Baraka Mina
JF-Expert Member
- Sep 3, 2020
- 581
- 574
Mnamo tarehe 27 Januari 1960 Rais wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Ndg. Samia Suluhu Hassan alizaliwa huko Makundichi Zanzibar.
Leo anatimiza umri wa miaka 62. Ni Rais wa kwanza mwanamke nchini kwetu na mfano wa kuigwa kwa wasichana, wanawake na watu wa rika na jinsia mbalimbali kwa namna moja ama nyingine.
Tunaamini kuwa leo asubuhi 27 Januari 2022 Saa 12:00 Asubuhi - 03:00 Asubuhi kupitia mahojiano maalum katika kipindi cha Jambo Tanzania katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) utakuwa na mengi ya kutueleza yakuhusuyo wewe, maendeleo endelevu ya nchi yetu na mustakabali bora wa nchi yetu pendwa ya Tanzania.
Tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu awe nawe katika uongozi wa awamu ya sita, akujalie afya njema, furaha, maisha marefu na nguvu za kuwatumikia watanzania bila kuchoka wala kukatishwa tamaa katika kuhakikisha taifa hili linapata maendeleo.
Heri ya Kumbukumbu ya Siku ya Kuzaliwa Rais wetu na daima Kazi Iendelee.