Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,900
- 944
WAZIRI ASHATU KIJAJI AAHIDI KUTATUA KERO YA UTOZAJI USHURU KWA WAFANYABIASHARA WADOGO MKOA WA MANYARA
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amewaahidi wafanyabiashara wa soko la Mchele la Magugu mkoani Manyara kufanyia kazi kero ya utozaji wa ushuru wa Shilingi 1500 kwa mfuko wa ujazo wa kilo 50 na kwa kushirikiana na Waziri wa Kilimo pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi.
Waziri Kijaji ametoa ahadi hiyo Mei 12, 2023 alipotembelea soko la Mchele la Magugu mkoani Manyara na kukutana na Wafanyabiashara kwa lengo la kujionea hali ya biashara katika soko hilo wakati wa mwanzo wa msimu wa mavuno ya Mpunga kwa mwaka 2023.
Wakiongea na Waziri Kijaji, Wafanyabiashara wa Magugu wameipongeza Serikali kwa kusaidia kuboresha mazingira ya Wafabyabiashara wadogo na wameiomba Serikali iwapunguzie tozo ya ushuru wa Shilingi 1500 kwa mfuko wa ujazo wa kilo 50 kwa kuwa inaongeza gharama katika biashara.
Aidha, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameshiriki Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika tarehe 12/5/2023 jijini Arusha. Mkutano huo pamoja na mambo mengine umejadili masuala ya kibajeti ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Attachments
-
WhatsApp Image 2023-05-14 at 11.37.28(1).jpeg54.2 KB · Views: 8
-
WhatsApp Image 2023-05-14 at 11.37.28.jpeg41.5 KB · Views: 6
-
WhatsApp Image 2023-05-14 at 11.37.27(2).jpeg40.2 KB · Views: 4
-
WhatsApp Image 2023-05-14 at 11.37.26(2).jpeg52.1 KB · Views: 5
-
WhatsApp Image 2023-05-14 at 11.37.27.jpeg39 KB · Views: 5