"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178
karma.jpg

Wanabodi,

Sio mara moja au mbili, umewahi kusikia mtu akitendewa jambo baya, anasema "namwachia Mungu!", au neno "Malipo ni hapa hapa duniani!". likitokea jambo zuri lolote watu hufurahi na kumshukuru Mungu, au likitokea jambo baya lolote, watu hufarijiana kuwa kusema hiyo ni "kazi ya Mungu!'. haina makosa!. Natumaini mmewahi kusikia kuwa kuna watu wenye bahati, familia zenye bahati, wamebarikiwa, wamesoma na wote wana kazi nzuri, na kuna watu/familia wenye mikosi, wamelaaniwa na kuandamwa na majanga, mikosi etc?, au nini huwa kinampata mtu aliyeachiwa kitu kinachoitwa 'laana!"?.

Hakuna kitu chochote ni kipya chini ya jua, hakuna bahati nzuri wala bahati mbaya, hakuna jambo lolote linalotokea kwa kujitokea tuu, au kwamba limetokea ghafla tuu, au kwa bahati mbaya, or just a coincident!, no way!. Kila jambo linalotokea, linatokea kwa sababu na lilikuwa destined kutokea hivyo hivyo lilivyotokea, yaani everything is a premeditated move, caused by cause and effects, by our actions or inactions!.

Jee ni nguvu gani zinafanya watu wengine wafanikiwe, na mambo yao kuwaendea vizuri, huku watu wengine wakikwama, kuandamwa na mikosi, majanga, mabalaa na kuishi kwenye maisha duni na umasikini uliotopea huku wakiandamwa na majanga, visa na mikasa lukuki?!.

Hizi ni powers zinazotumika kwenye 'cause and effects', ndizo zinazoitwa "Powers of Karma" yaani "what goes around, comes around".

Mambo yote haya hufanya kwa kupitia nguvu zinazoitwa Universal Laws, ambazo zinatumia zile kanuni tatu za Newtons Laws of Motion.


Kanuni ya Kwanza ya Karma ni The 1st Newstons Law of Motion
Newton's
first law states that "every object will remain at rest or in uniform motion in a straight line unless compelled to change its state by the action of an external force. ... The third law states that for every action (force) in nature there is an equal and opposite reaction"

Kanuni hii ni kuwa kila kitu kitaendelea kuwa hivyo kilivyo kilivyo hadi nguvu nyingine ije kukibadilisha. Yaani kama kitu kimesimama, kitasimama hivyo hivyo hadi nguvu nyingine ije kukihamisha, au kikiwa kwenye motion, kitaendelea kwenda hadi nguvu nyingine ije kukisimamisha! . Every object in a state of uniform motion tends to remain in that state of motion unless an external force is applied to it.
Kanuni ya Pili ya Karma, The 2nd Newtons Law of Motion
The second law states that the acceleration of an object is dependent upon two variables - the net force acting upon the object and the mass of the objec
t.
Hii ndio kanuni ya mafanikio katika kila jambo unalolitenda hadi mafanikio ya kimaisha, kufundisha kuwa ili kupata mafanikio katika jambo lolote, yatategemea nguvu unayotumia katika kulitekeleza jambo hilo. Ukifanya kazi kwa bidii kwa kutumia nguvu kubwa utapata mafanikio makubwa,

Kanuni ya Tatu ya Karma ni The 3rd Newton's Law of Motion.
Kanuni ya tatu ya kila nguvu itakayotumika kukihamisha hicho kitu, kuna nguvu nyingine ya pili, ambayo pia inatengenezwa ikivuta upande tofauti na hiyo nguvu inayotumika. For every action there is an equal and opposite reaction. This is the law of cause and effects!.

Msingi wa hoja hiyo ndio hizo nguvu zinazotumika kufanya kila kinachotokea duniani kwenye maisha ya kila binadamu! na ulimwenguni kwa ujumla zikiitwa cosmic forces. Yaani binadamu ameumbwa kwa mwili wa nyama, na damu ya kimiminika (Ying na Yang) na sehemu kubwa ya mwili wake ni maji, lakini kitu kikubwa binadamu alichoumbwa nacho ni roho, yaani spirit, uhai, hii roho yenye uhai, imeumbwa kwa powers, ndio hivyo nguvu responsible kwa kila kitu kuanzia uhai hadi kila kitu kinachomtokea binadamu, kinasababishwa na nguvu hizi zilizoko ndani ya kila binadamu, ambazo zinaitwa 'nature!'.


Wafanya Miujiza ya Uponyaji Wanatumia Nguvu Zao Kuamshia Nguvu Zako Ndizo Zinakuponya!
Wachungaji wote na imani za wokovu, walokole, wanaojitapa kuwa wana nguvu za uponyaji, au waganga wa kienyeji au tiba asili na tiba mbadala wanaotibu kwa kutumia tiba ya imani, (faith healing), wanatumia hizi powers zao kuziamsha tuu nguvu hizi zilizoko ndani yako, yaani ndani ya kila mtu kuna hizi nguvu, ambazo zikiamshwa ndizo zinazotenda miujiza ya uponyaji na mtu kujiponya mwenyewe bila kujijua huku akiamini huyo Mchungaji au mganga ndie amemponyesha!.

