Mwenezi Makonda ampatia tsh milioni 2 kijana mjasiriamali mwenye kujiendeleza kibiashara

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,399
3,921
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amempatia kijana wa kiume mjasiriamali mwenye ulemavu kiasi cha Tsh Milioni 2 kama sehemu ya kujiendeleza katika biashara yake ya duka la vinywaji.

Mwenezi Makonda amefanya hivyo mara baada ya kusikiliza malalamiko ya kijana huyo anayedai alichukua mkopo wa Halmshauri na kupatiwa fedha Tsh Milioni 2 lakini ndugu yake aliyemtaja kwa jina la Salvata Kalanga kwa kumnunulia bidhaa za vinywaji aina ya maji na soda visivyoendana na thamani ya pesa hiyo na hatimaye kumdhulumu na kumnyanyasa.

Mara baada ya kusikia hayo yote, Mwenezi Makonda aliamua kutoa fedha Tsh Milioni 2 na kumpatia kijana huyo kujiinua tena kwa biashara yake ambapo amesema fedha hizo shukrani iende kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani anayafanya hayo yote kwa kumwakilisha yeye.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Pangani na Waziri wa Maji Ndugu. Aweso aliunga mkono kwa kutoa Tsh Milioni 1 kwa kijana huyo.

#CCMKazini
#VitendoVinaSauti
#TunaendeleaNaMama
#KaziIendelee

PIA, SOMA:
Matamko mengine ya Paul Makonda
 
Akaribie huku kwetu, Kila la kheri kwake.... Lkn Gambo atatuletea urasimu, fitna na majungu alimradi tusipate nafasi ya KUSEMA na Mwenezi wetu
 
Back
Top Bottom