Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,896
- 3,206
Nchi zetu za Kiafrika kila kitu ni changamoto sana.
Viongozi wetu wanatamani kuwa viongozi wa Umma, lakini hawataki mambo yao yoyote yajulikane na Umma, Ajabu kwa kweli.
Ndiyo maana Wakili Msomi Boniface Mwabukusi aliwahi kusema kwamba; 'Kama kiongozi wa Umma hataki mambo yake yajulikane na Umma au hataki kuulizwa Ulizwa au kufuatiliwa fuatiliwa, basi aachie Ofisi zetu tuchague wale ambao wako tayari kuwajibika'.
Haiwezekani tuwatunze, tuwalishe, tuwalipe mishahara tena mikubwa sana na posho juu, halafu hamtaki hata tujue mko wapi hata kama hatujawaona ofisini kwa miezi na miezi!
Mkumbuke sisi ndio waajiri wenu. Kama mko likizo, au mnaumwa au mko ziarani ndani na nje ya nchi, tunapaswa kujua. Vinginevyo itakuwa ni dharau ya mfanyakazi (kiongozi/viongozi) kwa mwajiri wake (Umma).
Povu ruksa.