Kinachoponya ni Imani Yako Ndio Ina Nguvu za Uponyaji na Sio Mganga au Jina Lolote!
Wachungaji hutumia Jina la Yesu kuponyea, kutokana na kuamini, milango ya nguvu za Mungu zilizo ndani yako inafunguka na kuzifanyia muujiza wa uponyaji kwa kuamini ni Jina la Yesu, lakini kiukweli kilicho kuponya sio hizo nguvu za Mchungaji wala sio hilo jina Yesu bali ni nguvu zako zilizo ndani yako ila zimewezeshwa kuamka na kukuponya kwa imani yako kupitia kuamini ni Jina la Yesu, hivyo kinachoponya ni imani yako. Waganga wa kienyeji hutumia tunguli kuziamsha.

Mungu Hayuko Juu Mawinguni, Mungu ni Omnipresent, Yupo Kote Hadi Ndani Yako!
Wengi huwa wanaomba Mungu kwa kutazama juu kwa sababu hivyo ndivyo wengi tuliovyoaminishwa kwa kudanganywa na hizi dini za wazungu na waarabu kuwa Mungu yuko juu mbinguni, peponi, ahera, mawinguni etc, kitu ambacho sii kweli!.

Dunia ni Dunia Mbili, Physical World, Ulimwengu wa Mwili na Spiritual World, Ulimwengu wa Roho
Hii dunia tuliomo, japo inaonekana kama ni dunia moja au ulimwengu mmoja, sio dunia moja wala ulimwengu mmoja, bali ni dunia mbili, dunia hii au ulimwengu huu wa kifizikali, yaani Physical World wenye vitu vya kuonekanika, watu, ardhi, wanyama, mimea, milima, mabonde, bahari, mito, maji, hewa etc, na kuna dunia au ulimwengu mwingine ambao ni Spiritual World, Ulimwengu wa Roho, ambao haionekani kwa macho ya mwili bali kwa macho ya roho, huko sasa ndio mbinguni. Ulimwengu huo ndio mbinguni kwa mungu, huko zinaishi roho, spirits, both good and bad, huko ndiko mbinguni kwa Mungu na motoni kwa shetani.

Hivyo ukweli wa Mungu wa kweli hayuko mbinguni wala mbinguni sio juu mawinguni!, bali mbinguni, motoni na duniani kote ni hapa hapa tulipo, ila kategemea na state ya kiumbe kilivyo, ukiwa kwenye physical state of flesh state, mwili wa nyama kama tulivyo then tunajiona tuko duniani ndani ya physical world na mbinguni tunaelekezwa ni juu, lakini tukichange state into spirit, then ndio tunajiona tuko mbinguni, peponi or motoni, lakini Mungu wa kweli ni omnipresent, yupo popote na kila mahali, na sii mbinguni tuu, na kitu ambacho dini nyingi hazifundishi ni kuwa Mungu wa kweli, yuko ndani yako!.


Binadamu Ameumbwa Kwa Sehemu Mbili, Body, Mwili na Spirit, Roho

Kama ilivyo dunia ina sehemu mbili za ulimwengu wa mwili na ulimwengu wa roho, binaadamu nae ana sehemu mbili, ule mwili wa nyama ulioumbwa kwa udongo, mwili huu ndio unaokufa, kuoza na kurudi mavumbini, ila mwili wa roho, ulioumbwa na ile pumzi ya uhai binadamu aliyopuliziwa Mungu na kupata uhai, yaani 'life force', mwili ule haufi, unaishi milele, hivyo huko mbinguni na motoni, mwili unaokwenda kule ni ule mwili wa roho, huu mwili wa nyama ni kasha tuu, ukiisha kufa, zile taratibu nzuzi za mazishi, kwenye jeneza zuri, kaburi zuri, siku hizi hadi makaburi ya marumaru, kwa lengo la kukuhifadhi vizuri, ni kufurahisha tuu nafsi zetu, mwili huu wa nyama ukiisha kufa, ndio kwisha habari yake, unakwenda kugeuka mavumbi, na hapa naomba ili nisikosee heshima maiti za binaadamu, naomba nisiseme kile kinachoutokea huo mwili huko sandukuni baada ya kuzikwa, lati watu wangekuwa wanapata fursa ya kuuona huo mwili huko kabuni nini kinautokea, watu wengi wanfe opt for cremation na sio burial!.

Subject matter ya bandiko hili ni zile powers za Mungu zilizo ndani yetu na ndizo responsible kwa kila kitu kinachotokea kwa kila kiumbe humu duniani wakiwemo binadamu na ndizo zinazoitwa karma!.


Binadamu Ana Powers Ndizo Responsible Kwa Kila Kitu!.
Kupitia nguvu hizi za Mungu zilizo ndani yetu, binadamu amepewa utashi wa kuamua kuchagua au atende matendo mema au atende matendo mabaya au maovu!. Akitenda mema, ile nguvu inategeneza kitu kinachoitwa "positive energy", hivyo kila jema analotenda kwa kulitoa ndani yake, jema hili linatengeneza positive energy, ambayo inatoka ndani yake na kuwafikia wengine, hiyo nguvu ya matendo mema utakayo tenda, inafuata ile kanuni ya Newton kwa kureproduce equal and oposite positive energy ambayo itavurumishwa kutoka kila upande ambao umepeleka wema na kukuzalishia wema kutoka kila upande na kukurudia wewe, hivyo wema huo utakurudia kwa nguvu mara dufu ya ile uliopeleka wewe na hapa sasa ndipo inapotumika kanuni ya tatu ya Newton, ambayo ule wema ulioufanya utalipwa mara dufu na utakurudia wewe na kizazi chako kutegemeana na ukubwa wa wema wenyewe!. The relationship between an object's mass m, its acceleration a, and the applied force F is F = ma. Acceleration and force are vectors. in this law the direction of the force vector is the same as the direction of the acceleration vector.

