Huwezi tegemea wawekezaji wa kigeni ndiyo waendeleze nchi

Masikio Masikio

JF-Expert Member
Apr 12, 2023
1,840
3,375
Miaka ya karibuni kumezuka matukio kadhaa kwa serekali kushindwa kuendesha mashirika yake na imepanga kuwapa wageni, ili ni kosa instead serekali iajiri foreigner ambao wana exposure na sio hawa wasio na exposure na wengi wao ni machawa

Mpaka sasa hivi mabosi wa mwendokasi wangetakiwa wawe na kesi ya kujibu kwa kusababishia serekali hasara umepewa monopoloy kwenye route na bado inakushinda kwelii.

Mashirika ya Tanzania yanakufa kwa sababu mtu anaharibu hapa anahamishiwa kule au hachukuliwi hatua zozote zile za kisheria.

Jambo ambalo watu wengi hawajui mzungu au mwarabu anayekuja kama mwekezaji hawezi kuwa na uchungu na Tanzania hata siku moja.

Kama serekali imeshindwa kuendesha mashirika yake basi ikubali tu haitaweza kuondoa huu umaskini uliotamalaki hapa Tanzania.

Ulaya kupitia ukoloni waliiba rasilimali na wakatengeneza nchi zao na wakaendelea; ile miji mizuri unayoiona ulaya imetokana na ukoloni hasa america kule ndo walivuna kisawasawa.

Mfano nchi za saudi arabia baada ya kuvumbua mafuta waliunda shirika lao la aramco kuendesha na kusimamia shughuli zote za uchimbaji wa mafuta matokeo yake aramco lilikua moja ya mashirika makubwa sana dunia yanayoingiza revenue kubwa na hii imepelekea saudi arabia kuendelea sana na kwa mda mfupi.

Ukienda Qatar, UAE rasilimali zao zote zinashikiliwa na makampuni ya serekali, njoo Nigeria moja ya nchi ambayo ina mafuta mengi utajiri wake wa mafuta iliwakabidhi shell mpaka navyoongea mpaka leo yale maeneo ambayo yapo makampuni ya kigeni yana umaskini wa kufa mtu.

Geita kuna mgodi mkubwa sana wa dhahabu lakini hakuna impact yoyote ambayo Geita imepata kutoka na uwepo wa madini.

Kama Afrika tunataka kuendelea ni kuyaondoa makampuni yote ya kigeni kwa makubaliano ya pande zote ya kuvunja mikataba mbili ili tunufaike na rasilima zetu tofauti na hapo ni uongo.

Kuna approach nyingi nchi itatumia ili kuendelea ila njia rahisi ya kuendelea ni kutumia rasilimali zake njia ya kutumia kodi ni ngumu kwa nchi maskini kama Tanzania.
 
Kipind cha JPM wapinzani walimuashia kunguni eti wanataka wawekezaji 😅😅 Nilikuwa nacheka hizo taasisi walisema JPM alikuwa anapiga pesa huko sasa ngoja waone balaa tena alikuwa Lissu.

Kuna mashirika walitaka yafutwe eti serikali haifanya biashara. Ndio maana nakuambia wanasiasa hawana wanachojua.
 
JKN Rais wa kwanza na baba wa Taifa alianzisha mashirika ya umma 400 lakini watanzania walioaminiwa wakayaua na Mkapa akaja akayauza kwa wawekezaji wa nje.

Watanzania ni wezi sana, waaache wageni wapewe. Nenda maeneo ya Goba na Mbezi ni nyumba za wafanyakazi wa umma hasa TRA ndiyo wanaongoza kuwa mahumba mazuri na magari mazuri.

MATATIZO YA MENEJIMENTI ZA KITAZANIA
-Nepotism, political intervention, government bureaucracy, corruption, laissez faire, theft,

Hiyo Mwendokasi imeanzishwa mwaka 2016, sasa hivi iko ICU

Kampuni ya TANOIL ilianza mwaka 2020 saa hizi mufilisi.

TTCL inapumukia mashine, Posta hawajitambui

Mimi ingekuwa amri yangu ningeitoa Seikali katika biashara na kuacha selta binafsi ndiyo iendeshe biashara. Wao watengeneze sera na mazingira bora ya kufanya biashara

Wawekezaji WAJE WENGI TU, Nyie wezi
 
Hakuna Mzungu anakuja Afrika kuwekeza ili awasaidie Waafrika.

Tunaibiwa tu. Fukuza hawa wazungu tuchimbe madini yetu wenyewe. Tukishindwa bora yabaki ardhini vizazi vijavyo vitajua chakufanya
Huo ndo ukweli
Angalia uwepo wa geita gold mining iliyopo geita hakuna chochote kile walichofanya mji wa hovyo yaan kuna mambo yanatia hasira

Wakiulizwa wanasema wanapata hasara mwaka wa ishirini huu
 
JKN Rais wa kwanza na baba wa Taifa alianzisha mashirika ya umma 400 lakini watanzania walioaminiwa wakayaua na Mkapa akaja akayauza kwa wawekezaji wa nje.

