasiwe wanakubaliana/kukataliana na maamuzi ya JK lakini tuwaulize kama kuna policy zozote Muungwana alizoanzisha !
 
KadaMpinzani,

Hakuna haja ya kuwauliza walioko Bongo ila mrengo wa chama na JK haujulikani anachotaka kufanya hivyo inawauia vigumu wananchi kuelewa wanatakiwa kufanya nini..Hakuna policy zozote zinazomhusu mlalahoi! labda hiyo saccos na sijui 1billioni kwa mkoa!... what a joke, ndege kupaa!

Amezungumzia kilimo na hadi hivi sasa ni miaka miwili hatujaona (Policies) mikakati yoyote ile inayowawezesha wakulima.

It's too early ikiwa kuna juhudi fulani zinafanyika ndani ya nchi. Hata wale wenzetu wa Asia na kina Tigers tumeona mabadiliko ya mifumo ya kiuchumi na mikakati bora ndani ya nchi zao kwanza kbala ya wageni kuingia.

Na ni kutokana na mikakati hiyo ndio imewavuta wawekeshaji.. Leo hii huwezi kutegemea mtu kuja Tanzania kuanzisha kiwanda cha nguo ama uzalishaji wa denim hali kilimo kiko chini.

Leo hii Tanzania tunaagiza mahindi, mchele, ngano, vifaranga vya kuku toka nje tena sokoni Dubai na kuvijaza ktk maduka yetu. maendeleo yetu yamekuwa yakitajwa kwa sababu ya kuwepo mali za nje madukani! hata furniture leo zinatoka China tena zina bei kuliko mbao ya Muninga inayotengenezwa TMK...Ukiuliza sababu utaambiwa finishing ya mbao zetu ni mbovu zinapinda, hazina standard inayotakiwa. Korosho yetu bado tunalanguliwa na India tena kuna wachuuzi kibao wa ndani na nje kwa hiyo mkulima hana soko nje isipokuwa kupitia kwa walanguzi.

Sasa kinachopfuata utaona ni kuuza ardhi kwa wakulima toka nje ambao hawana ujanja zaidi yetu isipokuwa mbinu zao na mikakati yao toka kwao inawawezesha kuwa na soko moja kwa moja ndani ya nchi zao.

JK anatakiwa kwenda nje kuweka mikataba ya biashara na nchi hizo kama walivyofanya ktk samaki Sangara badala ya kutafuta wawekeshaji ambao wanakuja na mikataba yao mfukoni kisha sisi tunachoomba ati contribution as if wanatufanyia favour.

Kama nilivyosema JK hadi sasa anatafuta mabasha wa kutembea na mama yetu Tanzania akifikiria kuwa mimba itaweza tungwa na mzungu bila kufahamu kwamba kati ya hawa mabasha wapo wenye magonjwa kama Ukimwi na kadhalika!..

Ndugu yangu, yote haya sio kwamba hayaonekani yapo wazi hakuna haja kabisa ya kusubiri kusimuliwa na kamwe maendeleo ya nchi yetu hayawezi kutoka juu kwa hao mabillionea 100 ila yatakana na kuwawezesha wakulima wetu wapate soko la ndani ambalo litaweza kuinua maisha yao na kuweza ku afford hizo mali zinazoagizwa toka nje.

Besides, RUSHWA mjomba rushwa kubwa kubwa zinatuangusha vibaya sana na wala haihitaji miaka mitano kuweza kuisimamisha....mwenzako sioni ndani kabisa ktk uongozi huu.. nothing will work!
 
NAwashangaa sana Viongozi wetu. SUmaye alisema hilohilo na JK anasema hilohilo. NAdhania kama mtu akitoa sentensi kama hiyo cha kwanza inabidi ajiuzuru, kama hujui tatizo ni nini hakika huwezi kujua namna ya kutatua.

May be Mr President had the answer(Corruption within the party and Govermnent na uroho wa ELs na wenzao) but he was shy to speak it out.
 
