India yatoa msamaha wa kulipa faini kwa Watanzania waliokwama kurudi nyumbani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989


Balozi wa Tanzania Nchini India, Anisa Mbega ametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu msamaha uliotolewa kwa Watanzania baada ya mazungumzo maalum yaliyofanyika pamoja na Serikali ya India kwa kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ya India.

Balozi Mbega anasema “Ubalozi kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali ya India umekubaliwa msamaha wa kutolipia faini ya kuondoka Nchini India maarufu kwa jina la Exit Permit kwa Watanzania waliopitisha muda wao wa ukaazi Nchini India.

“Faini hiyo huwa inatozwa kwa Wageni wote waliopitisha muda wa ukaazi kinyume na taratibu za Uhamiaji, kuna Watanzania wengi walioshindwa kulipa faini hiyo kutokana na kutokuwa na fedha.

“Hali hiyo imesababisha waishi katika mazingira magumu, ambapo Ubalozi wa Tanzania Nchini India ukaamua kufanya juhudi ili kuwawezesha Watanzania warejee nyumbani kwa njia hiyo ya msamaha.

“Nawasii Watanzania wajitokezi kwa wingi kwa kuwa msamaha huo ni wa muda maalum kuanzia Mei 2023 hadi Oktoba 31, 2023 na utawagusa zaidi Watanzania ambao wamefika Nchini kwa shughuli zisizo rasmi pamoja na Wanafunzi.

"Wanaokabiliwa na kesi mbalimbali hawatahusika na msamaha huo hadi hapo utaratibu wao wa kisheria utakapoamilika.

“Wahusika wote wanaoangukia katika msamaha huo wanatakiwa kufuata taratibu kwa kutuma maombi yao kwa njia ya ‘online’ katika mtandao wa Uhamiaji wa India na kukamilisha taratibu zote kama inavyotakiwa.

“Wakifika hatua ya kulipa watatakiwa kukiri kushindwa kulipa fedha hizo kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha, baada ya hapo wawasilishe kwetu vielelezo vyote Ubalozini ili taratibu nyingine ziendelee.

“Taratibu za kukamilisha mchakato zitachukua wiki tatu hadi nne na wanufaika watatakiwa kujigharamia kulipa tiketi za ndege kwa ajili ya kurejea Tanzania.

“Watanzania wanaoishi India wanatakiwa kuheshimu na kufuata taratibu husika.

“Niwaombe watakaofanikiwa kurejea nyumbani hasa dada zetu mkawe mabalozi wazuri, mkawaeleze wale wenye ndoto za kuja India kwa njia ambazo mlipitia ninyi, muwaelezee changamoto mlizokutana nazo ili nao wasije wakaingia katika madhira ambayo mmekumbana nayo.”
 
Naona serikali inajigamba. Wale vijana ni wengi sana. Itaweza kuwalipia nauli wote?
Nakumbuka Mumbai, wahamiaji haramu, tulitukuwa tunalala kwenye pavement. Wale vijana wengi ni drug addicts. Nikakamatwa nikawa deported. Ama sivyo ningekuwa India mpaka leo.

Wale watu hawana passport. Ukisikia wahuni, ndio wao wale. Ndio ilikuwa maisha yetu pale: hatuna visa na, in fact, hatuna passport.
 
Naona serikali inajigamba. Wale vijana ni wengi sana. Itaweza kuwalipia nauli wote?
Nakumbuka Mumbai, wahamiaji haramu, tulitukuwa tunalala kwenye pavement. Wale vijana wengi ni drug addicts. Nikakamatwa nikawa deported. Ama sivyo ningekuwa India mpaka leo.

Wale watu hawana passport. Ukisikia wahuni, ndio wao wale. Ndio ilikuwa maisha yetu pale: hatuna visa na, in fact, hatuna passport.
Hatuna muda, tunatoa ndege kupeleka yanga fainali kwanza. Kila kitu ni priority
 
Back
Top Bottom