Kila Mtenda Mema, Hulipwa na Karma, Mema Mara Dufu!.
Hapa ndipo inapokuja hoja ya kila mtenda wema, atalipwa mema na kila mtenda ubaya au maovu atalipwa ubaya au uovu na malipo haya hufanyika hapa hapa duniani, ila malipo huwa ni mara dufu ya wema ulioutenda, au uovu ulioutenda, hii ndio hiyo karma yenyewe, what goes around comes around!.

Mfano wewe sio lazima uwe tajiri, bali umejaaliwa kuwa na kajiuwezo japo kadogo, lakini kwa kutumia uwezo huo huo kidogo ulio nao, ukasaidia masikini. Mfano kuna masikini amelala na njaa kwa muda wa siku 3, ikipita siku ya 4 bila kupata chochote, masikini huyu atakufa njaa!. Wewe ukampa masikini yule Shilingi 500, akanunua mkate wa 100 na kuula na maji ya vichochoroni, akala na kuendelea kuishi kwa siku 5 zaidi!. Ile mia 500 yako hapa imetenda wema mkubwa sana wa kuokoa maisha ya masikini yule, hivyo positive energy itakayo kurudia wewe sio tena ya ile 500 uliotoa bali ni 500 mara 500 sawa na thamani ya ile life uliosave, hivyo wema utakao kurudia ni wema wa mamilioni!.

Vivyo hivyo unaweza kutoa msaada wa bilioni 1.6 kama alivyotoa Rugemalila kwa mama Tibaijuka, japo ametoa bilioni, kumbe net value ya mama Tubaijuka ni bilioni 100!, hivyo hicho alichotoa Rugemalila ni kama punje tuu ya mchele kwenye gunia, ambayo ni asilimia 1% ya net value ya Mama Tibaijuka la labda ni 0.01% ya gross value!, hivyo positive energy toka kwa mama Tibaijuka kwenda kwa Rugemalila ni positive energy kiduchu tuu ya asilimia 1% tuu!, kutegemeana na umuhimu wa hiyo bilioni moja!. Kama lengo halisi la msaada ule lilikuwa ni kumsaidia mama T. "kupanda ghorofani", lakini wakazuga kuwa ni fedha za kusaidia watoto wa shule, lakini ni kweli sehemu ya fedha zile, ili kwenda kusaidia watoto wa shule, then payback ya hiyo bilioni moja itabaki ile ile asilimia 1% ya net value ya mama Tibaijuka, lakini kama kweli fedha zile zote zimepelekwa kwa the needy, kule shuleni kusaidia watoto, hata kila mtoto akipata mlo mmoja tuu wa siku moja kutokana na fedha hizo, then msaada huo una produce multiplied effects ya hiyo bilioni moja kwa watoto 1000, ambayo kwao ni muhimu, itamrudia Rugemalila mara dufu!, ndio maana watu wanashangaa, baada ya wema wa Rugemalila kwenye mgao wa escrow, sasa amepata tenda ya Shilingi Trilioni 54 upanuzi wa bandari ya Mwambani Tanga!.


Muujiza wa Pesa Uitwao Money Mystic!

Kwenye mambo ya pesa hii kitu inaitwa 'money mystic" "the more you spend the more you get!". Ila hiyo spending iwaguse the need ambayo watatoa big and huge positive energy ndio maana from time to time tunashuhudia matajiri wa kihindi na kiarabu, wanaojua the power of karma, wakiwafolenisha watu masikini siku nzima, kisha kuwapa mgao wa 10,000 some specific days siku ya Ijumaa na haswa kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani, au kuwafuturisha watu masikini/yatima etc, wanatengeneza hii positive energy ambayo wema wake hurudi maradufu!. Hii pia inasababisha wale masikini mnaowaona mjini haswa omba omba hawaishi kwa sababu wanapata!. Kanuni hii pia hutumia na matajiri wanaitwa ma philanthropists ku multiply utajiri wao, hivyo msiwashangae kina Manji, Mo, Mengi ku spend bilions za misaada kwa ufadhili wa timu za soka, au kufadhili masikini, huku wafanya kazi wakilipwa kiduchu na wakati mwingine kukosa hata mishahara on time!.

Kila Mtenda Ubaya, Hulipwa na Karma, Ubaya Mara Dufu!.
Vivyo hivyo kama ambavyo wema hurudi kwa kulipwa mema mara dufu, vivyo hivyo ukitenda ubaya, ubaya ule pia nao una tabia ile ile kama ya wema, nao pia huwa unakurudia mara dufu, unaweza kutenda ubaya mdogo tuu mfano mama wa kambo kumtesa mtoto yatima, kwa kumlaza na njaa, pay back ya mapigo yake ni kubwa sana kuliko ubaya unaotendwa!.

