Rais Samia amuasili mtoto mchanga aliyetelekezwa Nzega

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Rais Samia Suluhu Hassan, amemuasili mtoto mchanga wa kike Machi 11, 2026, katika makazi yake, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.

Mtoto huyo aliyepewa jina la Grace Samia Suluhu Hassan alitelekezwa mjini Nzega, mkoani Tabora, na amekabidhiwa kwa Rais Dkt. Samia na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Naitapwaki Tukai.

Akizungumza wakati wa kumkabidhi mtoto huyo, Mkuu wa Wilaya Tukai alisema mtoto huyo aliokotwa Januari 17, 2026 akiwa ametelekezwa katika eneo jirani na nyumba ya wageni ya Kasulu, Nzega Mjini.

Alieleza kuwa baada ya kupokea taarifa hizo, alishirikiana na Jeshi la Polisi kumchukua mtoto huyo na kumpeleka hospitalini kwa uchunguzi na uangalizi, huku juhudi za kumtafuta mama yake zikiendelea bila mafanikio.

Rais Samia amemkaribisha mtoto huyo katika familia yake na kuahidi kumpatia malezi, ulinzi na huduma zote muhimu ili akue katika mazingira salama na yenye upendo.

“Wanaotupa watoto hawajui wanalolifanya. Kuliko kumtupa mtoto ni afadhali ukamkabidhi katika mamlaka za kisheria au kituo cha kulelea watoto. Kila mtoto aliyezaliwa ni hazina, na hatuijui kesho yake,” alisema Rais Dkt. Samia.

1773219965645.png

Source: Ikulu
 
Kwahiyo huyu m1 ana thamani kuliko watu maelfu walio angamizwa tar 29/10?

Km huyu aliokotwa huko alikotupwa, basi na wale waliokufa 29/10 watupwe ili ndugu na wahusika wao wawaokote pia wakawahifadhi kadri ya taratibu zao.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemuasili mtoto mchanga wa kike leo tarehe 11 Machi, 2026, katika makazi yake, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.

Mtoto huyo aliyepewa jina la Grace Samia Suluhu Hassan alitelekezwa mjini Nzega, mkoani Tabora, na amekabidhiwa kwa Rais Dkt. Samia na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Mhe. Naitapwaki Tukai.

Akizungumza wakati wa kumkabidhi mtoto huyo, Mkuu wa Wilaya Tukai alisema mtoto huyo aliokotwa tarehe 17 Januari, 2026 akiwa ametelekezwa katika eneo jirani na nyumba ya wageni ya Kasulu, Nzega Mjini.

Alieleza kuwa baada ya kupokea taarifa hizo, alishirikiana na Jeshi la Polisi kumchukua mtoto huyo na kumpeleka hospitalini kwa uchunguzi na uangalizi, huku juhudi za kumtafuta mama yake zikiendelea bila mafanikio.

Rais Samia amemkaribisha mtoto huyo katika familia yake na kuahidi kumpatia malezi, ulinzi na huduma zote muhimu ili akue katika mazingira salama na yenye upendo.

“Wanaotupa watoto hawajui wanalolifanya. Kuliko kumtupa mtoto ni afadhali ukamkabidhi katika mamlaka za kisheria au kituo cha kulelea watoto. Kila mtoto aliyezaliwa ni hazina, na hatuijui kesho yake,” alisema Rais Dkt. Samia.
Huyu sasa ndie yule Samia, tuliyemzungumzia hapa, Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” ambaye ni tofauti na yule aliyesema ile nguvu iliyotumika ilikuwa nguvu stahiki!.

Kitendo hiki alichokifanya, Rais Samia, cha kumuasili huyu mtoto, malaika wa Mungu, kitamrudishia thawabu saba mara sabini, na kuipunguza adhabu yake ya karma ya October 29 kwa kiasi kikubwa!. The Power of Karma- Ndio hukumu pekee ya haki kamili hapa Duniani. Unahukumiwa kwa matendo yako!, humo nilisema,
Kila Mtenda Mema, Hulipwa na Karma, Mema Mara Dufu!.
Hapa ndipo inapokuja hoja ya kila mtenda wema, atalipwa mema na kila mtenda ubaya au maovu atalipwa ubaya au uovu na malipo haya hufanyika hapa hapa duniani, ila malipo huwa ni mara dufu ya wema ulioutenda, au uovu ulioutenda, hii ndio hiyo karma yenyewe, what goes around comes around!.

