Msaada: Nimetupiwa kipande nateseka mwaka wa 3 sasa, nahitaji msaada

Even MOre

Member
May 6, 2023
54
62


Habari wana jamvi, kama kichwa cha habari kinavyo jieleza ntaomba kuelezea kwa uchache changamoto ninazopitia kwa miaka 3 sasa. Ikibidi nitaandaa treads ya kusimulia mkasa mzima toka ulivyo anza mpaka hali niliyonayo kwa sasa.

Nipende tu kuwaomba wale wenye itikadi za kidini kukaa pembeni kwanza kwani kama hujapitia shida kubwa ktk maisha huwezi kujua kuwa kuna ya walimwengu pia.

Niende kwenye mada, mimi ni kijana wa kiume ambae kazi yangu kubwa ni media producer & fundi wa vifaa vya umeme. Nilihamia wilaya hii iliyoko mkoa x kutoka wilaya nyingine ya mkoa huu huu ili kufata fursa za kibiashara. Mwanzo mambo yalienda vizuri sana na kutokana na kazi yangu iliniwezesha kusafiri mara kwa mara nje na ndani ya mkoa.

Nitafupisha stori, mwanzoni mwa mwaka juzi ndipo nilianza kuona mabadiliko ktk biashara zangu ikawa hata mteja ukimpa bei akaomba punguzo na ukamkubalia ila haitachukua dakika kadhaa kukupigia kuwa ameahirisha kazi hiyo lakini nikifatilia nakuta amefanya kazi sehemu nyingine na haina ubora kama ninavyofanya mimi.

Kifupi niliona ni masuala tu ya kibiashara kufanya au kutokufanya kazi na mteja, lkn hali ikazidi kuwa mbaya kwangu binafsi hata nikienda kazini kwangu ni kulala na hakuna wateja, akienda mwingine kuna nafuu japo hela ya matumizi inapatika. Kiukweli naumia kuona nimewekeza almost vifaa + ofisi zaidi ya 10ml lkn unapata hela ya kula tu hata kodi naelekea kushindwa kilipa.

Kwa muda wote huo mabadiliko yalianza kwangu kuhisi naogopa watu, kujitenga hata sikuwa na ujasili tena ambao nilikuwa nao wa kwenda kwenda kukusanya habari kwenye mikutano, makongamano, sherehe nk kwani watu wamekuwa wakiona kama kitu flani cha ajabu hivi wengine kupelekea kukucheka 😭😭 jambo ambalo limeniathiri sana kisaikolojia, nikiwa na maana kuwa watu wanao cheka ni ambao tunafahamiana nao miaka kadhaa toka nihamie hapa ikiwa kipindi sina tatizo lolote. (Jaribu kuwaza ikiwa wewe ikatokea siku staff wenzo, watu wako wa karibu pengine na familia wanakucheka, kukusengenya na kukudhihaki huku unawaona ni jambo gani utafanya?).

Mpaka sasa nimebaki pekeangu hakuna rafiki wala watu wa dini kuwa karibu tena na mimi, nimebaki na familia yangu hasa mke na watoto ndo wafariji wangu. Na kinachoniumiza zaidi ni mama yangu ambaye kwa sasa anasumbuliwa na pressure iliyotokana na kuniona nikiwa ktk hali hii na jinsi jamii inavyo ni treate kwani mimi ndiye msaada mkubwa kwake.

Kwa muda wote huo nimekuwa nikitafuta suluhiso la tatizo hili, ni nilianzia kwenye maombi miezi kadhaa bila mabadiliko ndipo nikashauriwa kuangalia tiba asili napo nimepita maeneo mengi ya ndani na nje ya mkoa. Kikubwa ambacho nimeambiwa na wengi ni kwamba NIMETUPIWA KIPANDE. Kifupi nimepotea fedha nyingi mpaka sasa na uchumi wangu umeyumba bado sijapata nafuu ya tatizo sababu siwezi kusema kuwa labda wale wataalam wa tiba asili kuwa walikuwa matapeli, hapana sababu kila mtu anao uwezo wake ktk kutatua matatizo ya watu, ndio maana nikaja huku kuomba msaada wa kupata matibabu kwani hali ni mbaya ndugu zangu na familia wananitegemea na sioni nuru mbeleni sababu nimekuwa nikiota ndoto za ajabu ajabu na za kutisha mara nyingi, mara uote unazikwa mara unabeba jeneza nk. 😭.