Sisi Wakristu Wakatoliki tulifundishwa kuwa siku ya hukumu ya mwisho, matendo yako mema yanachukuliwa na kuwekwa kwenye mizani, na kulinganishwa na matendo yako mabaya/maovu, mema yakizidi, unaingia mbinguni, mabaya yakizidi, unatupwa motoni!. Lengo ni binadamu tutende mema kuliko maovu!.


Maajabu ya Karma, Waovu Kulipwa Mema, Wema Kulipwa Maovu, Mfano wa Bush, Blair na Obama Upande Mmoja Huku Osama, Saadam na Gaddafi Upande Mwingine!.

Kwa kutumia kanuni hii, mfano Osama aliua idadi fulani ya watu ile September 11 kule Marekani lakin Osama huyo amewasaidia Taleban wengi zaidi kuliko idadi ya wale aliowaua kwenye September 11, na Bush kwa hasira ya September 11, ameaua watu wengi zaidi wasio na hatia kule Iraq, kuliko wale Osama aliowaua, siku ya hukumu ya mwisho, mnaweza kushangaa kuwakuta Osama, Saadam na Gaddafi wakaingia peponi!, halafu Bush, Blair na Obama wakatupwa motoni!.

Vivyo hivyo mnaweza msiamini pale mtakaposhuhudia viongozi wa dini tunao waaminia, wakitupwa motoni, huku majambazi na wauaji wakipeta kuingia peponi, kutegemeana na ukumbwa wa wema wao ukilinganisha na ubaya wao, yaani ile 'karma ya mema yao ndio what matters most after all tunaokolewa kwa neema na sio kwa matendo, na ila kuhukumiwa ni kwa matendo mema au mabaya yako.

Karma ina Apply Kwenye Kila Kitu, Kisiasa, Kiuchumi, Kijamii!.
Karma hii ina apply kwenye kila kitu, kifamilia, kisiasa, kiuchumi na kijamii mfano Zitto ametimuliwa Chadema kwa tuhuma za usaliti, kama ni kweli Zitto ni msaliti, then Karma ya usaliti itamshughulikia Zitto na hiki Chama chake cha ACT kitajinyaukia na kujifia kabla hata hakujakuchwa kwa uchaguzi!, na Chadema kitaendelea kung'ara, kuneemeka kuchanua na kushamiri!. Lakini kama Zitto amesingiziwa usaliti na hakuhukumiwa kwa haki bali ameonewa, then Karma ya kuonewa itamlipa Zitto kwa kumuimarisha, ACT itaneemeka, itachanua na kung'ara, Zitto atarejea bungeni kwa kishindo, wakati Chadema, wale walio husika kusingizia uovu, karma itawatandika bakora za Karma, mmoja baada ya mwingine, in two ways, a collective karma kwa Chadema kama chama kitakula bakora zake na kitaishia kupukutika, lakini wana Chadema individual wenye mkono kwenye dhulma hii kwa Zitto, nao karma zao zitawatembelea mmoja mmoja kwa mujibu wa mchango wake hivyo watadhoofika, kudorora na kunyauka!.

Pamoja na Karma Kuwa Hukumu ya Haki, Ina Uzuri na Mazuri Yake, Uzuri wa Karma ni...
Pamoja karma kuwa ndio hukumu pekee ya haki hapa duniani, pia karma nayo ina mazuri yake na mabaya yake. Moja zuri kubwa la karma ni kila unachotenda, lazima utalipwa!, haikopeshi!, ukitenda mema, utalipwa mema na ukitenda ubaya utalipwa ubaya au lazima utalipa, ila pia katika hukumu za karma, kuna wakati unatenda baya dogo, unakuja kulipwa ubaya mkubwa wa ajabu, au una tenda ubaya, haulipwi ubaya na unalipwa wema, vivyo hivyo, kuna wakati unaweza kutenda wema mdogo, ukalipwa wema mkubwa ajabu, au ukatenda wema mkubwa, ukalipwa wema kiduchu au usilipwe na hata ukulipwa ubaya!. This explani kwanini sometimewa watu wabaya ndio wanapeta, halafu watu wema wanasulubiwa!.


Uzuri Mmoja wa Karma, Ukitenda Wema Halafu Ukafa Kabla ya Kulipwa, Familia Yako Inalipwa!.
Kwa haraka haraka na uzuri mmoja wa karma na ubaya mbili. Uzuri ni ukitenda wema halafu ukafa kabla ya karma kukulipa ule wema wako, then familia yako uliyobakia huku nyuma, itaendelea kulipwa pensheni ya wema wewe ulioutenda hivyo kupelekea watu kuona kuna familia fulani fulani zimebarikiwa kila wanafamilia hiyo wanapata mafanikio lukuki!, na hapa ndipo ulipo ule msemo wa "wema hauozi", and tenda wema uende zako, usitarajie shukrani", ikimaanisha ukitenda wewe wowote bila kujionyeshea wala kujitangaza, unapata karma kubwa zaidi, kuliko wale watenda wema huku wakijitangaza!, mfano Bakhressa anasaidia sana ila kamwe hutakaa uone akiita waandishi kujitangaza au kuonyeshea jinsi anavyosaidia!. Hili la kutenda wema, kiofisi linaitwa Corporate Social Resiponsibility (CSR) ambalo makampuni au mashirika yanafanya wema kwa jamii iliyowazunguka, hivyo ku produce positive energy itakayofanya wakubalike na kupendwa katika eneo husika. Huku kukubalika na kupendwa, kuna produce positive energy, ambayo inayanyoosha mambo ya hiyo kampuni, kama ni mgodi, unatema!.

