Mbunge Saashisha Mafuwe: Ili Mkurugenzi wa Halmashauri ateuliwe anatakiwa awe amefanya kazi miaka 12 Utumishi wa Umma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
"Nakupongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Hongera sana. Hii kwasababu una uwezo mkubwa sana na umetuheshimisha sana" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai.

"Namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayoifanya kwaajili ya nchi yetu. Juzi wananchi wa Hai walikuwa barabarani umeme ulizimika, tumewekewa taa za barabarani, barabara ya Bomang'ombe, wanasema wanamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayoifanya na Makamu wa Rais" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai.

"Kuhusu KADCO, pamoja na Uwekezaji unaofanyika Serikali imetoa Shilingi Bilioni 11 kwaajili ya kulipa fidia wananchi wa eneo la Uwanja wa Ndege wa KIA (Kilimanjaro Airport) watoke na wamekubali. Lakini Nashangaa, tumepitisha Bungeni KIA isimamiwe na Mamlaka ya Serikali lakini mpaka sasa halijafanyika, jambo hili linaudhi" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai.

"Tuunde Kamati teule tuone CAG aliagiza nini, nini kimefanyika na hatua gani zinapaswa kuchukuliwa. Sote tunafahamu watumishi wa umma kuna shida hawa watu wameshakuwa sug. Tumepita Kamati ya TAMISEMI tunawasikiliza Mkurugenzi kwenye Halmashauri hata kujumlisha Hesabu zinawashinda" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai.

"Kamati imefanya uchambuzi wa kina na kujiridhisha kutokuwepo kwa ufanisi wa utendaji wa Wakurugenzi. Kama watu hawana ufanisi maana yake wameshindwa kazi. Tumeenda Iringa kuangalia soko ni aibu ni kilio" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai.

"Mtu anapewa Shilingi Trilioni 1.2 aende akajenge madarasa, pesa amepewa keshi, tengeneza ramani wewe, tengeneza mpango wa ujenzi wewe, tengeneza visibility wewe. Unaenda kujenga Madarasa hayakamiliki. Kama siyo makusudi, hila na mpango mbaya wa kumuhujumu Mheshimiwa Rais ni kitu gani?" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai.

"Tulikuwa Mbeya kukagua miradi ya Elimu, nilijikuta nimesema hivi kwanini hawa watu wasipigwe risasi, inafika mahali unaona hujuma kwa Mheshimiwa Rais" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai.

"Kwenye Elimu, TAMISEMI wamepewa Trilioni 1.2, wamepewa fedha za BOOST Trilioni 1.15, Fedha kwaajili ya Vyoo Bilioni 230, haijawahi kutokea. Hawa watu wamechanganyikiwa wanadhani fedha ni za kwao. Nendeni mkachukue hatua, kwenye Utumishi wa Umma kuna jambo la kufanya" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo Hai.

"Turudini kwenye utaratibu, Kanuni za Kudumu, za Utumishi wa Umma namna ya upatikanaji wa Wakurugenzi imeelezwa. Awe amefanya kazi miaka 12, awe na uzoefu. Tunashauri turudi kwenye Sheria" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai.

 

Kwamaana nyingine Bwana Mafuwe anamwambia Rais na mwenyekiti wake wa Chama aache kuzikanyaga taratibu na afuate sheria?

Haya ndio mambo akina Mbowe wamekuwa wakiyasema na mnawaona wapuuzi kwakuwa hao wakurugenzi ndio wanawatangaza washindi wa ubunge wenu usio na maana yeyote kwa Watanzania.
 
Back
Top Bottom