Mheshimiwa njoo JF upate sababu:

* Asema anajiuliza swali hilo kila siku bila jibu



...Mungu wangu!... ndio kusema Nahodha kapoteza dira!?, chombo kinakwenda mrama, hala hala asijegonga mwamba ikawa ndio mwisho wa safari!!
 
Siku zote kama hujui mgonjwa wako anaumwa nini ni vigumu kumpatia dawa. JK hajui tatizo la umasikini wa Watanzania, hivyo hawezi kutupatia dawa.Atoke.
Ndo maana tunamwita Msanii.
 
Mtanzania

Hii kali. Kama Raisi haelewi kwa nini tanzania bado ni fukara, huu ni usaliti wa hali ya juu. Moja, naanza kuamini aliyosema Dr.Nchimbi kwamba kazi ya raisi ni kufuga njiwa ikulu yana ukweli.Mbili, nazidi kushawishika kuwa raisi kikwete ni msanii.

Anataka kutuambia muda wote huo aliokaa madarakani toka akiwa waziri, ameshindwa kuona uozo uliopo serikalini???Nchi haina sheria, maadili na kanuni.

Hata kama hayo yapo, hakuna anayetii, kuanzia raisi mwenyewe, mawaziri mpaka askari magereza. Analinganisha matumizi ya mbolea kwa wakulima wa tanzania na uholanzi badala ya kulinganisha ruzuku inayotolewa kwa wakulima katika hizo serikali mbili!! This is utterly non-sense!

OK! Moja, punguza ukubwa wa baraza lako la mawaziri kutoka 30 hadi kufikia 15. Pesa utakayookoa hapo peleka kwenye bararabara, zahanati, na shule.

Mbili, Punguza muda wa vikao vya bunge. Muda wa kukutana dodoma usizidi siku 30 katika siku 366. Hapa utaokoa kiasi fulani cha pesa. Hii pesa toa ruzuku ya mbolea kwa hao wakulima unaokusudia kuwasaidia.

Tatu, timiza ahadi yako ya kupitia upya mikata ya madini. Pesa utakazookoa hapo peleka kwenye sekta ya umeme. Ukihitaji ushauri zaidi nitafute.

Moja, Hii ni porojo!! Mbili, Lini tutakomaa?Tatu, hii kauli inapingana na kauli ya bosi wake (i.e, kikwete) ambaye amekiri waziwazi kuwa mikataba ya nyuma ina mapungufu. Sasa mapungufu maana yake ni nini hasa?? sio kwamba serikali ilikuwa ikiporwa na wawekezaji?

Hivi wee kikwete mbona hawa mawaziri wako wanaboronga sana na wewe unawatazama tu?? kuna mmoja amesema eti wewe kazi yako ni kulinda njiwa ikulu. Huyu membe naye anapingana na kauli zako, kwa nini unawachekea?

Hebu watie adabu hao.
 
Last edited by a moderator:
Hakika sidhani kama kikwete ni rais wa nchi hii!

Hivi huyu ni mshenzi gramu ngapi? kama ukimuuliza kwanini aligombea urais atasema nini? nilikuwa na hasira sana wakati nasoma maelezo ya rais, lakini naona rais wetu hana kabisa uwezo huyu rais sioni kama anastahili kuchambuliwa na watu wasomi, alistahili kuondoka tu kwa kosa la yeye kushindwa kujua umaskini wa Tanzania.

Kifupi kikwete hana sifa ya kuwa rais elimu yake hajawahi kuitumia tangu ametoka chuo kikuu anajua nini huyu katika uchumi bila kufanyia kazi? kama anajua uchumi Tanzania sio maskini viongozi ndio wajinga! hivi kweli rais anakwenda ufaransa halafu anajibu hajui kwanini Tzania ni maskini? hawa wazungu kwanini wanampa kikwete msaada wakati hajui anaomba ili kufanyia nini? ama tuseme wanampa ili nao wapewe buzwagi zetu?

Hakika watz tukimrudisha Kikwete mimi bora nisiseme hata kitu kimoja, niwe bubu tu.

