TAMISEMI kushughulikia miundombinu ya shule za umma liangaliwe upya

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Hujambo ndugu?

Nimetafakari kwa kina uamuzi wa serikali kuziweka shule za umma chini ya usimamizi wa TAMISEMI hususan miundombinu yao ninaona ni uamuzi unaohitaji kupitiwa upya.

Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mujibu wa ibara 1415 na 146 za Katiba ya JMT (nimenakili hapa chini)

MADARAKA YA UMMA Serikali za Mitaa Sheria ya 1984 Na.15 ib.50

145.-(1) Kutakuwa na vyombo vya Serikali za Mitaa katika kila mkoa, wilaya, mji na kijiji, katika Jamhuri ya Muungano, ambayo vitakuwa vya aina na majina yatakayowekwa na sheria iliyotungwa na Bunge au na Baraza la Wawakilishi. (2) Bunge au Baraza la Wawakilishi, kadri itakavyokuwa, litatunga sheria itakayofafanua utaratibu wa kuanzisha vyombo vya Serikali za Mitaa; miundo na wajumbe wake, njia za mapato na utaratibu wa utekelezaji wa shughuli za vyombo hivyo.

Kazi za Serikali za Mitaa Sheria ya 1984 Na.15 ib.20

146.-(1) Madhumuni ya kuwapo Serikali ya Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi. Na vyombo vya Serikali za Mitaa vitakuwa na haki na mamlaka ya kushiriki kuwashirikisha wananchi katika mipango na shughuli za utekelezaji wa maendeleo katika sehemu zao na nchini kote kwa jumla. (2) Bila ya kuathiri maelezo ya jumla yaliyomo katika ibara ndogo ya (1) ya ibara hii, hiki chombo cha Serikali za Mitaa, kwa kuzingatia masharti ya sheria iliyokianzisha, kitahusika na shughuli zifuatazo - (a) Kutekeleza kazi za Serikali za Mitaa katika eneo
lake; (b) Kuhakikisha utekelezaji wa sheria na ulinzi wa wananchi; na (c) Kuimarisha demokrasi katika eneo lake na kuitumia demokrasi kuharakisha maendeleo ya wananchi.


tunaona wazi kabisa majukumu yalioainishwa kwenye Katiba yamelenga kugatua madaraka na kuyapeleka kwa wananchi kupitia TAMISEMI. Jukumu hili ni pamoja na kuwashirikisha kikamilifu wananchi kupendekeza mipango ya maendeleo kwenye maeneo yao, kushiriki usimamizi wa rasilimali za umma na kustawisha demokrasia.

Kwa maamuzi ya serikali kuipa TAMISEMI jukumu la kusimamia shule zetu za umma hususan miundombinu, na hapa karibuni tukaona kabisa Waziri wa TAMISEMI akisimamia mpaka upangaji wa tahsusi kwa vijana wanaoenda elimu ya juu ya msingi ni wazi kuna muingiliano usio wa kawaida kwenye eneo hili.

Wizara ya Elimu ambayo miaka yote imekuwa msimamizi kamilifu wa shule zote za umma kuanzia msingi hadi elimu ya juu baadaye ikaja kumegwa ili kutenganisha elimu ya juu na wizara ya Elimu ikasimamia Elimu na vyuo vya Ufundi. Bado iliendelea kusimamia shule kujumuisha mtaala, udahili na hata miundombinu.

TAMISEMI bado inayo changamoto nyingi sana zinazohusisha ugatuaji wa madaraka kwa wananchi kwani inasimamia michakato na uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Viongozi jambo ambalo wabobezi wa sheria na masuala ya Uchaguzi wanaona si sawa.

TAMISEMI bado inayo changamoto kubwa kwenye eneo la usimamizi wa rasilimali za umma haswa mafungu ya pesa za maendeleo.

Kuna asilimia 20% za mapato ya Halmashauri zetu ambazo miongo kwa miongo zinasomeka kuwa zinapelekwa kuchochea maendeleo ngazi za Kata, Mitaa, Vijiji na Vitongoji ambapo hata kwenye ripoti za CAG hatuzioni pesa hizi zimesimamiwaje na mrejesho wake ni upi.

Miradi mingi ya maendeleo imewekwa chini ya Watendaji wa Kata ambao hawawashirikishi viongozi wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji kama mwongozo unavyoelekeza. Hii imechochea uduni wa ubora kwa miradi mingi ya maendeleo na kupelekea wakuu wengi wa vitengo kwenye Halmashauri kushirikiana na Watendaji Kata na Madiwani kutafuna pesa za umma

TAMISEMI inazo changamoto nyingi kwenye eneo la mfumo wa madaraka kuanzia ngazi za mkoa hadi chini. Waumini wengi wa Demokrasia tulitarajia kuona viongozi wa Mikoa, Wilaya, Mitaa, Vijiji na Vitongoji wakipitia wote kapu la uchaguzi kwa sababu kuna ombwe kati ya kamati za Vijiji, Vitongoji, Mitaa na Wilaya.

Tunahitaji kuona madiwani, Magavana wa Wilaya na Mikoa wakipitia mchakato wa Uchaguzi ili kupata wawakilishi wa Wananchi ambao wanawajibika kwa umma badala ya sasa ambapo viongozi wakuu wa Wilaya na Mikoa wanawajibika kwa Rais ambaye HAWAJIBIKI kwa umma.

Changamoto zinazoikabili TAMISEMI ni nyingi na zinahitaji utulivu na umakini kwenye kuzitatua.

PENDEKEZO LANGU
Serikali ifanye tathmini kuhusu uamuzi wa TAMISEMI kusimamia shule za umma hususan miundombinu na kama inaonekana bafo Wizara ya Elimu haina uwezo wa kusimamia moundombinu, basi kitengo cha miundombinu ya shule na vyuo vyote vya umma viwekwe chini ya Wizara ya Ujenzi na Miundombinu hususani chini ya Wakala wa Majengo ya Serikali.

Retired Mdude_Nyagali Gwappo Mwakatobe Erythrocyte Sky Eclat Pohamba David Ben Gurion Benjamin Bryceson johnthebaptist GENTAMYCINE madajose Kukudume2013 dronedrake
 
Back
Top Bottom