Waziri Mavunde aelezea mafanikio ya sekta ya madini katika miaka mitatu ya Rais Samia

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
-Ukusanyaji wa Maduhuli ya Serikali Katika kipindi cha kuanzia Machi 2021 hadi Februari 2024, Wizara kupitia Tume ya Madini imeendelea kutekeleza jukumu la ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yatokanayo ada za mwaka za leseni, ada za ukaguzi, ada za kijiolojia, mrabaha, fines, penalties and forfeitures na malipo ya huduma za maabara. Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake (Machi, 2021 hadi Februari, 2024) jumla ya Shilingi Trilioni 1.9 zilikusanywa kutokana na vyanzo hivyo.

-Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa umekuwa ukiongezeka hadi kufikia asilimia 9.1 mwaka 2022. Aidha,katika kipindi cha muda mfupi wa kati cha robo ya tatu (Julai – Septemba) ya mwaka 2023 sekta ilichangia asilimia 10.4 ikilinganishwa na mchango wa asilimia 9.5 katika kipindi kama hicho mwaka 2022. Mwenendo huu wa mchango unaakisi dhamira ya Serikali kuhakikisha sekta hii inaimarika na kuweza kuchangia hadi asilimia 10 katika Pato la Taifa ifikapo mwaka 2025 kama ilivyoainishwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025.

-Katika kipindi cha mwezi Machi, 2021 hadi Februari, 2024, Wizara kupitia Tume ya Madini imeendelea kusimamia biashara ya madini katika masoko ya madini hapa nchi ili kuhakikisha yanafanya kazi kwa ufanisi. Katika kipindi rejewa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini zimeendelea kuongezeka ambapo jumla ya Masoko 42 na vituo vya ununuzi wa madini 100 vimeanzishwa nchini.

-Katika kipindi cha mwezi Machi, 2021 hadi Februari, 2024 kiasi cha tani 52.9 za madini ya dhahabu, tani 1,204.83 za madini ya Bati, karati 54,025.89 za madini ya Almasi, karati 183,551.87 na tani 121.34 za madini ya tanzanite na kiasi cha karati 171,286.92 na tani 94,647.94 za madini mengine ya vito yaliuzwa katika masoko ya madini. Mauzo
ya madini hayo yamechangia makusanyo (mrabaha na ada ya ukaguzi) kiasi cha Shilingi bilioni 476.78.

-Kwa kipindi cha miaka mitatu leseni za uchimbaji mkubwa wa madini mkakati zimetolewa ambapo leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini adimu (rare earth elements) imetolewa kwa Kampuni ya Mamba Minerals Corporation Limited (MMCL) katika eneo la Ngualla lilipo Mkoa wa Songwe na leseni ya uchimbaji mkubwa wa
madini ya kinywe imetolewa kwa kampuni ya Faru Graphite Corporation Limited (FGCL)
katika eneo la Mahenge lililopo Mkoa wa Morogoro.

-Leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini ya heavy mineral sands kwa Kampuni ya Nyati Mineral Sands Limited (NYSL) katika eneo la Tajiri, Wilaya ya Pangani,Mkoa wa Tanga inatarajiwa kutolewa wakati mfupi ujao.

-Serikali imeliwezesha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kununua mitambo mitano (5) ya uchorongaji (Rig) kwa ajili ya kuwahudumia wachimbaji wadogo. Mitambo hiyo imesambazwa katika maeneo ya Itumbi (Chunya), Lwamgasa (Geita), Katente (Bukombe), Buhemba (Butiama) na Dodoma.Ifikapo Juni 2024 mitambo yote itafikia idadi ya 15.

-Idadi ya Watanzania walioajiriwa kwenye migodi imeongezeka kutoka 14,308 kati ya waajiriwa wote 14,742 sawa na asilimia 97 kwa mwaka 2021 hadi kufikia ajira 18,580 kati ya 19,165 sawa asilimia 97 hadi kufikia Februari 2024.

-Idadi ya Watanzania wanaotoa huduma na kuuza bidhaa kwa wamiliki wa leseni za madini nchini. Kwa mwaka 2023 jumla ya dola za Marekani Bilioni 1.65 zilitumika kununua bidhaa na huduma kwa Kampuni za madini nchini.

-Manunuzi ya huduma na bidhaa kwa kampuni za Kitanzania yameongezeka kutoka dola za Marekani Milioni 713 ambayo ni sawa na asilimia 82 ya manunuzi yaliyogharimu kiasi cha dola za Marekani Milioni 874 kwa mwaka 2021 hadi kufikia dola za Marekani bilioni 1.43 ambayo ni sawa na asilimia 86 ya kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.65 ya manunuzi yote yaliyofanyika mwaka 2023.

-Kuanza kwa hatua za ujenzi wa Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) wa jengo la ghorofa nane (8) kwa ajili ya shughuli za kituo hicho. Jengo hilo litakuwa na miundombinu ya madarasa, mabweni ya wanafunzi, karakana za uongezaji thamani madini, maabara za madini ya vito, duka la bidhaa za usonara, ofisi na kantini. Lengo ni kujiimarisha katika masuala ya uongezaji thamani madini ya vito na kufanya nchi yetu kuwa kitovu cha shughuli za madini ya vito katika Bara la Afrika.

-Serikali ya Awamu ya Sita imejipanga kufanya utafiti wa kina wa kijiolojia kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kurusha ndege “High Resolution Airborne Geophysical Survey” ili kuboresha taarifa za kijiolojia zilizopo katika vitalu sita (6) vilivyoko katika maeneo mbalimbali ya nchi.

IMG-20240314-WA0023.jpg

IMG-20240314-WA0025.jpg
IMG-20240314-WA0027.jpg
IMG-20240314-WA0024.jpg
IMG-20240314-WA0026.jpg
IMG-20240314-WA0032.jpg
IMG-20240314-WA0030.jpg
IMG-20240314-WA0028.jpg
IMG-20240314-WA0029.jpg
IMG-20240314-WA0031.jpg
 
Back
Top Bottom