Japo wengine hufikiria kujiua ili kuondokana na hizi shida za dunia lakini mimi NASEMA KAMA MUNGU ALIRUHUSU MATATIZO HAYA KUNIPATA BASI ASIPORUHUSU KUPATA MSAADA WA KUPONA KABISA BASI NITAISHI HIVIHIVI, SIWEZI KUJIUA.

Naomba nifupishe stori na kuwasilisha kwenu. Kama kuna mtu anaweza nisaidia tiba, namna ya kupona nitashukuru sana.

Mungu awabariki kwa muda wenu.
🙏🏻🙏🏻

Mshana Jr
Hizb Tahrir Tanzania
Hizbu Sharifu
 
Ukiamini hakuna anayeweza Kukuloga Dunia hii jua unamuamini aliyekuumba anayekupa Riziki.

Kuamini kuna anayeweza Kukuloga ndio uchawi mkubwa kuliko. Na hiyo ndio tafsiri ya kukufuru. Kwani unaamini Mungu hawezi kukulinda.

Hakuna atakayekusaidia katika hilo zaidi yako wewe mwenyewe. Imani na badili mindset.
 
Usijione umefanyiwa kitu sijui umetupiwa kitu ndiyo maana mambo yako yanaenda ndivyo sivyo. Kila mmoja wetu hapa kuna vitu au sehemu anatamani kuwa lakini sio kila kitu kwenye maisha utakipata.

Take your time, day by day, punguza matarajio makubwa, jichunguze nyendo zako mwenyewe na uangalie mambo yanayokurudisha nyuma, punguza washauri na binafsi siamini utapata msaada zaidi ya kupata matapeli kwa kukuona wewe fursa kwa sababu uko desperate.
 
Wewe Utapona Kanisani, inabidi urudi Kanisani...!

Ongeza sana Imani yako, isiwe na shaka ndani yake....!

Nakupa Siri ya kupona kwenye maombi...!

Kabla ya maombi, ya Mchungaji yoyote, Amini kuwa umeshapona, Amini kuwa tatizo lako lilikwisha, na sasa ni mtu huru, mwambie Mungu asante .... Hii iwe kabla ya maombi.

Usiende tena kwa Mganga yoyote, Usiende Jumapili Kanisani jumatatu kwa Mganga...!

Katika Jina la Yesu utakua mzima kama zamani, narudia tena...!

Wachawi na Majini huwa wanaogopa sana mtu akiamua ku deal nao kwa njia ya maombi.... Huwa wanaogopa, kwa sababu nnguvu ya Mungu kupitia Mchungaji inapoachiliwa ili ifanye kazi huwa ni over 100%... Thats wy wannaogopa...!

Ila ukienda kwa Mganga tu, Majini na Wachawi hawaogopi tena, sabbabu ni Vita wanavyoweza kupigana, Ni vita ambapo uwezo wa Nguvu unazidiana.

Mwammbie Mungu akusamehe, na umuhaidi hutoenda tena kwa Mganga maisha yako yalobaki, then jenga imani upya, na utashinda.
 
Pole sana ila nahisi ungefunguka zaidi kuhusiana na hiyo kutupiwa kipande maana si kila mtu anajua maana/ugonjwa huo.

Katika swala la maombi, hupaswi kufanya kwa kujaribu bali unapaswa kufanya kwa kuamini kuwa ndio njia pekee. Unaposema ulifanya maombi halafu ukaamua kwenda kutafuta njia mbadala hiyo haikukaa sawa.

Yote kwa yote Mungu akuepa ahueni ya matatizo yako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom