Sasa moja kwa moja kwenye mada husika,tangu huyu Mama aingie madarakani nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana mwenendo wake,ingawa kweli ni mapema sana kuanza kumtolea hukumu,lakini nachelea kusema huyu Mama HATUFAI hata kidogo especially kwa wale tunaotaka kuona Tanzania inapiga hatua za kweli za kimaendeleo na sio siasa,
Kwa sasa nisingependa kuongea mengi ila ninachoweza kusema ni kwamba HAJUI Taifa hili linataka nini ili kujikomboa,anaonekana ni mtu wa KUFURAHISHA watu tu,bila kujali hii inchi inaathirika au inafaidika vp na anachokifanya,nauona mtindo wa utawala wa Kikwete ukijirudia kwa kasi sana nchini,
Ni dhahiri mpaka sasa huyu Mama anafanya mambo kwa kupangiwa au kuchukuliwa na upepo tu wa kwenye mitandao ya kijamii lakini yeye binafsi hana mipamgo na maono yoyote ya kueleweka juu ya Tanzania.