Ubaya Mmoja wa Karma, Ukitenda Ubaya Halafu Ukafa Kabla ya Kulipwa, Familia Yako Inafidia!.
Kama ilivyo kwa wema, na kwa ubaya ni vivyo hivyo!, ukitenda ubaya au uovu, halafu ukafa kabla ya kuchapwa bakora za karma kuulipia ubaya wako, kwa vile malipo ni hapa hapa duniani, then familia yako uliyoiach huku nyuma ndio inaendelea kuubeba ubaya huo, hivyo kuchwapwa hizi bakora za karma bila kosa lolote!, kitu ambacho kwa maoni yangu, this is not right na sio fair kabisa, it is very unfair!.

Sometimes Karma Haitendi Haki ni Unfair na Unjust!
Ubaya wa pili wa karma ni kiwango cha adhabu kinakuwa determined na maumivu ya mtendewa na sio mtenda. Unaweza kutenda dhambi kubwa kama kumuua mtu adhabu yake inapaswa kuwa kubwa lakini ukakuta mtu ni muuaji halafu anapeta tuu, kumbe yule uliyeuliwa alikuwa muovu sana, mchawi, mlozi, mwanga, mfitini, mchonganishi etc kiasi kwamba kifo chake ni blessing kwa wengi, muuaji anabarikiwa badala ya kuhukumiwa. Na ukakuta mtu umetenda ubaya mdogo tuu kama kumuahidi mtu kumuoa halafu humuoi, ikitokea huyo mtu hakuolewa tena, mapigo ya karma yatayokushukia ni usipime.
Yaani unaweza kupata mapigo makubwa kwa kosa ndogo na mapigo madogo kwa kosa kubwa. This is not fair.


Kama Inawahukumu Wasio na Makosa!
Mfano kwa mtoto mdogo malaika wa Mungu kuzaliwa bila dhambi yoyote kisha anakuja kujikuta kumbe mzazi wake alifanya ubaya fulani, hivyo mtoto huyo kujikuta anapaswa kubebeshwa mizigo ya dhambi za wazazi wake bila kosa lolote!.

Karma Hutoa Hukumu Kali Kwa Makosa ya Hisia, Emotions Yanayosababisha Kulia Machozi ya Ndani!
Kati ya malipo makubwa ya 'karma' yenye fidia kali ni pale ubaya au uovu unaofanyika ni uovu wa mambo ya moyoni, emotions kama mapenzi, uongo, kusingizia, fitna, dhulma, etc na hata uongo kwenye mambo ya mapenzi!. Mfano ikitokea binti amekupenda anatamani wewe ndio umuoe, akakuonyesha kila dalili ya kukupenda kumbe wewe hujampenda ila kwa vile kajileta, unaamua kumpitia tuu binti wa watu lakini huna mpango naye wowote wa maana zaidi ya kumtafuna!. Katika kumpitia kule binti akakuuliza utanioa?!, wewe ukajijibia tuu "ndio nitakuoa!", lakini hukumaanisha bali amejibu tuu ili kupata game!, na baada ya kupata ulichokitaka , unaendelea na maisha yako as if nothing happened huku huna mpango tena na huyo binti!. Kama binti atakuwa amejitunza ili kukutunzia kwa ajili ya ahadi yako kuwa utamuoa, na kupoteza chances zake zote za kuolewa kwa sababu yako, utakapo amua kuoa mwanamke mwingine yoyote, kama huyu binti atakuwa anakulilia chozi la ndani, ambalo karma yake ni kali sana, karma ya mtu aliyedhulumiwa!, then wewe utalipia adhabu ya karma kwa mikosi kwenye ndoa yako, hadi kumaliza deni la yule mwanamke wa mwanzo uliyemuahidi kumuoa ukamtosa, hivyo kujikuta huyo mke wako mpya ambaye hana kosa lolote kuingia kwenye ndoa ya mateso na akiadhibiwa kwa raha ya ndoa yako kuwa counter checked kwa matukio ambayo yeye hayamhusu kabisa!.

Kuweni makini sana na kutochezea feelings za watu!, if you don't mean it, don't promise chochote, ukiahidi ahadi, lazima utimize na kuitekeleze ulichoahidi, kwa sababu ahadi ni deni lazima deni hilo lilipwe, na lisipolipwa linafidiwa kwa gharama kubwa maradufu!.


Hitimisho
Kwa kumalizia, hivyo jambo lolote zuri lilikutokea, usidhanie ni kwa bahati nzuri tuu, au limejitokezea tuu!, shukuru Mungu huku ikihesabu hayo ni malipo ya mema yako au ya wazazi wako!, hivyo una obligation ya kutenda mema ili kuendelea kupata mema na kuwawekea pensheni ya mema watoto wako wakati wewe umeishaondoka kwenye dunia hii!.

