Isabella Mwampamba, mgonjwa wa kwanza kugundulika Corona Tanzania aomba msamaha kwa Watanzania

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,014
2,000
Isabella Mwampamba, Mtanzania wa kwanza kugundulika kuwa na Virusi vya Corona hapa nchini, leo amezungumza na Watanzania kwa njia ya simu kupitia Mkutano wa Waandishi wa habari, na kuwaomba radhi Watanzania kwa kuwa Mtu wa kwanza kuingia na Virusi hivyo hapa nchini.

 

malisoka

JF-Expert Member
Jul 8, 2012
1,863
2,000
Tumemsikia Waziri Ummy Mwalimu akiwasiliana na mgonjwa wa kwanza wa virusi vya corona akiwa Arusha leo.

Hapa maadili na sheria za kitabibu zinaruhusu haya.

Au amefanya hivyo kama kutapatapa kwa branda alizozifanya mpaka leo mamilioni ya wanafunzi na watoto wetu wanahangaika.

Pia naona ni kama kuhatarisha maisha ya huyu mgonjwa . hatuoni kwamba watu wanaweza kumfikiria vibaya, kwa maneno na hata kwa vitendo?

Nina wasiwasi sana na kwamba huyu mgonjwa kama hata pata shida ya kisaikolojia kwa lawama na manung'uniko kutoka kwa watu.


Nasema hivyo kwa maana tumeishaona post nyingi zikianza polepole kuattack personality ya huyu mgonjwa wa Arusha.

Mgonjwa na ugonjwa anaougua ni sir ya mgonjwa na daktari wake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom