Waziri Ashatu Kijaji: Limeni Miwa kwa Wingi Soko la Miwa Limekuwa Kubwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

WAZIRI DKT. ASHATU KIJAJI - LIMENI MIWA KWA WINGI, SOKO LA MIWA LIMEKUWA KUBWA

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amewataka wakulima wa miwa kuendelea kulima miwa kwa wingi kwani soko la miwa limekuwa kubwa kutokana na ongezeko la viwanda vya sukari nchini.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Agosti 10, 2023 alipotembelea kiwanda cha Sukari cha Kilombero kilichopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kujionea maendeleo ya uzalishaji wa Sukari Pamoja na upanuzi wa Kiwanda hicho.

Dkt. Kijaji amesema kuwa lengo la Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Miwa inayolimwa na wakulima wadogo wa maeneo ya jirani na kiwanda iweze kununuliwa yote na kuchakatwa kwani soko la miwa lipo na linaendelea kukua kila siku kutoka Tani la nane na kuongezeka kwa Tani laki tisa nyingine ndani ya Kiwanda cha Kilombero.

Aidha ameongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara inaendelea kufanya kazi nzuri ya kusimamia Mpango wa uboreshaji wa Mazingira bora ya Uwekezaji na Ufanyaji Biashara Nchini unaofahamika kama MKUMBI hali inayofanya kuwepo kwa wawekezaji wengi wa viwanda ndani ya Tanzania.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima amempongeza Dkt.Kijaji kwa ziara yake hiyo katika Kiwanda hicho Pamoja na Kusimamia vyema masuala ya viwanda na biashara hali iliyopelekea uongozi kupanua kiwanda hicho kwa kuwekeza tena zaidi ya fedha za Kitanzania Bilioni 600 ili kuongeza uzalishaji wa sukari chini.

Vilevile kwa niaba ya Mkurugenzi wa Biashara wa kiwanda hicho amesema kuwa kiwanda kinatekeleza kwa vitendo na kuunga mkono dhamira ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia juu ya Uwekezaji na biashara nchini ambapo kiwanda kimeamua kufanya upanuzi wa Kiwanda hicho kinachofahamika kama K4 kitakachozalisha Sukari kwa Kiwango cha Kisasa.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.12.26.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.12.26.jpeg
    37.2 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.12.27.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.12.27.jpeg
    68.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.12.28.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.12.28.jpeg
    39.3 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.12.28(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.12.28(1).jpeg
    39.8 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.12.28(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.12.28(2).jpeg
    38.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.12.29.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.12.29.jpeg
    47.7 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.12.29(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.12.29(1).jpeg
    39.9 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.12.29(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.12.29(2).jpeg
    34 KB · Views: 3
Back
Top Bottom