Kila Majanga ni Ama ni Majaribu ya Mungu, Mipango ya Shetani au Fidia ya Karma.
Ukikutwa na majanga yoyote na mabalaa yoyote, yapokee kwa mikono miwili, kwa hoja kuwa majanga hayo yalikuwa destined kukutokea, namna hiyo hiyo yalivyotokea, yaani premeditated moves, huku ukijihesabu sababu ya hayo majanga ni moja kati ya mambo matatu haya.

Moja: Majanga hayo ni ama ni majaribu au mitihani ya Mwenyezi Mungu kukupa mitihani ni kwa kiasi gani wewe ni mcha Mungu, hivyo kukuletea majaribu ili kujihirisha uwepo wake na uwezo wake kwa kukuwezesha kuyashinda, kama alivyowafanyia wana Israel wakiwa utumwani Misri.

Pili: Majanga mengine ni kazi ya mwovu shetani, amekuletea majanga makubwa zaidi ambayo aliyapanga ikiwemo kukuangamiza kabisa wewe, familia yako na ukoo wako wote mfutike kutoka kwenye uso wa dunia, lakini Mungu ameyazuia hayo makubwa na mabaya ambayo yameelekezwa kwako, na katika vita vya kukukinga na kukuokoa, then hayo yaliyokukuta, ni kiduchu tuu, hivyo ni kushukuru Mungu, ndio nafuu yake ukilinganisha na yale yaliyozuiliwa au kuepushwa yasikufike, kama Mungu alipomuepusha Lutu na ile Sodoma na Gomola, japo Lutu alimpoteza mkewe kwa kugeuka jiwe la chumvi, na aliwalala mabinti zake bikira,na kuwapa ujauzito, yote hayo ni madogo ukilinganisha na kilitokea Sodomana Gomora.

Tatu: Majanga hayo ni mavuno ya karma ya ulichokipanda, au malipo ya fidia ya kufidia ya ulichokifanya au walichokifanya wazazi wako, hivyo una obligation ya kuepuka kufanya matendo maovu, uli usihukumiwe na kuwaachia watoto wako mizigo ya kukulipia madeni ya uovu wako wakati wewe haupo duniani!.


Uzuri wa Karma, Ukiisha Lipa, Deni Linafutwa, .
NB. Kitu kizuri kuhusu hii karma, ukiisha adhibiwa, au kupata mapigo ya karma, deni likiisha, au kuisha fidiwa, adhabu inamalizika, unainuka tena.


Uzuri wa Karma ni Reversible, Ukifanya Ubaya, Unaweza Kuupindua Ubaya Huo Kwa Wema, Ukaepuka Adhabu ya Karma!.
ila pia kwa kujitambua, ukifanya jambo baya, ukaomba msamaha kabla karma haijaanza kukushughulikia, then una weza ku reverse bad karma isikutokee, au hata kuizuia kabisa kwa kufanya mema mengi zaidi kuliko uovu!. Hii inaitwa kuireversi karma, hivyo mtu muuaji, akibaini kosa lake na kujutia, kisha akatembea na fuko la fedha kuwagawia yatima na masikini, adhabu ya karma ya uovu wake inapinduliwa na mema yake, anabarikiwa!.

Shukuru Kwa Yote!
Tukipata mema na mafanikio, tuseme asante, na tukipata balaa na majanga, pia tuseme asante, kwa sababu hata kama ni majanga, majanga mengine ni blessing in disguise, kama ilivyo kwa Yesu, japo ni Yuda ndio alimsaliti Yesu, na Yesu aliteswa kwa usaliti wa Yuda, lakini tukio lote, lilikuwa pre meditated siku nyingi, litokee hivyo hivyo lilivyotokea na kuonekana kama janga, kumbe kwa kuteswa kwake, sisi tuliponywa!.

Nawatakia Jumapili njema!.

Paskali

Kwa ufahamu zaidi kuhusu haya mambo ya powers, tembelea nyuzi hizi,
Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo Bila Kujitambua!,

"Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu ya Miujiza Ya Uponyaji kwa Imani!. Kila Mtu Anazo!.
 
Pasco
Mkuu Pasco,nimetoka kwa kanisa,nafungua JF tu,uzi wa kwanza kukutana nao ni huu.Ikabidi niweke gari pembeni,niusome mpaka mwisho,halafu ndio nikaendelea na safari zangu.
Hii kitu ungeandaa hata kitabu au fanya semina kaka,itasaidia watu wengi kujitambua.
Ubarikiwe sana Pasco na akhsante kwa neno jema sana kwa jumapili ya leo.Hakika hii imekuwa ni siku njema sana kwangu,kwanza kwa mahubiri niliyoyapata kanisani na pili kwa darasa hili la kwako.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna kitu naogopa hapa Duniani kama kumdhulumu mtu au kumshutumu Mtu yeyote yule,kutenda matendo ambayo ni kinyume na ubinadamu ikiwemo kujipatia fedha kinyume na taratibu ikiwemo rushwa au ujanja ujanja,malipo utalipa hapa hapa duniani,ni nani aliyewahi kujiuliza Polisi wa usalama barabarani mwisho wao unakuwaje?jiulize na badilika hapa duniani ukitaka kuwa na mwisho mwema kaa mbali na maisha ya ujanja ujanja
 
