CCM Moshi Manispaa acheni uonevu

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,828
21,461
Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!!!!!

Napenda kuchukua fursa hii kwa furaha kubwa kuwaaga wana Moshi na viunga vyake niwashukuru sana kwa muda wa miezi mitatu kasoro niliofanya kazi moshi mmenipatia ushirikiano wa dhati katika utendaji wangu.

Najua kwa namna moja ama nyingine katika kutekeleza majukumu yangu ya kikanuni inawezekana wapo ambao nimewakwaza,au nimewaumiza ,mimi ni binadamu naombeni mnisamehe sana ndugu zangu haikuwa maksudi bali ni katika kutimiza wajibu wangu wa kila siku.

Namshukuru sana Mungu aliyenipa kibali ya kuwatumikia wa moshi kwa kipindi kifupi sana ni historia kubwa ndani ya utumishi wangu.

Nawakaribisha sana wilaya ya Iramba mkoa wa Singida Tanzania,daima nitaendelea kuamini katika uzalendo wa kweli,haki,usawa, uadilifu uliotukuka kwa chama changu na jumuiya yangu ya uwt wilaya

Nitakuwa mkweli daima fitina kwangu mwiko,Nikiwa na imani kubwa sana kwamba Mungu ndie anayepanga kila kitu na hakuna mkubwa zaidi ya Mungu na daima nitaendelea kumshukuru yeye kwa kila hatua ninayoipitia.

Niwashukuru sana viongozi na wanachama wote ,kwa moyo wa dhati nimshukuru sana Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la moshi mjini Priscuss Tarimo kwa ushirikiano wake wa dhati kwenye jumuiya yetu pindi nikiwa katibu hapa,naomba uendelee hivo hivo usiwaache wanawake wao bila wewe hawataweza na wewe bila wao hautaweza.

Nimshukuru sana mwenekiti wa ccm wilaya ya moshi mjini Comred Faraji Swai,kwa kuwa Bega kwa Bega na jumuiya ya uwt pamoja na kutushauri kila wakati ili jumuiya hii iendelee kuwa imara zaidi.

Namshukuru sana katibu wa ccm wilaya Comred Fridah Kaaya na makatibu wenzangu wa jumuiya ya uvccm na wazazi kwa kushirikiana kwa pamoja ili jumuiya zetu ziendelee kustawi.

Niwashukuru sana waheshimiwa madiwani wa ccm kata zote,madiwani wa viti maalum,wenyeviti wote wa ccm kata na jumuiya ,makatibu wote wa chama na jumuiya kwa pamoja,wanawake wote na makada mbalimbali wa ccm nawashukuru sana.

Namshukuru sana Mheshimiwa Mkuu wetu wa wilaya jembe letu kamisaa wa chama Cha Mapinduzi,kwa kuendelea kuilea jumuiya yetu ya uwt kindakindaki ,kwa afya ya chama cha Mapinduzi.

Nawashukuru sana viongozi wetu wa chama cha Mapinduzi mkoa wa kilimanja na Jumuiya zake kwa pamoja nasema ahsanteni sana kwa upendo wa dhati juu ya jumuiya yetu pendwa ya uwt .

Nasema kuwa nawapenda sana na nitaendelea kuwapenda mimi ni mzawa wa kaskazini kwa hiyo tutaendelea kuwa wote katika mambo mengine ya kijamii.Mungu wa Neema awabariki sana sana na awajalie afya njema.

👏👏👏👏😘😘🙇‍♀️
 
Kwahiyo unawaaga wana Moshi au wana UWT🤔.Kwani wanasema waarabu hujuana kwa vilemba vyao🏃🏃😂😂.
 
Mbona “heading” ni kuhusu uonevu halafu “content” ni kitu kingine kabisa?
 
Mbona “heading” ni kuhusu uonevu halafu “content” ni kitu kingine kabisa?
Huyu karibu wa UWT wa huko moshi Mjini, atafutwe na kuhojiwa anayo Siri kubwa sana kuhusu ufisadi ndani ya miradi ya UWTndani ya ccm.

Ametolewa kafara na katibu wa ccm mkoa na Uwt mkoa.

Wizi ni mkubwa na unabarikiwa na vigogo wa ccm ndani ya ccm.
 

Attachments

  • 5D9F62F2-386C-4E7E-B4DB-38EC94593F9F.jpeg
    5D9F62F2-386C-4E7E-B4DB-38EC94593F9F.jpeg
    71.6 KB · Views: 2
Huyu karibu wa UWT wa huko moshi Mjini, atafutwe na kuhojiwa anayo Siri kubwa sana kuhusu ufisadi ndani ya miradi ya UWTndani ya ccm.

Ametolewa kafara na katibu wa ccm mkoa na Uwt mkoa.

Wizi ni mkubwa na unabarikiwa na vigogo wa ccm ndani ya ccm.
Ok, Sasa issue hapo ni wizi na ufisadi wa ccm unaosimamiwa na katibu wa ccm.

Hapo ni pesa za chama.

Moshi kwa kawaida ccm haichaguliwi. Ni Maghufuli aliyelazimisha ushindi uende ccm iwe iweje.
 
Back
Top Bottom