Membe huyu hana kitu hata sihangaiki naye wale wale mtandao, anaongea ujinga.

Eti kikwete anasema aliyekeuka maagizo yake tumuachie! hivi karamagi hajatishia kumshtaki slaa? rais aliwaagiza kila mtu ajibu huoni huu ni usanii? hakika kikwete ni mjinga sisi sio watoto wa kudanganyia pipi?

Nadhani kikwete akapimwe uwezo wa akili ni nakuhahakishieni watz kikwete naona amekwisha Tz haina rais hadi mtakapoamua kumtoa kivuli huyu!
 
Usiwe mbumbu wewe kada! umekuwaje kama hujui unaongea nini? Kuwa nje ya Tanzania si kibali cha wewe kukosa akili! kama hujui hujui tu, huko nje unabeba magunia? Acha ushamba wewe kama mimi, naomba changia unachojua maendeleo ya bubble gum yako wapi na ni uchumi upi huo? Yawezekana uwezo wako wa akili ni duni kikwete hajafanya lolote zaidi ya kutetea mikataba na mawaziri wezi.

karamagi mwenyewe aliiba katika kiwanda cha sementi alikokuwa na kizuri kwa CCM aliwapa milioni 500 kumfikisha kikwete madarakani leo kumfukuza ni issue kikwete anawaza lakini hapati jibu!
 
Kwa kweli sijaona watu wabishi kama watanzania. Sasa Presido kasema ukweli nyie mnakuja juu!! Jk has no idea matatizo ya Tz ni yapi wala yatatatuliwa vipi!! Kudos kwa Jk kwa kuwa mkweli mwezi huu wa mfungo.

Sasa kama Jk anatumia 90% ya muda wake kufungua mashule, kutembelea masoko, kuangalia mpira, kuzunguka overseas na hiyo 10% akiwa Ikulu anafuga na kulisha Pigeons ni saa ngapi atakuwa na muda wa kuangalia policy issues na mikakati mizito?? Give me a break. Rais wetu.

Who wants to bet, kama Presido amerudi bongo this weekend in less than 10 days tutasoma magazetini yuko mkoa fulani!! Akitulia Ikulu for 2 weeks straight, sitaisema serikali hii for 3 yrs.
 
Ukitaka maendeleo ya BubbleGUm ni kwa kuleta hao Foreign investors badala ya ku-promote local investors.
Eg kulikuwa na maana gani kupinga wachimba wadogo wadogo iwe mererani au Buzwagi Geita nk, na badala yake kuwapa exemption hao foreign investors.

Je hao wabongo wange saidiwa hiyo mitambo na kupewa elimu endelevu kulikuwa na maafa gani.?

Pili ni kuweka washikaji ktk serekali badala ya kufuata uwezo wa ntu.

Eg kuna watu walisha vurunda hapo mwanzo, lakini leo hii bado wapo kwenye serekali au kwenye mashirika then unategemea nchi itaendelea eg ATC,

Sasa wao mali ya tanzania wamefanya yakuchezea mdumange, nchi kweli itaendelea hapo, unatetea Mbunge kihiyo, sasa unategemea sera za kimaendeleo zitatoka hapo. Unawekeza kwenye mashangngi badala ya barabara unategemea maendeleo hapo?
 
Naomba nipingane kabisa na maamuzi ya wizara yetu ya madini ya kuweka kipengere kwenye mikataba ya madini kwamba wawekezaji wailipe nchi yetu izo $ 200,000 iwapo tu watapata faida, na si vinginevyo.

To my understanding, mwekezaji yeyote hawezi kujiingiza katika biashara yoyote ya mabilioni (hata ya maelfu ya shilingi) bila ya kufanya kitu kinachoitwa feasibility studies. Katika feasibility study yake, pamoja na mambo mengine, mwekezaji yeyote aliye serious huwa anafanya risk assesment ya investment anayoitegemea kuifanya. Kama mwekezaji anaamua kuingia kichwakichwa katika hiyo business inamaanisha kwamba amegundua kwamba benefits of doing such a business outweigh risks involved. Hivyo mimi nafikiri kwamba serikali yetu inafanya dhambi kubwa mno kuwabeba hawa wawekezaji. JK inabidi a-acknowledge kwamba vitu kama hivi ndio vinasababisha TZ yetu iendelee kuwa masikini. Unapoamua kufanya biashara yoyote lazma ukubali unaingia kwenye risk; Si mara zote utapata faida.. Sometimes unahitajika kutegemea kupata hasara.. Hii ndio maana halisi ya biashara.

