Pole kwa kuchelewesha kuchangia
Super Villain, Pamoja nipo nje ya muda kwenye huu uzi wetu ila nitajibu, nilipitiwa pasipo kuona hii hoja hapa nimepitia nikaiona,
Ni hivi nikupe sifa kwanza za wanadamu, sifa kuu ya mwanadamu hupendelea sana apewe attention mfano akiumwa umpe muda wako wa kutosha hata kama upo busy kiasi gani, hupendelea sana kuona anajaliwa kumpa pole pindi anapitia magumu, huependelea sana kuona anathaminiwa mfano zawadi..sasa tuongele zawadi, moja ya vitu mwanadamu yoyote ukifanya hufurahia ni pale unapompa zawadi ukiwa nazo kubwa mfano gari, nyumba unampa tu, ila zawadi ndogo ndogo huwa naona zina count sana mfano pipi, biscuti, keki, drinks, chocolate, nguo, raba, simu nk hivyo ni vitu vidogo sana lakini vina count sana kwa mtu unaempatia,
sasa ukirudi kwenye swali lako kumnunulia mpenzi wako PED ni kitu kizuri humjengea furaha sana kwanza anaamini sio rahisi kwa mwanaume ukaenda dukani ukaulizia ped, so kwa mtu unaempatia anathamini sana hilo, hata chupi ukipata nafasi unamnunulia tu mwenza wako, huwa ni jambo ambalo wanalipenda sana wakina dada, so jaribu utanipa mrejesho, huwa linatia faraja sana,