Ukitembea tembea huko mitaani hasa vijijini, utawahurumia sana wananchi wenzetu wanavyoishi kwenye hali duni kabisa kimaisha. Naam, namaanisha uduni wa kukosa huduma za msingi kama vile barabara nzuri, maji safi na salama, elimu bora, matibabu bora, mawasiliano ya uhakika, huduma za nishati...