Uzuri wa Karma ni Reversible, Ukifanya Ubaya, Unaweza Kuupindua Ubaya Huo Kwa Wema, Ukaepuka Adhabu ya Karma!.
ila pia kwa kujitambua, ukifanya jambo baya, ukaomba msamaha kabla karma haijaanza kukushughulikia, then una weza ku reverse bad karma isikutokee, au hata kuizuia kabisa kwa kufanya mema mengi zaidi kuliko uovu!. Hii inaitwa kuireversi karma, hivyo mtu muuaji, akibaini kosa lake na kujutia, kisha akatembea na fuko la fedha kuwagawia yatima na masikini, adhabu ya karma ya uovu wake inapinduliwa na mema yake, anabarikiwa!.

Paskali
Hili Rais Samia alilofanya ni jema,
Mungu ambariki sana Rais Samia.
 
Huyu sasa ndie yule Samia, tuliyemzungumzia hapa, Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” ambaye ni tofauti na yule aliyesema ile nguvu iliyotumika ilikuwa nguvu stahiki!.

Kitendo hiki alichokifanya, kumuasili huyu mtoto, kitamrudishia thawabu saba mara sabini, na kuipunguza karma ya October 29 kwa kiasi kikubwa!.

Mungu ambariki sana Rais Samia.

P
Kwa hiyo mkuu tufanye ujambazi tu ila tusaidie mambo yanakaa poa tu?
 
.
Huyu sasa ndie yule Samia, tuliyemzungumzia hapa, Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” ambaye ni tofauti na yule aliyesema ile nguvu iliyotumika ilikuwa nguvu stahiki!.

Kitendo hiki alichokifanya, Rais Samia, cha kumuasili huyu mtoto, malaika wa Mungu, kitamrudishia thawabu saba mara sabini, na kuipunguza adhabu yake ya karma ya October 29 kwa kiasi kikubwa!. The Power of Karma- Ndio hukumu pekee ya haki kamili hapa Duniani. Unahukumiwa kwa matendo yako!, humo nilisema,

Hili Rais Samia alilofanya ni jema,
Mungu ambariki sana Rais Samia.

P
White washing..
 
Hata afanye zuri lipi kwa sasa hakuna atakae msifia au kumpongeza ashaharibu kitambo sana. Akitaka afanye zuri ambalo litagusa wote aachie kiti hapo
Usitujumuishe kwenye ujinga wako huo

Sema wewe hautampenda
 
Huyu sasa ndie yule Samia, tuliyemzungumzia hapa, Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” ambaye ni tofauti na yule aliyesema ile nguvu iliyotumika ilikuwa nguvu stahiki!.

Kitendo hiki alichokifanya, Rais Samia, cha kumuasili huyu mtoto, malaika wa Mungu, kitamrudishia thawabu saba mara sabini, na kuipunguza adhabu yake ya karma ya October 29 kwa kiasi kikubwa!. The Power of Karma- Ndio hukumu pekee ya haki kamili hapa Duniani. Unahukumiwa kwa matendo yako!, humo nilisema,

Hili Rais Samia alilofanya ni jema,
Mungu ambariki sana Rais Samia.
Daaah Mzee Pasco Unafki ni jadi Yako 😁😁😁😁
 
Rais Samia Suluhu Hassan, amemuasili mtoto mchanga wa kike Machi 11, 2026, katika makazi yake, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.

Mtoto huyo aliyepewa jina la Grace Samia Suluhu Hassan alitelekezwa mjini Nzega, mkoani Tabora, na amekabidhiwa kwa Rais Dkt. Samia na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Naitapwaki Tukai.

Akizungumza wakati wa kumkabidhi mtoto huyo, Mkuu wa Wilaya Tukai alisema mtoto huyo aliokotwa Januari 17, 2026 akiwa ametelekezwa katika eneo jirani na nyumba ya wageni ya Kasulu, Nzega Mjini.

Alieleza kuwa baada ya kupokea taarifa hizo, alishirikiana na Jeshi la Polisi kumchukua mtoto huyo na kumpeleka hospitalini kwa uchunguzi na uangalizi, huku juhudi za kumtafuta mama yake zikiendelea bila mafanikio.

Rais Samia amemkaribisha mtoto huyo katika familia yake na kuahidi kumpatia malezi, ulinzi na huduma zote muhimu ili akue katika mazingira salama na yenye upendo.

“Wanaotupa watoto hawajui wanalolifanya. Kuliko kumtupa mtoto ni afadhali ukamkabidhi katika mamlaka za kisheria au kituo cha kulelea watoto. Kila mtoto aliyezaliwa ni hazina, na hatuijui kesho yake,” alisema Rais Dkt. Samia.

Source: Ikulu
Hii haiwezi kufuta dhambi yake ya kutuulia watoto wetu zaidi ya 10,000.
 
Hamna mtoto aliyetelekezwa hapo,

Ni janja janja tu.
 
Back
Top Bottom