Sasa basi, mimi nafikiri kwamba wawekezaji kwenye sekta ya madini katika nchi yetu ni either wameingia kijanja-kijanja ama kuna dirty business inaendelea between hao wafanya biashara na wawakilishi wetu tunaowategemea. It is a SIN for our government kuendelea ku-take risks ambazo ilibidi ziwe taken na hao wawekezaji. To me, I consider this as purely DIRTY BUSINESS.

Issues za kama how to start and run a business, feasibility analysis, risk assessment etc nina uhakika zilikuwemo katika mtaala wa Bachelors degree ya uchumi pale UDSM wakati JK akipiga shule, hivyo nina uhakika anavifahamu vizuri. Vilevile, hivi vitu hata mkulima wa kijijini ambaye hakubahatika hata kuanza darasa la kwanza huwa anavi-apply kila siku katika ukulima ama biashara yake. Ni bora kuwa wakweli na waogopa Mungu tunapotoa statements zetu..
 
Nikifufukammekwisha,

Shukran, hiyo ndio lugha ya biashara ambayo wengi wetu Wajamaa tumeshindwa kuifahamu. Ujamaaa ulitulemaza kiasi kwamba biashara huona kama ni ya mwenye mali, tajiri na wengine wote waliobaki ni watumwa wanaotakiwa kuchukua risk kubadilisha maisha yao.

Kumbe biashara ina risk kubwa sana na mwekeshaji ndiye siku zote mwenye roho mkononi ktk maamuzi yake. Ni mwekezaji anayefanya feasibility study ya Biashara na sio mwenye nyumba ama nchi kufanya study na kuchukua risk kwa sababu ya kuwavutia wawekeshaji.
 
ukifufukatumekwisha,
Hiyo Migodi yao wote, wana ubia nayo, subiri tu haya yote utakuja kuyaona. hizo nafuu wamejiwekea wenyewe. ndiyo maana wanadiriki kuwaambia wananchi kwamba mkataba wa Buzwagi ni safi. hata Rais anasema hizo $200,000 zinatosha. kila kitu hovyo, viongozi hovyo, mikataba hovyo na wawekezaji ni hovyo.

Labda na mimi nimpe somo kidogo Rais, Umasikini wetu unatokana na yafuatayo.
-Hatujawekeza kwenye Elimu inavyostahili.
-Hatukuwa serious na Kilimo
-Tunachanganya siasa na maslahi ya Taifa.
-Tunapenda starehe (kusafiri sana, magari ya fahari n.k) kuliko uwezo wetu
-Uwezo wa viongozi kufikiri ni mdogo (wengi Vilaza)na wengine akili zao zimechoka.
-Wananchi hawana easy access na financial institutions
-Sector isiyo rasmi haijatambuliwa na serikali
-Hatuna Barabara na umeme wa uhakika hivyo kusababisha gharama za maisha kupanda.
-Vikwazo vya ku access market kwenye mazao yetu.
-Hatujawasaidia wajasilimia wetu badala yake tunawanyang'anya na kuwapa wageni
-
 
Upinzani this is a golden opportunity wakiamua kufanya kweli.

advise to Upinzani::

Paint a clear picture to wananchi and not rhetoric ya kina JK.
Say something to wananchi wote nchini::

If the govt can do this, maisha bora yatakuja ASAP.

1) All exemptions will be removed Pronto:: Savings ~~ 500 billion. These funds will be used to construct hospitals all over the country

2) Tourism taxes will go up so hoteliers, safari owners, tour operators blah blah will start paying asap Savings ~~ 100 billion. These funds will go towards fertilizers importation to help wakulima.

