Rais Samia achangia mamillioni ya pesa taasisi ya profesa Jay Foundation, atoa maagizo mazito kwa Wizara ya Afya na Muhimbili

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,272
9,716
Ndugu zangu Watanzania,

Rais Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia,nuru ya wanyonge,nyota ya matumaini,simba wa nyika, komandoo wa vita, mama wa upendo, mzalendo wa kweli,mwamba wa siasa ameendelea kuonyesha moyo wake mkubwa wa upendo na ukarimu kwa watanzania anao waongoza.

Siku ya jana katika uzinduzi wa taasisi ya profesa jay foundation ya msanii na mbunge wa zamani wa jimbo la mikumi Joseph haule maarufu kama profesa Jay, Rais wetu mpendwa aliipatia tabasamu na furaha taasisi hiyo ambayo imelenga kuwasaidia watu wenye matatizo ya figo kwa kuichangia kiasi cha Millioni hamsini.

Lakini pia Rais wetu mama wa huruma ,ukarimu na upendo aliahidi kuwa atagharamia gharama zote za matibabu ya profesa jay ikiwa itatakiwa abadilishiwe figo ambapo gharama yake ni millioni 47.

Pia Rais wetu mpendwa ametoa maagizo mazito sana yanayotakiwa yatekelezwe kama yalivyo kwa wizara ya afya na hospitali ya Muhimbili kuweka utaratibu na mazingira mazuri na wezeshi ya kuendelea kumuhudumia profesa jay kila itakapohitajika kufanya hivyo.

Kwa dhati ya moyo wangu ninampongeza sana Mh Rais wetu kwa upendo wake mkubwa aliouonyesha yeye binafsi na serikali yake tangia awali katika kumpatia matibabu profesa jay ,Ambapo Kama siyo msaada wa serikali yetu ingekuwa changamoto sana kwa profesa jay kumudu gharama za matibabu kwa kipindi chote alichougua.lakini pia nampongeza kwa dhati kabisa profesa jay kwa wazo lake la kuamua kuanzisha taasisi hiyo ambayo italeta tabasamu kwa watu wengi wenye matatizo ya figo.

Mwisho pia napenda nitoe ushauri wangu kwa mama yangu na Rais wangu mh Rais mama Samia Suluhu Hasssan pamoja na serikali yake kuhakikisha kuwa inaendelea kufanyia kazi na kuumiza kichwa juu ya namna ya kufanya katika kupunguza gharama hizo kubwa za matibabu ya figo.kwa sababu kama gharama za kubadilisha figo ni millioni 47 kama ilivyoelezwa.

Naamini kwa mtu anayetokea familia ya kawaida ambazo ndio familia nyingi za kitanzania hawezi kumudu gharama hizo hata kwa nusu yake tu. Na matokeo yake inakuwa ni kupoteza maisha huku ndugu wakiwa kando yake wakibubujikwa na machozi ya huzuni na unyonge kwa kukosa pesa za kugharamia matibabu ya mpendwa wao ambaye pengine angeweza kupona kama wangekuwa na uwezo wa kifedha.

Siyo katika hili la figo tu bali katika yale magonjwa yanayooneka yanatumia gharama kubwa basi serikali yetu Sikivu inaweza kukaa chini kama ilivyo kawaida yake na kuangalia ifanye nini kuhakikisha gharama zinapungua na watu wanapata matibabu bila kujali kipato cha familia wanazotokea,hii itasaidia wagonjwa wengi sana kuwa na matumaini ya kupata huduma.

Naendelea kuipongeza serikali yetu na Rais wetu kwa juhudi kubwa ambazo imekuwa ikifanya katika kuboresha huduma za afya hapa nchini,matibabu ya profesa jay katika hospitali zetu kwa kutumia wataalamu wetu wa afya ni ushuhuda wa ubora wa huduma uliopo na unaotolewa hapa nchini,ni ushahidi wa ubobezi wa wataalamu wetu katika magonjwa mbalimbali ,ambapo hapo zamani tulikuwa tukiwapeleka wagonjwa nje ya nchi ambapo ni wachache kutoka familia za kipato kizuri ndio waliweza kuwa na uwezo wa kupeleka wagonjwa wao nje ya nchi kupata matibabu.

