Isabella Mwampamba, mgonjwa wa kwanza kugundulika Corona Tanzania aomba msamaha kwa Watanzania

Maboso,
Tusimhukumu sana Isabella .
 

Attachments

  • Screenshot_20200318-124923_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20200318-124923_WhatsApp.jpg
    55.4 KB · Views: 4
Unajau nchi nyingi za Ulaya zinaruhusu abiria (on transit passengers) kuendelea na safari. Tatito liko hapa kwetu, ilitakiwa kila abiria anayeingia nchini kutoka mataifa yenye visa vya COVID 19, wawekwe chini y uangalizi iwe amepatwa na COVID 19 au bado lakini iwe ni lazima kuwekwa chini ya ungalizi kwa muda huo wa siku 14
 
Isabella Mwampamba, Mtanzania wa kwanza kugundulika kuwa na Virusi vya Corona hapa nchini, leo amezungumza na Watanzania kwa njia simu kupitia Mkutano wa Waandishi wa habari, na kuwaomba radhi Watanzania kwa kuwa Mtu wa kwanza kuingia na Virusi hivyo hapa nchini.


Anaomba msamaha kwa lipi?
 
Ili kupunguza panic kwa wananchi na kuondoa ile hofu napendekeza serikali kupitia wizara ya afya, mbali na watu kukumbusha njia mbalimbali za kujikinga na maambukizi ya virus vya Corona pia iwe inatoa updates za mara kwa mara za hali ya yule mama mgonjwa wa kwanza. Inawezekana huu ugonjwa ukawa sio tishio sana kwa rangi nyeusi kama inavyotangazwa ni vile tu haijathibitika, lakini,

Yule mama awe ndio dirisha letu la matazamio, kwa maana kila mmoja na afya yake lakini nadhani wengi wetu tunamsikilizia zaidi huyo mama.
Kwa kuamini survival yake ndio itakuwa ya waTz wote, akitoboa yeye basi tumetoboa wote na ni jambo la kheri kusikia anaendelea vizuri.



.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ondoa hofu mkuu ugonjwa huu utapita jilinde kama inavyostahiri
 
Maboso,

Hivi huyu mgonjwa si alijua kwamba ameshirikiana na watu wenye corona na bado akapanda ndege kuja nchini? Je dhana sio kwamba alitaka kuja kuugulia nchini ili kama mauti yakimpata awe Tanzania? Kwa namna hiyo sio kwamba alifanya makusudi kutuletea coronavirus?

Akitoka tu hospitali napendekeza awekwe mahabusu kujibu mashitaka ya kutuletea corona makusudi
 
Back
Top Bottom