Joseph Haule (Prof. Jay): Sasa nipo Imara, Namshukuru Rais Samia, Mbowe, Watanzania na Familia. See you soon

kyagata

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
6,528
12,622
Huyu jamaa, naona bado hajapona vizuri.

Halafu mbona kakonda sana?

Wazee wa ramli chonganishi, vibuyu vinasemaje huko?

====

Salaam Ndugu zangu,
1683046714591.jpg


Kwanza namshukuru sana Mungu aliye hai kwa uponyaji na kunipa nafasi nyingine ya kuendelea kuwa hai. Hali yangu ilikuwa mbaya isioelezeka, asante sana Mungu baba (nitakutukuza na kukusifu siku zote za maisha yangu).

Pili Kipekee namshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu Dr. Samia Hassan Suluhu na Serikali yake kwa kunigharamia matibabu yangu yote ya Muhimbili na Nje ya Nchi.

Asante sana Mama pamoja na serikali yako yote, kwani viongozi wako wa chama na serikali walikuwa wanapishana kila siku kuja kuniona na kunifariji.

Tatu, namshukuru sana Mwenyekiti wa chama changu cha CHADEMA Kamanda Mbowe, Wanachama na Viongozi wote Waandamizi wa chama kwa jitihada zao za kuhakikisha napata matibabu bora zaidi kwa kushirikiana na serikali.

Zaidi nawashukuru sana Madaktari na Manesi wote wa Muhimbili na kote nilikopitia kwa kunipa matibabu ya kiwango cha juu kwa zaidi ya mwaka mzima niliolala hapo Muhimbili, hasa zile siku 127 za hatari nilizokuwa nimelazwa ICU, mlijitoa kwa uwezo wenu wote kuhakikisha kuwa mnaokoa uhai wangu, ahsanteni sana.

Mwisho na kwa umuhimu mkubwa sana nawashukuru sana Watanzania wote mliojitolea kwa maombi na michango ya fedha zenu kuhakikisha natibiwa na kusema ukweli ilinisaidia sana kulipa bills za awali kabla ya Serikali kuamua kuingilia kati na kuubeba mzigo huu asanteni sana na sitowasahau.

Shukrani sana kwa Malisa GJ na Lyenda kwa kusimamia michango hiyo pamoja na vyombo vyote vya habari na social media nchini vilivyoshirikiana navyo kama Clouds FM, Millard Ayo, Wasafi FM na vyombo vingine mbalimbali pamoja na Watumishi wa Mungu wote walioongoza ibada maalum ya kuniombea, Mungu awabariki sana.

Kuanzia Wachungaji, Mashekh na Mapadre wote wa kanisa langu Katoliki sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea Mungu awabariki sana.

Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipoishukuru familia yangu, mke wangu, kaka zangu, dada zangu, wadogo zangu na familia yote ya Mzee Haule kwa ushirikiano mkubwa na upendo mlionipa.

Kwa sasa nipo imara na ninaendelea vizuri sana, Mungu ni mwema sana siku zote🙏🏻🙏🏻🙏🏻.

Ahsanteni,
Joseph Haule (Prof. Jay)
#MgodiUnaotembea
#SeeYouSoon❤️❤️❤️❤️
 
Huyu jamaa,naona bado hajapona vizuri.
Halafu mbona kakonda sana?
Wazee wa ramli chonganishi,vibuyu vinasemaje huko?

Kukonda ndio ishara ya afya yake kuimarika. The guy was overweight na hiyo linaweza kuwa ilichangia hayo maradhi kumpata. Mungu aendelee kumponya kwani alikuwa artist mzuri sana. Nasikia Samia kafuta bili zote za matibabu yake!
 
Huyu jamaa,naona bado hajapona vizuri.
Halafu mbona kakonda sana?
Wazee wa ramli chonganishi,vibuyu vinasemaje huko?

#SeeYouSoon ❤️❤️❤️❤️

Sipendi kusema watu lakini mdomo wake umelika kwasababu ya pombe. Ujumbe hapa ukifika miaka 40 jitahidi achana na pombe za kuzidi, sukari, vyakula vya wanga, fanya mazoezi na medical check up!. Bila kuelezana ukweli na vitu vilivyo changia tatizo lakini hatuta tenda haki kutoa elimu ya afya. Pole sana Prof Jay
 
Back
Top Bottom