Eng. Ezra Chiwelesa: Watumishi wa Umma kuanzia ngazi ya Wakurugenzi wapewe kazi kwa mikataba ya miaka 5

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Akichangia hoja bungeni Mbunge Eng. Ezra Chiwelesa amesema Watumishi wa Umma kuanzia ngazi ya Wakurugenzi wasiwe wanapata nafazi zao siziwe hazina ukomo, badala yake wapewe mikataba ya miaka mitatu au mitano na kazi hizo zitangazwe wenye vigezo waombe ili kuleta uwajibikaji katika utendaji wa majukumu yao.



Eng. Ezra amesema watumishi wa umma hawatakaa waguswe hata mara moja kwasababu wana uhakuka kuwa Waziri ataondoka lakini yeye atabaki, Katibu Mkuu ataondolewa lakini yeye atabaki.

Akisema Wabunge wa kuchaguliwa wanajikita kwenye kukamilisha majukumu yao kwakuwa wamepewa kipindi maalum cha kuonesha umuhimu wao na miaka 5 ikiisha wanachi wanasubiri kuwawajibisha. Sasa kwanini watumisi wa umma wanaachwa kufanya watakayo, wanawajibishwa wengine lakini kundi hili linaachwa kuednelea kuharibu?

Ezra asema ngazi kuanzia Wakurugenzi wapewe mikataba ya miaka mitano mitano, isizidi hapo, na kazi zitangazwe watu waombe.

Akiongeza hajawahi kusikia hata siku moja kampuni za watu binafsi zinapata hasara halafu akawaacha wale wanaosababisha hasara hiyo waendelee kuwepo, hawajakuwa sababu wanabeba watu, ni sababu kazi ni za kipindi fulani na mtu asipotimiza majukumu yake anatolewa na kuwekwa watu wengine.
 
Tuanzie kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya wanaotangaza matokeo ya uchaguzi mkuu na hata kama wamekosea hawahojiwi.
 
Back
Top Bottom