We wa koromije uliyekuja juzi Dar na fuso ya dagaa huwezi mjua Makalla!! Kaa utulie au rudi ukauze furu Chato.
Nimecheka Sana Watu mnamajungu na fitna zaidi yq Makatibu Uenezi mbona hii nafasi mnaofaa mpoo wengi humu teuzi inayofata Mama apitie humu atapata Watu wa kumfaa 😂
 
Ally Hapi ni mfano mzuri kwa kufanya kilimo baada ya kutenguliwa ukuu wa mkoa. Ameonesha kwa vitendo kwamba siyo lazima apate cheo cha kisiasa ili aishi.
Kwa uzoefu aliopata kwenye kilimo, atakuwa kiongozi anayejua shida za wakulima.
 
Wataalamu wa serikali na siasa hii ya kupata appointment za chama na serikali inaingilianaje? Inaruhusiwa kisheria hiyo?
 
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo tarehe 03 April, 2024 jijini Dar Es Salaam, katika kikao chake maalum, chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na masuala mengine, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, imefanya mabadiliko madogo ya Sekreteriet ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kuwachagua wajumbe kama ifuatavyo:
  • Ndugu John Mongella kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, akichukua nafasi ya Anamringi Macha ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Shinyanga,
  • Ndugu Amos Gabriel Makalla kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, akichukua nafasi ya Ndugu Paul Makonda ambaye ameteulia kuwa Mkuu wa Mkoa Arusha.
  • Ndugu Ally Salum Hapi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania, akichukua nafasi ya Ndugu Gilbert Kalima ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga,
  • Ndugu Jokate Urban Mwegelo kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM akichukua nafasi ya Ndugu Fakii Raphael Lulandala ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.
Aidha katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imezipongeza Serikali zake zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, chini ya Rais Dkt. Hussein Mwinyi, ambaye pia ni Mwenye kiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa kazi kubwa na nzuri ya kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 – 2025.

IMETOLEWA NA IDARA YA ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO 03 APRIL, 2024
Lucas Mwaashambwa na Mayalla naona wanaendelea kukosa mvuto.
 
Back
Top Bottom