Watanzania ni wezi sana, waaache wageni wapewe. Nenda maeneo ya Goba na Mbezi ni nyumba za wafanyakazi wa umma hasa TRA ndiyo wanaongoza kuwa mahumba mazuri na magari mazuri.

MATATIZO YA MENEJIMENTI ZA KITAZANIA
-Nepotism, political intervention, government bureaucracy, corruption, laissez faire, theft,

Hiyo Mwendokasi imeanzishwa mwaka 2016, sasa hivi iko ICU

Kampuni ya TANOIL ilianza mwaka 2020 saa hizi mufilisi.

TTCL inapumukia mashine, Posta hawajitambui

Mimi ingekuwa amri yangu ningeitoa Seikali katika biashara na kuacha selta binafsi ndiyo iendeshe biashara. Wao watengeneze sera na mazingira bora ya kufanya biashara

Wawekezaji WAJE WENGI TU, Nyie wezi
Tatizo ni hakuna sheria kali kwamba ukifanya ubadhilifu hakuna kuamishwa ni kuuliwa watu wangenyooka
 
Uwekezaji unaleta Maendeleo sema sisi ndio tunajiibia wenyewe ninakumbukuka Barrick walipoingia walikuwa wakitoa Mishahara minono sana Serikali ikawaambia wapunguze kwasababu Watumishi wa Umma wataacha kazi na kuhamia Migodini.
Serikali inaweza kutumia faida za sehemu nyingine kufix hata mishahara ya walimu.

Mbona pesa za kodi nchi nzima zinajenga kula Dodoma ,ukiacha pesa za Dodoma tu hawatoweza kujenga majengo yale
 
Mtanzania ni bora aone mgeni ananeemeka na anaishi maisha mazuri kuliko kuona mTanzania mwenzie, sijui hii roho mbaya tuliitoa wapi.

Mtu anaona ni bora hata muhindi, muarabu au mzungu anaishi maisha ya kifahari na kufuru lakini kuona mwenzake hata ile ana kula milo mi3 kwa siku, anasomesha watoto shule nzuri, ana biashara zake basi inakuwa ni vita.

Hata serikali ndivyo ilivyo.
 
Tatizo ni hakuna sheria kali kwamba ukifanya ubadhilifu hakuna kuamishwa ni kuuliwa watu wangenyooka
Kwanini uue binadamu aliyeumbwa na Mungu? Huo unyama hauna nafasi kwenye dunia ya kistaarabu. Tanzania imeridhia Universal Human Rights Declaration ya Umoja wa Mataifa (UN), kila binadamu ana haki ya kuishi
 
Wazungu wanadanganya sana wanavyolazimisha mambo yao ya human rights hadi kwa mtu ambaye ni mwizi wazi wazi

Maendeleo sio swala la lelema watu wanaiba mabilion ya fedha za umma maksudi alafu uwachekee ndo maana afrika kuna umaskini wa kutisha

Watu wanaiba wanajua hakuna watakachofanywa
 
Serikali inaweza kutumia faida za sehemu nyingine kufix hata mishahara ya walimu.

Mbona pesa za kodi nchi nzima zinajenga kula Dodoma ,ukiacha pesa za Dodoma tu hawatoweza kujenga majengo yale
Tatizo la Serikali na Chama chake ni kwamba Fedha nyingi zinaibwa na kupigwa kwa mfano Nyumba uliyoijenga wewe Serikali inajenga Nyumba kama hiyo kwa gharama mara Mia moja (100) ya gharama zako UPIGAJI.

Tusingekuwa tunajiibia sisi wenyewe na UPIGAJI Tanzania leo tungekuwa mbali sana sana.
 
Hilo ndio tatizo pesa nyingi zinaenda mifukoni mwa watu wachache.

China wamefika pale kwa vile serikali inamiliki asilimia kubwa ya biashara zote nchini
 
Kipind cha JPM wapinzani walimuashia kunguni eti wanataka wawekezaji 😅😅..Nilikuwa nacheka hizo taasisi walisema JPM alikuwa anapiga pesa huko sasa ngoja waone balaa tena alikuwa Lissu .

Kuna mashirika walitaka yafutwe eti serikali haifanya biashara ...Ndio maana nakuambia wanasiasa hawana wanachojua .
Naunga mkono hoja. Ni kweli ukiona umeshaingiza mambo ya siasa kwenye shughuli za kiuchumi ambazo huwa zina Formula zake ujue kwa uhakika ww kwisha habari yako.
 
Back
Top Bottom