3)Mining Taxes and Real renew of contracts will commence ASAP. Savings ~~ 500 billion. To be used for schools

+++++++ plus plus other ideas blah blah


This is a format which Upinzani can start another upcountry tour after this mawaziri nonsense which will gain traction. Now, we will sit and see how the govt can counter that!!!
 
'RAIS Jakaya Kikwete amesema haelewi ni kwa nini Tanzania bado ni fukara ingawa imejaliwa rasilimali nyingi za asili kuliko nchi nyingi za bara la Afrika.

Rais Kikwete aliyasema hayo Oktoba 4, mwaka huu mjini Paris Ufaransa katika mahojiano na Mhariri wa masuala ya Afrika wa gazeti la Financial Times, William Wallis na Mwandishi wa gazeti hilo,Tom Burgis'.
.

Hivi PM aliposema 'ndege yetu inapaa' kumbe Mr prez 'ukiwa rubani mkuu' unairusha ndege bila 'mbawa wala mafuta', na wala hujui unapokwenda ilhali mnataka sie abiria tufunge tu mikanda? I bet hiyo inflight menu mnayotwambia ni 'tonge' kwa picha ya huyo 'sungura'!...

...in truth hii inajionyesha 'binadamu' alivyorahisi kujisahau? Mheshimiwa mR Prez uliahidi maisha bora kwa kila mtanzania kwa sababu zipi? na misingi gani uliojiwekea?, JE misingi hiyo imetekelezeka?, kwa kipindi gani? na kwa mafanikio gani? Kumbuka ulituahidi kasi, nguvu na ari mpya,... sasa iwapo mwaka wa pili tayari 'unamlalamikia' refa, mnh!?...

...Mr Prez, you are losing touch with the reality!... umezungukwa na 'kichaka' cha 'wapambe' ambao ni fisi ndani ya ngozi ya wanakondoo ambao wanatafuna na kufuta midomo yao bila wewe kung'amua, tatizo waliondani ya kichaka hicho wanakujia kwa 'ndio mzee, mambo yote safi mzee, wananchi wanakupenda kweli mzee, usiwe na wasiwasi mzee nyingiiiiiiiiiiii, nawe unaona hakuna linaloharibika.

...mheshimiwa 'RUDI SHULE!, badala ya kula maraha kwenye hoteli za nyota tano, Marekani , Asia na Ulaya, fanya zile ziara zako za kustukiza kwenye masoko yetu uujue ukweli, fanya ziara za kustukiza kwa wakulima wetu, wafanyabiashara wa sokoni kariakoo, huko vijijini, hata kwenu BAGAMOYO 'ujikumbushe' mwananchi anavyoishi, na labda uchungu utakurudia na kujua kwanini hatuendelei!

...Mr Prez, badala ya kujifariji na CNN, BBC, MTV CRIBBS nk, jiburudishe na TVZ, TVT, STAR TV, na kina ITV, ili ujionee ukweli wa mambo na maisha ya kweli ya TANZANIA. vile vile usiwe mvivu wa kusoma magazeti na kudodosa Laptop yako, 'njoo' mwenyewe kupata habari moto moto ndani ya JAMBO FORUMS na forums nyingine 'ujue' mapungufu yapo wapi, badala ya kutegemea 'wasaidizi' kukusomea kila kitu, kuna 'ukweli' mwingine hawakusomei!!!!

...aheri yako ulosema ukweli, kutuingiza machakani na 'ndege yenu', ama kupotea njia ndio kujua njia, basi hujachelewa sana kuitafuta njia, kwani muda ulobakiza kabla ya chaguzi zijazo waweza ukata mzizi wa fitina na kufanikiwa 'machache' ulotuahidi! nasi tu nyuma yako kwa kujua tumekukabidhi nchi utuongoze, na pindipo unahitaji msaaada wananchi wapo nyuma yako kukusaidia umeteleza wapi, kwa masharti ya huyo 'sungura' tumle sote!

 
Back
Top Bottom