Heri ya kuzaliwa kwako Mh. Tundu Antipas Lissu.
(Kawimbo) Happy Birthday to youuu, Happy Birthday to youuu Happy Birthday Deat Lissuuu, Happy Birthday to youuuuuuuuuu!
Unapoanza mwaka wako wa 54 Mwenyezi Mungu akujalie afya njema na maisha marefu.
You are the HERO!
Ule mkono wa Mungu uliokuepusha na risasi 38 ukakulinde siku zako zote Mungu alizokupangia kuishi hapa duniani. Lile kusudi la Mungu alilolikusudia la kuwepo kwako chini ya jua ndani ya nchi hii LIKATIMIE.
Umekuwa Mwalimu wa maarifa katika maeneo mbalimbali yahusuyo nchi yetu., kwa huku mitandaoni tunakushukuru sana kuwa niaba ya watumiaji wa Twitter, Club House na Space.
Na umefanya hivyo bila kuchoka. Unastahili hizo Phd ambazo tunaona zinaenda kwa kina Msukuma (Mbunge). Ulistahili kuwa Dr. Lissu au Prof. Lissu, kwa elimu unayotoa ambayo inatufumbua macho na kutunoa ubongo.
Mungu akubariki Mh. TUNDU LISSU!