Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,754
Rais ni madaraka ya juu kabisa kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Yeye ndiye mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama.
Sheria ya Wastaafu inampa Rais unafuu mkubwa kuendelea kuhudumiwa na Hazina kwani pamoja na kujengewa makazi na serikali, anaokea mshahara 100% ya rais aliyepo madarakani na marupurupu kadhaa.
Anapewa ofisi na wahudumu wa ofisi hiyo wanalipwa kutoka Hazina.
Lakini cha ajabu ni kwamba wanarudi kinyemela kwenye ofisi za umma kwa teuzi kadhaa. Hawa wakuu wa vyuo ambao ni wastaafu ni aibu kwa nchi yetu. Chuo Kikuu kipo chini ya Waziri mhusika na kinapokuwa na mkuu wake ambaye ni rais Mstaafu ni jambo linaloaibisha sana.
Rais Mstaafu halali yake iwe ni kuongoza Tume za Kikanda ama zinazojumuisha diplomasia ya nchi na nchi. Anaweza kuongoza convoy maalum inayotupeleka dunianina siyo kuziba ajira za watu hapa nchini
Katiba Mpya iweke wazi kuwa mtu akishamaliza muhula wake wa urais basi ha-qualify kushika ofisi yeyote ya umma. Wajifunze kuridhika maana kwanza hawalipi kodi na wanaendelea kufaidi Hazina maisha yao yote. Ni kama tunageuzwa mchwa-manamba kumlisha malkia wa mchwa
Uzi tayari