Kimsingi Kenya haiwezi kuwa na lengo la ku-export gas kutoka Tz in the near future. Huo utakuwa zaidi ya ukichaa kwao.
Kwa kuzingatia kanuni za uchumi wa usafirishaji ni more economical kuelekeza hilo bomba Mombasa kabla ya Nairobi hata ikiwa Nairobi ndiko kuna viwanda vingi.
Miji ya pwani ina potential kubwa zaidi ya kuwa industrialized kuliko ile ya inland. Hapa nazungumzia miji iliyoko kati ya Dar na Nairobi (Tanga inclusive). Hivyo bila shaka wanatambua kuwa sisi tutataka bomba lipite kwanza Tanga.
Pia hizi nchi zetu bado hazijajenga misingi ya industrialization. Ili ujenge sekta imara ni lazima ujenge kwanza basic industries ambazo mainly ni steel & chemical.
Ukiiangalia Jiografia ya Kenya, ni wazi mji unaopaswa kubeba hizo heavy industries ni Mombasa (kwa kuanzia na pengine Lamu hapo baadae). Gesi ni input kubwa sana kwenye basic industrialization.
Hivyo ni wazi bomba lazima liambae kwenye Pwani ya EA kisha kuwa branched kuelekea mainland.
Nadhani itakuwa rahisi tu kuliextend kutoka Mombasa hadi Nairobi.
Sent using
Jamii Forums mobile app