MOI watoa tamko kuhusu uvunjifu wa maadali uliofanywa wodini. Mgonjwa aomba radhi

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Menejimenti ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imetoa ufafanuzi kuhusu uvunjifu wa maadili uliofanywa na Mgonjwa (jina limehifadhiwa) na anayedaiwa kuwa Mpenzi wake (jina limehifadhiwa) ndani ya wodi (3A) siku ya Jumapili mchana tarehe 9/07/2023 ambapo katika uchunguzi wa awali mgonjwa amekiri kufanya tendo la busu la midomo na ndimi na Mpenzi wake katika mazingira ya kuumwa ndani ya Hospitali kitu ambacho ni kinyume cha maadili ya kitanzania.

“Menejimenti imebaini kwamba Mpenzi wa Mgonjwa huyo si Mtumishi wa Taasisi ya MOl, aidha tukio hilo liligunduliwa na Muuguzi aliyekuwepo wodini ambapo alichukua hatua ya kuzuia Wahusika kuendelea na kitendo hicho, Menejimenti inaendelea kuchukua hatua zaidi kwa Wahusika”

“Uchunguzi zaidi umebaini pia wakati vitendo vinaendelea kuna Mgonjwa jirani (jina linahifadhiwa) ambaye alisharekodi video, Menejimenti ya MOl inalaani kitendo hicho cha uvunjifu wa maadili kilichofanywa na Mgonjwa huyo pamoja na Mpenzi wake, vilevile Menejimenti inalaani na kukemea kitendo cha kurekodi video wodini na kutuma kwenye mitandao ya kijamii kilichofanywa na Mgonjwa jirani”

“Matukio haya yote ni kinyume na mwongozo wa Wizara ya Afya unaozuia kufanya matendo ya uvunjifu wa maadili kwa mgonjwa na kurekodi video wodini, Menejimenti inaendelea kuchunguza zaidi tukio hili ili kujiridhisha kuwa hapakuwa na uzembe katika kusimamia usalama wa Wagonjwa wakati Ndugu wanawatembelea Wagonjwa wodini”

1689020614486.png

Baada ya Tamko hili Mgonjwa aomba radhi
MGONJWA aliyelazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) ambaye video yake imesambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha akibusu midomo na ndimi na mpenzi wake wodini ameomba radhi kwa kitendo hicho na kuahidi hatorudia tena.

Taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa Moi, Patrick Mvungi inasema kuwa kitendo hicho kimefanyika katika Wodi 3A siku ya Jumapili mchana Julai 9, 2023.

Aidha, amesema katika uchunguzi wa awali mgonjwa amekiri kufanya tendo la busu la midomo na ndimi na mpenzi wake katika mazingira ya kuumwa ndani ya Hospitali kitu ambacho ni kinyume na maadili ya Tanzania.

“Menejimenti imebaini kwamba mpenzi wa mgonjwa huyo si mtumishi wa Moi.”Amesema

Amesema, tukio hilo liligunduliwa na muunguzi aliyekuwepo wodini ambapo alichukua hatua ya kuzuia wahusika kuendelea na kitendo hicho na menejimenti inaendelea kuchukua hatua zaidi kwa wahusika.

 
Huu ni ujinga wa hali ya juu. Wanaobusiana ni wapenzi sasa shida ipo wapi kubusu? Mie nilidhani walikulana wodini!! Halafu what if ilikuwa anamtia moyo mgonjwa kwa kumpa mabusu motomoto?

Aliyerekedi ashughulikiwe sababu amevunja faragha ya watu ya kiss.sidhani kiss ni kosa kwakweli. Huyo aruhusiwe.
 
Menejimenti ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu uvunjifu wa maadili uliyofanywa na mgonwa (jina limehifadhiwa) na anayedaiwa kuwa mpenzi wake (jina limehifadhiwa) ndani ya wodi (3A) siku ya Jumapili mchana tarehe 9/07/2023.

Katika uchunguzi wa awali mgoniwa amekiri kufanya tendo la busu la midomo na ndimi na mpenzi wake katika mazingira ya kuumwa ndani ya Hospitali kitu ambacho ni kinyume cha maadili ya kitanzania.

Pia, Menejimenti imebaini kwamba mpenzi wa mgonjwa huyo si mtumishi wa Taasisi ya MOl. Aidha, tukio hilo liligunduliwa na Muuguzi aliyekuwepo wodini ambapo alichukua hatua ya kuzuia wahusika kuendelea na kitendo hicho na Menejiment inaendelea kuchukua hatua zaidi kwa wahusika. Uchunguzi zaidi umebaini pia wakati vitendo vinaendelea kuna mgonjwa jirani (jina linahifadhiwa) ambaye alisharekodi video.

Menejimenti ya MOl inalaani kitendo hicho cha uvunjifu wa maadili kilichofanywa na mgonjwa huyo pamoja na mpenzi wake. Vilevile Menejimenti inalaani na kukemea kitendo cha kurekodi video wodini a kutuma kwenye mitandao ya kijamii kilichofanywa na mgonjwa jirani. Matukio haya yote ni kinyume na mwongozo wa Wizara ya Afya unao zuia kufanya matendo ya uvunjifu wa maadili kwa mgonjwa na kurekodi video wodini.

Menejimenti inaendelea kuchunguza zaidi tukio hili ili kujiridhisha kuwa hapakuwa na uzembe katika kusimamia usalama wa wagonjwa wakati ndugu wanawatembelea wagonjwa wodini.

Taasisi ya MOl inaendelea kuwakumbusha wagonjwa pamoja na ndugu wa wagonjwa kuheshimu miongozo ya Wizara ya Afya kwa kutofanya vitendo vyenye uvunjifu wa maadili au kupiga picha/video katika maeneo ya kutolea huduma za atya.
 
Back
Top Bottom