Hakuna kitu naogopa hapa Duniani kama kumdhulumu mtu au kumshutumu Mtu yeyote yule,kutenda matendo ambayo ni kinyume na ubinadamu ikiwemo kujipatia fedha kinyume na taratibu ikiwemo rushwa au ujanja ujanja,malipo utalipa hapa hapa duniani,ni nani aliyewahi kujiuliza Polisi wa usalama barabarani mwisho wao unakuwaje?jiulize na badilika hapa duniani ukitaka kuwa na mwisho mwema kaa mbali na maisha ya ujanja ujanja

Uliyosema ni SADKTA...malipo yote papahapa duniani.Dhana,Dhulma ni miongoni mwa dhambi na tunahadharishwa kuepukana navyo.Mimi na wewe tukifuata tuliyoamrishwa na kuacha tuliyokatazwa hakuna shaka tutafanikiwa hapa duniani na huko kwenye maisha ya milele.
Kumbuka.....Dua ya mwenye kudhulumiwa huwa haina pazia inapokelewa haraka saana.
 
Kuna jamaa mmoja alimwibia baba yake hela kakimbilia Afrika Kusini baada ya miaka 10 jamaa karudi Tz kamnunulia baba yake gari la kifahari kamjengea gorofa na kamsaidia kuinua biashara yake sasa hvi huyo mzee ni mambo safi! hapo yanaweza yakaja kumkuta kama ulivyosema hapo chini?
 
Mkuu asante sana kwa somo zuri.Nina kisa nikiangalia kinakubaliana na somo lako ijapo nina maswali pia.Nilikuwa mtumishi wa umma,sikuipenda sana kazi yangu kwani ili ufanikiwe ilikuwa ni lazima ujihusishe na either 10% ama wizi wa mali ya umma.Miaka kama miwili nyuma,alitokea jamaa fulani aliyejihusisha na ununuzi wa mali za dili ambaye alinishawishi sana nimuuzie alichotaka.Hata hivyo dhamiri yangu haikuwa radhi kuafiki ushawishi huo.Jamaa aliendelea kuniletea pesa nyingi tu lakini sikuwa radhi kukubali.Nakumbuka nilikuwa na hali ngumu kifedha lakini nilikuwa na amani sana kuikataa pesa ile haramu.Baada ya kama wiki mbili hivi,niliota ndoto ya kutisha na ilipofika asb.nilpata simu toka kwa baba kuwa anakitu muhimu sana anataka kuniambia,hivyo nisafiri hadi nyumbani sehemu iliyonilazimu niwe na zaidi ya nauli ya sh.laki 2.Sikuwa na pesa hizo kwani nilitoka kulipa ada za watoto.Nilishawishika kuchukua ile pesa haramu ili niitumie kama nauli.Haikuchukua masaa 24 nikawa nimekamatwa na kuwekwa ndani na kesi ilifunguliwa.Nikaja kujua baadae kuwa jamaa alitumia ndumba kunishawishi nichukue pesa ile kwa mujibu wa confession yake mwenyewe!Kifupi nilishinda kesi lakini ilinigharimu vitu vingi ikiwemo nyumba niliyojenga kwa jasho,gari niliuza na biashara yangu ya duka ilifilisika!Nilidhulumiwa biashara ya barbarshop ya kisasa,na sasa nimeajiriwa na mtu binafsi masimango kibao.Maswali yangu,ni kwa nini nimeona watu wengi katika kazi kama yangu wakistawi sana kwa wizi huo huo wao na familia zao na hawajawahi kuadhibiwa na "karma" kama ninavyodhani imekuwa kwangu?
Je ulozi una mchango gani kumfanya mtu atende jambo hata ambalo hakukusudia?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Kuna jamaa mmoja alimwibia baba yake hela kakimbilia Afrika Kusini baada ya miaka 10 jamaa karudi Tz kamnunulia baba yake gari la kifahari kamjengea gorofa na kamsaidia kuinua biashara yake sasa hvi huyo mzee ni mambo safi! hapo yanaweza yakaja kumkuta kama ulivyosema hapo chini?
Mkuu kaka
Jambazi
, kwanza baada ya kumwibia baba yake, yule baba hakumlaani, yaani hakumwachia radhi, bali alizidi kumuombea, hivyo ile negative karma ikawa neutralized na sala za baba!. Pili yule kijana kabla hajamuibia baba yake, aliiishajilimbikizia akiba kubwa ya positive karma kwa kutenda mema mengi au hata akiba ya pesheni ya karma iliyoachwa na babu yake, hivyo alipoiba, ile negative karma yote ikawa neutralized, hizo hizo pesa kubarikiwa na kuzaa matunda!.

Pesa yoyote ya dhulma, inaendana na negative au bad karma!.

