Waziri Dkt. Ashatu Kijaji Akitaka Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) Kusimamia Mikataba ya Wawekezaji

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
942

WAZIRI DKT. ASHATU KIJAJI AKITAKA KITUO CHA UWEKEZAJI (TIC) KUSIMAMIA MIKATABA YA WAWEKEZAJI

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akitaka Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kusimamia mikataba ya wawekezaji mahiri na wa kimkakati ili kujenga uchumi imara wa nchi yetu kupitia viwanda.

Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ameyasema hayo tarehe 23 Julai, 2023 katika kikao cha utiaji saini mikataba ya utekelezaji na wawekezaji wa kimkakati uliofanyika katika ukumbi wa TIC jijini Dar es salaam.

Dkt. Kijaji amewapongeza wawekezaji hao kwa kazi wanayofanya ya kuwekeza nchini kwani serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka msukumo katika sekta binafsi kuwa kiongozi katika kukuza uchumi wa nchi yetu.

Katibu Mkuu ofisi ya rais Uwekezaji Dkt. Tausi Kida amesema kuwa kupitia uwekezaji wa kimkakati unaofanywa na wawekezaji mahiri ambao wamewekeza Dola za kimarekani milioni 1,805.12 na utatengeneza ajira za moja kwa moja kwa watanzania zipatazo 16,355, fedha za kigeni, na kodi kwa serikali.

Naye mwenyekiti wa bodi ya TIC Dkt. Bilinith Mahenge amesema kuwa kazi kubwa imefanyika kukamilishwa kwa mikataba hiyo ambapo sasa TIC imejipanga kuongeza wawekezaji kutokana na sheria mpya ya uwekezaji ya mwaka 2022 ambayo imeboresha mazingira ya uwekezaji nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bw. Gilead Teri amesema kuwa miradi iliyopewa hadhi ya kimkakati na kamati ya Taifa ya Uwekezaji NISC ni pamoja na Kongani ya Viwanda Kwala, Kilombero Sugar, Mradi wa mchele wa Wilmar, Lake Cement, uchakataji wa gesi na kampuni ya Oilcom, Mradi wa mafuta ya kula wild flower, mufindi paper mills, lodhia steel, dangote cement na mount meru millers.
 

Attachments

  • FzUUjluWIAAxDVM.jpg
    FzUUjluWIAAxDVM.jpg
    155.2 KB · Views: 5
  • FzUUihHXsAAw86W.jpg
    FzUUihHXsAAw86W.jpg
    238.8 KB · Views: 5
  • FzUUkl6XoAMUtpy.jpg
    FzUUkl6XoAMUtpy.jpg
    203.1 KB · Views: 4
  • FzUUlYEXwAk6e6d.jpg
    FzUUlYEXwAk6e6d.jpg
    112.3 KB · Views: 4
Back
Top Bottom