chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,003
20,663
Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM kwa sasa inaongozwa na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Majukumu ya Idara hiyo kama yaliyovyoanishwa kwenye Tovuti ya CCM ni pamoja na;
  • Kushughulikia masuala ya msingi ya Itikadi na Sera za Chama Cha Mapinduzi.
  • Kueneza na kufafanua Itikadi na Sera za CCM.
  • Kupanga na kusimamia Mafunzo na Maandalizi ya Makada na Wanachama.
  • Kusimamia Vyombo vya Habari vya Chama, Mawasiliano na Uhamasishaji wa Umma kwa Jumla.
  • Kuongoza na kusimamia maandalizi ya Sera, Programu na Ilani za Uchaguzi za CCM.
  • Kusimamia Utafiti, Maktaba na Nyaraka za Chama
 
CCM kweli ni chama imara na kinachojua propaganda. Leo kimemteua Makonda, hakuna tena cha Waraka wa TEC, wala DP WORLD, wala sijui maandamano ya Mwambukusi, wala Dk. Sla. Kila mtu sasa hivi Makonda na CCM. Kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mkishindwa eti mmeibiwa kura!!!
 
Tokea ameanza kutoa maelekezo yake siku ya kwanza kwa Mawaziri na Jana kwa Mhe. Waziri Mkuu, yeye anelekezwa tu na anaongea kwa mujibu wa chama utamsikia akisema ameagizwa, hivyo hata akiongea kwa namna yotote ile ifahamike kuwa ameongea kwa maelekezo, tusijesema ameanza tena, kwa sasa ipo wazi kuwa ameelekezwa, huo ni mtazamo wangu tu labda kama kuna mtu ana mawazo tofauti
 
Huu ni mtazamo wako tu....!
 
Mkuu, ungeambatanisha na video clip
 
Back
Top Bottom