Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la Bunge la 12 Mkutano wa 11, Kikao cha 25 leo Mei 15, 2023.



WAZIRI MASAUNI: SERIKALI HAIJAJIRIDHISHA URAIA PACHA NI MATAKWA YA WENGI
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema “Bado Serikali haijajiridhisha kwamba uraia pacha ni takwa la Wananchi wengi, ndio maana hata katika mchakato wa katiba uliokwama hakukuwa na pendekezo, Serikali ipo katika hatua za mwisho kuanzisha utaratibu wa Hadhi Maalum kwa Watanzania waliochukua uraia wa Nchi nyingine.”

Awali, Mbunge Agnesta Lambert Kaiza alihoji kama Serikali haioni haja ya kuwasilisha Muswada wa marekebisho wa uraia Pacha akieleza kuwa kuwakana Watanzania wanaochukua uraia wa Nchi nyingine ni sehemu ya ubaguzi.

MWONGOZO KUHUSU MGOMO SOKO KUU LA KARIAKOO
Mbunge wa Makete Festo Sanga ameomba mwongozo wa Spika kuhusu mgomo unaoendelea kwenye soko la kariakoo ukihusishwa na kamata kamata pamoja na changamoto zingine za ukusanyaji wa mapato.

IMG-20210623-WA0103.jpg

Festo Sanga, Mbunge wa Makete
Sanga amesema kuendelea kwa mgomo huu kunakosesha taifa mapato, pia mikoa inatikisika kwa kuwa wafanyabiashara wengi nchini huchukua biadhaa hapo.

Akitolea maelezo ya kinachoendelea kariakoo muda huu, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema "Kumekuwa na majadiliano ambayo yanaendelea kati ya Serikali na wafanyabiashara wetu ambao wapo kariakoo, kuhusu hoja zao mbalimbali ambazo wanatamani Serikali izifanyie kazi na mpaka sasa hivi tunapoongea Mhe. Spika, Mhe. Mkuu wa Mkoa pamoja na wataalamu wetu kutoka wizara ya fedha, wizara ya viwanda na biashara wapo kwenye kikao na uongozi wa wafanyabiashara wa kariakoo"


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji
Ameongeza, "Na yapo baadhi ya maeneno ndani ya Kariakoo ambayo shughuli zinaendelea na wengine kama ilivyo uhuru wa kila mtu kufanya kile anachokiona, anatakiwa kukifanya, wengine wamefunga maduka yao wengine maduka yanafanya kazi"

Kwa mujibu wa Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Bunge halitajadili hoja hii kwa sasa hadi pale atakapojiridhisha kuwa madai ya Mbunge Festo Sanga yana ukweli, pia kwa kuwa jambo hilo linafanyiwa kazi na Mkuu wa Mkoa.

Katika Mwendelezo wa Sakata hili, Mbunge Hawa Mwaifunga amesimama kuomba pia mwongozo ambapo amesema Wafanyabiashara wamegoma kufungua maduka yao hadi siku ya Alhamisi watakapopatiwa majibu ya malalamiko yao.

maxresdefault (1).jpg

Hawa Mwaifunga, Mbunge wa viti maalumu
Amedai pia kauli ya Waziri wa Viwanda kuwa baadhi ya maduka yamefunguliwa sio ya kweli kwa kuwa hakuna duka lolote lililofunguliwa, na kuna onyo kwa wafanyabiashara yeyote atakayefungua biashara ni halali ya wengine.

Waziri Dkt. Ashatu Kijaji amesisitiza kuwa "Wapo wafanyabiashara waliotumia uhuru wao kufungua maduka na wapo waliotumia uhuru wao kufunga maduka, ni demokrasia, hakuna mtu anayelazimishwa kufanya jambo"

Amesema kwa sasa Serikali bado ipo kwenye mazungumzo na wafanyabiashara na ikitokea kuna maelezo mengine atayatoa.

SPIKA ASITISHA BUNGE BAADA YA HITILAFU YA UMEME
Shughuli za Bunge Jijini Dodoma zimesitishwa kwa muda hadi saa kumi jioni kutokana na hitililafu ya umeme ndani ya Bunge

Spika Dkt. Tulia Ackson amelazimika kusikitisha shughuli hizo saa nne asubuhi ya leo Jumatatu Mei 15, 2023
 
Haya

Ngoja tuone kama wamevaa barakoa ama la!

Hata wakati Ule angalizo lilitolewa na mbunge wa Kinondoni
 
Mbunge wa Makete Mhe. Sanga ameomba Bunge lijadili kwa dharura mgomo wa Kariakoo.

Spika amemuuliza Waziri wa Biashara ambaye amejibu hakuna mgomo ila Wafanyabiashara wametumia uhuru wao wa kufunga au kufungua.

Festo Sanga amesema anazo taarifa kamili kwa sababu 50% ya Wafanyabiashara wa Kariakoo wanatoka Makete.
 
Hoja ya mbunge wa makete Deo Sanga kuwa bunge lisitishe shughuli zake za kila siku na kujadili kero ya kariakoo imekataliwa na spika.

Waziri wa viwanda na biashara Dkt. Ashantu Kijaji amesema mambo sio mabaya maana shughuli za soko zipo under control chini ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

Hoja wa Waziri anasema ni haki kwa kila mtu kufanya biashara au kutofanya pia asema wapo walioruhusiwa na waliokataa.

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ndio serikali ya CCM na mambo yake, Waziri anasema hakuna mgomo kwasababu hayo mduka ni ya watu binafsi?

Sasa inakuwaje hata kama yakiwa ya watu binafsi, leo siku ya kazi halafu maduka mengi yafungwe kwa wakati mmoja? kama sio mgomo ni kitu gani?

Mwambie Waziri aende field kujionea uhalisia na kuambiwa ukweli, asiendeleze tabia yao kutoa majibu mepesi bungeni kwa maswali mazito wanayoulizwa ilimradi siku ziende.
 
Back
Top Bottom