Pasco
 
mkuu asante sana kwa somo zuri.nina kisa nikiangalia kinakubaliana na somo lako ijapo nina maswali pia.nilikuwa mtumishi wa umma,sikuipenda sana kazi yangu kwani ili ufanikiwe ilikuwa ni lazima ujihusishe na either 10% ama wizi wa mali ya umma.miaka kama miwili nyuma,alitokea jamaa fulani aliyejihusisha na ununuzi wa mali za dili ambaye alinishawishi sana nimuuzie alichotaka.hata hivyo dhamiri yangu haikuwa radhi kuafiki ushawishi huo.jamaa aliendelea kuniletea pesa nyingi tu lakini sikuwa radhi kukubali.nakumbuka nilikuwa na hali ngumu kifedha lakini nilikuwa na amani sana kuikataa pesa ile haramu.baada ya kama wiki mbili hivi,niliota ndoto ya kutisha na ilipofika asb.nilpata simu toka kwa baba kuwa anakitu muhimu sana anataka kuniambia,hivyo nisafiri hadi nyumbani sehemu iliyonilazimu niwe na zaidi ya nauli ya sh.laki 2.sikuwa na pesa hizo kwani nilitoka kulipa ada za watoto.nilishawishika kuchukua ile pesa haramu ili niitumie kama nauli.haikuchukua masaa 24 nikawa nimekamatwa na kuwekwa ndani na kesi ilifunguliwa.nikaja kujua baadae kuwa jamaa alitumia ndumba kunishawishi nichukue pesa ile kwa mujibu wa confession yake mwenyewe!kifupi nilishinda kesi lakini ilinigharimu vitu vingi ikiwemo nyumba niliyojenga kwa jasho,gari niliuza na biashara yangu ya duka ilifilisika!nilidhulumiwa biashara ya barbarshop ya kisasa,na sasa nimeajiriwa na mtu binafsi masimango kibao.maswali yangu,ni kwa nini nimeona watu wengi katika kazi kama yangu wakistawi sana kwa wizi huo huo wao na familia zao na hawajawahi kuadhibiwa na "karma" kama ninavyodhani imekuwa kwangu?
Je ulozi una mchango gani kumfanya mtu atende jambo hata ambalo hakukusudia?

Sent from my blackberry 9220 using jamiiforums

cc: Pasco
 
Last edited by a moderator:
Hiyo ya kumuahidi binti utamuoa alafu usimuoe kama ina ukweli flani,bro wangu alimuahidi binti atamuoa kisha badae akapiga chini,binti akamwambia bro atamkumbuka tu,kweli bro anasafa kweli kwenye ndoa yake hadi huwa anasema au ni laana za flani,hii mambo inaweza kua kweli!
 
ukizaliwa kwenye mishipa ya kibinadamu ukapata malezi bora na iliyojaa utu na kupata elimu ya kesho mbele ya haki itakuaje wala huhitaji kuzisoma karma hizi huwa ziko Natural.

Unajua kipi kibaya na kipi kizuri bila ya kusomeshwa kila kitu, ila utashangaa unamkuta mtu anzidishiwa pesa anasema ni riski imemjia.

Mtu anadondosha pesa au kitu chochote unasema ni riski yako na umemuona kabisa, hiyo ni dhulma na utapata majibu yake.

Unakuta kuna watu kila siku wanalalamika wanaibiwa, wanashindwa kuitafuta karma hii nini chanzo chake.
 
Pasco
"...Kwa kutumia kanuni hii, mfano Osama
aliua wale aliowaua ile Septembe 11,
lakini amewasaidia Taleban wengi zaidi
kuliko wale aliowaua kwenye September
11, na Bush kwa hasira ya September
11, ameaua watu wengi zaidi wasio na
hatia kuliko wale Osama aliowaua, siku
ya hukumu, mnaweza kushangaa
Osama, Saadam na Gaddafi wakaingia
peponi, halafu Bush, Blair na Obama
wakatupwa motoni!.

Vivyo hivyo mnaweza msiamini pale
mtakaposhuhudia viongozi wa dini
tunao waaminia, wakitupwa motoni,
huku majambazi na wauaji wakipeta
kuingia peponi, it is 'karma ya mema
yao ndio what matters' kwa
kuhukumiwa kwa neema tuu na sio
lazima kwa matendo!..."

Mkuu nimemkumbuka Mhadhiri wetu mmoja (Mnyasenga) alisema hivi:
"mwisho wa siku Mungu atahukumu mtu kwa matendo yake bila kuzingatia yuko kwa imani gani!"

Nakumbuka tulikuwemo wengi darasani (Muslim and Christian) Save me, wote waliobakia walipinga, Muslim wanaamini Hakuna asiekua Muislamu na kuingia peponi hata awe na mema kiasi gani, yaani mtu akimpinga tu Allah huyo ni Kafi.ri na hatoingia peponi! Wema wa mtu huyo ni kama sufi ktk mlima in a sense that ukija upepo tu sufi hizo zita tawanyika.
...

Then ktk maelezo yako umesema wote tunanguvu sa uungu = Miungu ni sisi wenyewe!!! Ivi mkuu ukiacha uungu wetu je unaamini kuna Mungu mwengine muweza wa vyote kama inavyodaiwa na waislamu na wakiristo?

Coz concept mzima ya karma haiamini uwepo wa Mungu huyo mmoja kama inavyodaiwa na Wakiristo na waislamu.

Hembu toa mtazamo wako hapo.
 
Last edited by a moderator:
Kule kwetu kuna msemo, 'ekajaga mu banho, itajaga mu miti', nikimaanisha 'majanga huenda kwa watu, sio miti'

Hii karma ni sisi tu kujihumu kwa mabaya tulotenda, hata utende mema kiasi gani, majanga yapo tu na ikifika yatakupata tu.

Yesu alifanya nini hadi asulubiwe? Si aliwalisha mikate, wapa mvinyo ana kuponywa bure na wakamsulubu.
Karma imepandikizwa ili watu tukae kwenye mstari.
 

Similar Discussions

70 Reactions
Reply
Back
Top Bottom