Serikali iendelee na juhudi zake za kuboresha huduma za afya kwa kuhakikisha watalaamu wa afya wanakuwepo kuanzia ngazi ya zahanati mpaka hospitali ya Taifa,kuhakikisha vifaa tiba,madawa na hudumu niyingine zote zinakuwepo na kupatikana katika hospitali za umma,kusudi hospitali hizi ziwe kimbilio la watanzania wasioweza kumudu gharama katika hospitali za binafsi. hongera sana Rais samia kwa kujidhatiti katika kufanya uwekezaji mkubwa kwa wizara ya afya ili kuhakikisha kuwa Watanzania wana kuwa ni wenye afya njema wakati wote na kuendelea na uzalishaji mali, maana huwezi ukafanya kazi kama ni mgonjwa. Afya ndio mtaji namba moja wa kumuinua mnyonge.

Lakini pia watanzania tuendelee kutunza afya zetu kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu na kujiepusha na vitu au mambo yanayoweza kuathiri afya zetu,kinga ni bora kuliko tiba,tujikinge kwa kadiri tuwezavyo kujiepusha na maradhi au magonjwa yanayo epukika kwa kanuni tu za kiafya.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Wengine ambao sio akina Prop Jay ambao ni mamilioni ya watu tunafanyeje, maana umezungumzia Rais kutoa maagizo mazito dhidi ya huduma kwa Prop Jay, maana yake Rais anakubali pale Muhimbili kuna tatizo, sasa hawa watanzania wengine mamilioni ambao kila siku wamejaa pale Muhimbili.
 
wengine ambao sio akina Prop Jay ambao ni mamilioni ya watu tunafanyeje, maana umezungumzia Rais kutoa maagizo mazito dhidi ya huduma kwa Prop Jay, maana yake Rais anakubali pale Muhimbili kuna tatizo, sasa hawa watanzania wengine mamilioni ambao kila siku wamejaa pale Muhimbili.
Nimeshatoa ushauri kwa mh Rais na serikali yake katika andiko langu juu ya nini kifanyike kwa hawa watanzania wengine wasio na uwezo wa kumudu gharama kubwa za matibabu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia,nuru ya wanyonge,nyota ya matumaini,simba wa nyika, komandoo wa vita,mama wa upendo, mzalendo wa kweli,mwamba wa siasa ameendelea kuonyesha moyo wake mkubwa wa upendo na ukarimu kwa watanzania anao waongoza.
Bila shaka anaongoza njia Tumbo lako wewe shetani. Wewe pamoja na mashetani wenzako mungu awachukue haraka.
 
Aisee hapo ulipo toa sifa hizo utafikiri Samia hana dhambi yeyote yani kwakifupi ni kama umesema dhambi zake ubebe wewe! Hivi hizo hela ni zake au za serikali?
😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Kwani million hamsini ni kitu gani kwa kiongozi kama Rais? Yaani wabunge tu wanazo hizo million hamsini ndio Rais asiwe nazo? Hata hivyo kutoa ni moyo na siyo utajili. Kuna wengine wana fedha nyingi lakini huwezi kuwaona wala kuwasikia wakitoa misaada kwa watu wenye uhitaji.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia,nuru ya wanyonge,nyota ya matumaini,simba wa nyika, komandoo wa vita,mama wa upendo, mzalendo wa kweli,mwamba wa

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Mkuu unapamba sana mpaka unaharibu na kuboa sasa...
Unakuta wewe unafamilia kabisa mke na watoto
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia,nuru ya wanyonge,nyota ya matumaini,simba wa nyika, komandoo wa vita,mama wa upendo, mzalendo wa kweli,mwamba wa siasa ameendelea kuonyesha moyo wake mkubwa wa upendo na ukarimu kwa watanzania anao waongoza.

0742-676627.

Duhhh!!! Imebidi nicheke tu!

Huu upuuzi mimi nikiwa rais ukanisifia hivi lazima wakuokote coco beach


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom