kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,428
- 7,216
Serikali ya Samia eti inatazama mashirika ya umma kama uwekezaji wa kibiashara ambapo serikali haistahili tena kuwekeza ila watu binafsi. Msimamo huo sio sahihi kwa sababu mashirika ya kibiashara ya umma yalikwisha binafsishwa yote tangu awamu ya Mkapa. Yale yaliyobakia ni yale ya kimkakati kwa maendeleo ya nchi hayawezi kupewa watu binafsi.
Mashirika kama TANESCO, TTCL, TRC, Air Tanzania, mashirika ya kuzalisha na kusambaza maji, TPA, etc etc. Ili mashirika ya kimkakati kua na tija na kufikia malengo ya uwepo wake lazima serikali iwe na utashi wa kuyasimamia vema.
Serikali inayoruhusu vigogo wake wale kwa urefu wa kamba zao kwa vyovyote itakua na muelekeo wa kuwaacha vigogo kupora kutoka mashirika ya kimkakati ya umma na hatimae kujidai kuyabinafsisha huku ni uporaji wa mali ya umma.
Hatuna haja kuonesha kwa nini mashirika ya kimkakati kwa maendeleo ya nchi yawepo. Na tukisema maendeleo ya nchi tunamaanisha maendeleo ya umma wa wananchi na sio tabaka fulani.
Tuliwahi kubinafsisha TRC, TTCL, na air tanzania na tulichokiona kama matokeo ilibidi kuyarudisha mashirika hayo mkonono mwa umma kwa maana ya kumilikiwa na serikali.
Reli tuliibiwa na wahindi mali zote zisizohamishika kama majumba na viwanja kwa maana walipiga hela wao na mwisho hadi karibu kuibiwa uwezo wa kujitegemea kwa wao kuanza kupeleka vichwa vya treni india kwa matengenezo ambapo karakana na wafanyakazi wenye ujuzi na uwezo walibakia kinywa wazi.
Kuhusu Air Tanzania vivyo hivyo makaburu wakatuadhibu vibaya.
Kinachotakiwa ni Samia kuwa makini na ajue sera na itikadi za CCM bado ni relevant asituchanganyie ulaji kwa urefu wa kamba wakati ni uporaji wa umma.
Kinachotakiwa ni usimamizi imara wa mashirika ya kimkakata na kuacha kufanya uteuzi kishikaji ambapo wapigaji na watu wasio na weledi na uzalendo kupewa kuendesha mashirika hayo.